Kuwashwa baada ya kutoka kuoga

Truth Teller

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
1,165
2,000
Habari zenu wakuu, matumaini mnaendelea vyema.

Hivi inakuaje mtu akitoka kuoga huwa anawashwa? Majua mtasema maji au sabuni lakini HAPANA. Unakuta mtu kama hatoga kwa siku 3 au 2 akija kuoga atawashwa. Hii imekaaje?

Unakuta anaweza chukua kama dakika 15/30 akawa anawashwa na mbaya zaidi endapo akajikuna muwasho unazidi lakini kama ataupotezea kukuna basi muwasho utapungua taratibu.

Naomba majibu wakuu
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,131
2,000
Acha kula chips

Oga kila Siku asubuhi na jioni

Kama ulizoea mazoezi usiache kufanya, ukikaa Muda mrefu ukianza tena utawashwa mpaka mwili uzoee

Punguza kula kula hovyo hasa Usiku
 

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
2,926
2,000
Hayo ya kuto oga sifahamu lakini kama unawashwa mara kwa mara Vinyoleo huchangia hali hiyo.

Source: Mimi, Morata na Chama cha Madaktari Ulimwenguni.
 

Dinnah

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
804
1,000
ni allergy ambayo inawapata baadhi ya watu kutokana na mazingira hata mm ninayo hiyo

mf ukiishi sehemu za joto kama dar
nikioga maji ya kisima au kujifutia nguo mbichi, au ukitoka kuoga ukagusana na kitu, mazingira yakiwa machafu au ukashika maji ya baridi huenda nawe katika haya lipo linalosababisha hali hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

bardizbah

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
2,605
2,000
ni allergy ambayo inawapata baadhi ya watu kutokana na mazingira hata mm ninayo hiyo

mf ukiishi sehemu za joto kama dar
nikioga maji ya kisima au kujifutia nguo mbichi, au ukitoka kuoga ukagusana na kitu, mazingira yakiwa machafu au ukashika maji ya baridi huenda nawe katika haya lipo linalosababisha hali hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswa

Nyongeza
Hii sana sana hutokana na baada ta kubadilisha mazingira na maji ya tofauti na yale ulioyazoea kuoga
 

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,272
1,500
Hata mimi nina hilo tatizo, nimejaribu kila sabuni, ila nikitumia maji ya moto kidogo nkuna nafuu
Hii shida iliwahi kunipata kwenye mwaka 2000, mwanzoni nilidhani kuwa bafuni kulikuwa na wadudu warukao ambao huenda waliniuma lakini hali hiyo iliendelea hasa nilipooga maji ya mvua na nikajisugua kwa dodoki. Na endapo nilioga maji ya moto mwasho ulipungua, nimeendelea hivyo mpaka miaka ya karibuni ndo naona hali hiyo kupungua kwa kiasi kikubwa.

Hiyo shida inakera sana kiasi kwamba mtu akija kukusemeshasemesha wakati wa mechi ya kuwashwa wawezamjibu vibaya kutokana na maumivu ya mwasho kwa wakati huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom