Kuwe na elimu ya uandishi wa habari kuanzia shule za msingi

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
657
Habari?

Kutokana na hali ilivyo sasa ya teknolojia ya habari na mawasiliano, nashauri wahusika waweke somo la UANDISHI WA HABARI kwenye mitalaa (mitaala) kuanzia elimu ya Msingi angalau kwa kiwango fulani iwe ni LAZIMA kwa kila mwanafunzi afikie.

Hii itasaidia sana kwa watu wengi wanaotoa habari hususani kwa njia za mitandao kutokiuka maadili ya uandishi kwa kutokujuwa.

Nawaailisha.
 
Uandishi wa habari ni taaluma na siyo somo kama jiografia. Mwishowe mtataka hata udaktari ufundishwe kuanzia chekechekea...
 
mkuu sisi tunavunja sheria tu, ili uandike habari inabidi uwe na degree ya Mass communication. nakumbuka malalamiko ya enzi zioe mswaada wa habari ukipingwa na wadau mbalimbali.
 
Uandishi wa habari ni taaluma na siyo somo kama jiografia. Mwishowe mtataka hata udaktari ufundishwe kuanzia chekechekea...
Nukta yangu ni kwamba sehemu ya taaluma hiyo (mfano kipengele cha maadili) yaanze kutolewa kuanzia elimu ya msingi.

Hata udaktari (MD) angalia vizuri, kuna sehemu mafundisho yake yapo kuanzia elimu ya msingi.

Hoja siyo watu wote wawe waandishi wa habari bali hali halisi ilivyo sasa watu wengi wanaandika habari na wengi wao hawajui maadili ya uandishi.
 
Nakubaliana na wewe, hata Uanasheria pia ni taaluma, lakini bado haizuii wanafunzi wa shule za msingi kufundishwa baadhi ya sheria, mfano Sheria za usalama barabarani angalu kwa kiwango cha uelewa wao.

Nukta yangu kubwa ilikuwa hii hali ilivyo sasa na simu hizi sa kisasa (smartphones) "automatically" zimewafanya watu wengi kuwa watoa habari kwa jamii kupitia mitandao ya kijamii...

Kukiwa na elimu hiyo tangia msingi kutaepusha sana 'makosa' ya uvunjaji wa sheria ama maadili ya uandishi HATA KAMA WAO SIYO WAANDISHI RASMI WA HABARI lakini ukweli ni kwamba wanaifanya kazi hiyo kwa namna fulani.
Uandishi wa habari ni taaluma na siyo somo kama jiografia. Mwishowe mtataka hata udaktari ufundishwe kuanzia chekechekea...
 
Back
Top Bottom