Mwanamke unapolipiwa mahari ujue umebadilishwa ukoo. Kupewa misaada ni hisani na maadili ya mume, lakini sio shuruti. Kwenu kama kuna watoto wakiume limekuwa ni jukumu lao kuitegemeza familia yenu, sio wewe muolewaji. Hakuna hadidu za rejea kwenye ndoa kuwa mume atahakikisha anafuta umaskini wa ukoo wa mke, hazijawahi kuwepo.Ndungu kwa lawama hawajambo yaan wanataka kuona upande mmoja ukae maskini nisijenge kwetu wakati pesa mnatafuta kila siku umefanya vizuri sanaa
Mwanamke unapolipiwa magari ujue umebadilishwa ukoo. Kupewa misaada ni hisani na maadili ya mume, lakini sio shuruti. Kwenu kama kuna watoto wakiume limekuwa ni jukumu lao kuitegemeza familia yenu, sio wewe muolewaji. Hakuna hadidu za rejea kwenye ndoa kuwa mume atahakikisha anafuta umaskini wa ukoo wa mke, hazijawahi kuwepo.
Hahahahahahaah hingera mkuuNamshukuru Mungu nilipooa wanajiweza na niliyemuoa hategemewi na mtu
Mnaongea na mumeo, anafanya awezalo. Sio formula ya ndoa, ni kutegemea nafasi aliyonayoYaan pesa ipo nisijenge kwetu na naitafuta wewe mi nalala pazuri mama yangu analala pabaya wewe
ThanksOne in million mzee...
Usimuache halafu bora wewe una shukrani na unajua mchango wa mke wako,hi ni good story kushare..
Kwenu sijui mmelelewaje lakini mdogo wangu au mama angu hana uwezo wa kumtukana mke wangu.Toka nakuwa niliweka wazi msimamo wangu kwa mama na ndugu zangu kwamba mimi nina maamuzi binafsi ingawa napokea ushauri ila sipangiwi cha kufanya...Na ndo tunaishi hivo mimi na ndugu zangu Ila hii ya mdogo wako kumtukana mke wako aiseeee mpenzi tu kingewaka motoooo
Anyway maroho yao hayo ya kijinsia ndo yanawasumbua..shukuru mke wako muelewa ungekuta Ana mdomo sasa
sidhani kama dina anakuelewa kama amejiandaa kubishaMnaongea na mumeo, anafanya awezalo. Sio formula ya ndoa, ni kutegemea nafasi aliyonayo
Umwezeshe, heros are madeAiiise na mimi nina kichaga changu ni kiform four leaver sijui kitakuwa kama mke wako
huyo mwanamake alikuwa na akili tangu muda tangu jamaa hajamuoaUmejitahidi kutunga mkuu, ila tu mama yako alikuwa sahihi. Pia wewe una tatizo, kujiita huna akili. Unapotoa pesa kuongeza mtaji ni akili, unapomsapoti mkeo ni akili. Halafu kujiita kuwa eti huna kitu wakati wewe ndio mtoa mtaji sio sawa. Wewe ni baba wa mji, utabaki hivyo, ili siku akikengeuka mkeo uwe na nguvu ya kusimama kwenye nafasi yako. Suala la ndugu ni kawaida, ingawa wengi mmekimbilia kuwashutumu. Wanachofanya ni kukulinda, kwa kuwa ukoo unajengwa na upande wa mume, si vinginevyo unless ni ndoa ya kuku wa kisasa. Wapo wanaume wengi wametekwa fikra na wake zao na kujikuta wakiumizwa baadaye, ndio tu sababu ya familia yako kujaribu kukudodosa, ni kukulinda usitekwe. Ilikuwa jukumu lako kuwaelewesha taratibu bila kutumia ubabe huo unaotambia mtandaoni. Hivi mfano siku mambo yakienda kombo uhusiano ukafa, utakuwa na nani wa kukuokoa? Au ndio umehama ukoo kabisa!!
Nikuulize tu, huyo mkeo alisubiri umuoe ndio awe na akili hiyo? Maana kama ukimpa laki moja tu anatajirika, alitoka familia duni kiasi gani? Ummejitahidi kutunga mkuu. Ila kuwa mume, usimpinge huyo mkeo, muunge mkono, usiuze nafasi yako kwa ajili ya kunde kama Esau.
Wale waliopewa limbwata na wake zao wataendelea kuusapoti huu uzi aloandika huyu alopewa limbwata,Ndungu wana Jamvi nimeleta kwenu uzi huu ili tuweze kuuchambua, natumai humu wamo walioowa na wanaotarajia kuoa. Hapa utajifunza
Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.
Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.
Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.
Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;
“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”
Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.
Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”
Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.
Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!
NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatulia
Sijui ndugu huwa mnamatatizo gani hasa wadada
Ndungu wana Jamvi nimeleta kwenu uzi huu ili tuweze kuuchambua, natumai humu wamo walioowa na wanaotarajia kuoa. Hapa utajifunza

[/QQUnimekuelewa vzr Cha muhimu hapo tumia Sana akili kubalance huo mgogoro usiwajie Sana juu nduguzo ma mama yako hata kama wanamatatizo kiasi gani Bado huwezi kulinganisha walipokutoa ndugu na alipokutoa mkeo wape heshima yao,na jishushe kwa mama ako kaa tu chini na mkeo muambie Hawa ni ndugu zangu tuwavumilie
Sasa ulitaka aombe nani na wewe jamaa ndo mwanaume sasa sio kusikiliza ndugu kuua ndoa yake
Even if hao ni nduguzo wavumilie tu usiwadhalilisheMama aliombea watoto sio matumizi yake yeye,
🙏🙏🙏 Kinachonipa woga inaonyesha jamaa Hana kauli kwa mkeweHapana mkuu, ni mchango wangu tu. Naangalia nafasi za wote wawili.
mama aliyemlea na kumsomesha hata kufika chuo kikuu na akapata mtaji wa kumpa mkewe na mke aliyemsaidia katika maisha. Wote ni muhimu lakini pia kama mwanaume ajue ku-handle situation bila kusababisha mgawanyiko