Kuwashwa mwili unapopigwa na jua

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
Habari wanajamvi?

Mimi nina tatizo naomba msaada wa ushauri.
Mimi ni mfanyakazi katika kampuni flani hapa mjini Zanzibar. Kazi zangu hazihusiani na ukaaji wa kwenye jua.

Sasa nimekuja kujigundua nina tatizo kila ninapokaa kaa,kutembea au kufanya shughuli zangu binafsi juani.

Kama jua likinipiga zaidi ya dakika 10 nawashwa sana na ngozi.nijikuna sana hata mbele za watu na muwasho wake hauvumiliki.lakini cha kushangaza sipati vipele,uvimbe wala harara yeyote.

Kuna siku jua lilinipiga sana usoni ngozi ya shavu ikajikunja kama nimeparalaizi.

Nilikwenda hospital pale agha khan morogoro wakaniambia sina tatizo pia Global zanzibar(turkish hospital)wakasema sina tatizo.

Naona kwa sasa tatizo linazidi.wajuvi wa magonjwa kama haya naomba msaada wenu tafadhal nakosa raha
 
Mm pia ninalo ila nkjkuna sana hutokeza vipele vyekundu na hupotea dk kadhaa mbele
 
Mi nilisumbuka sana na hii hali nimeona huu uzi adi nimesisimuka mwili mzima nimepuma damu tena hosptal kubwa ,dah! Sitaki kukumbuka hii hali natambea atua 10 mwili mzima nasikia nachonywa baada ya dakika vipele mwili mzima nikikaa pemben kdg hali inaisha kbsa dah! Dawa nilitumia sana ila nitakushauri tu usitumie vinywaji vya sukari kwanza katika hali hii acha kbs natafuta card la hosptal nikipata nitakutumia bro!
 
Mi nimeepuka kutembea juani
 
Mimi pia nilipata hili tatizo na nikapata dawa za msabato mmoja hivi nikirudi home nitatuma mawasiliano,nashukuru Mungu niko poa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom