Kuwasaidia ndugu wa mkeo ni limbwata?

Ndungu wana Jamvi nimeleta kwenu uzi huu ili tuweze kuuchambua, natumai humu wamo walioowa na wanaotarajia kuoa. Hapa utajifunza


Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.

Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!

NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatulia

Sijui ndugu huwa mnamatatizo gani hasa wadada
Hongera sana mkuuu kwa kuona kitu kikubwa alichonacho mkeo sio wanaume wote wenyemacho ya kuona kitu anachofanya mkewake na kumsifia na kumpa sapoti

Kaka nakupongeza kwa kuwaeleza ndugu zako ukweli,sio wote wanaliweza hukooo

Kuna wanaume wengine hukaa sebleni na ndugu zake na kumsema vibaya mkewake na haongei kitu yuko kimya tuu
 
Mosi ulimuinterview (pale bank)
Pili ukamuamini (kuamua kumuoa)
Tatu ukampa nafasi ya kuprove kile kilichomo ndani yake (fikra zake)
Nimekubali mbinu zako
 
Umeongea ukweli kabisa mkuu, wanaume wengi walopata mafanikio baada ya kuoa ni kwasababu ya wake zao. Basi tu huwa hawasemi.
Hongera sana kwa kujitambua na kusimama na mke wako, wasipokuelewa sasa hivi ipo siku watakuelewa tu.

Ila wanawake wa kichagga ni noma kwenye mambo ya kusaka pesa, na ukimpata alietulia ni walezi wazuri sana wa familia.
 
Hongera, yote kwa yote upande wa mkeo ndo unaonekana kuwin

Umejitutumua kutonyesha umefaulu kuwatisha ndugu zako ila ukweli ni kuwa huna power Tena juu ya nyumba yako.
 
Wewe mbona kama shemeji mtu? Comment yako imejaa chuki hivi
Hapana mkuu, ni mchango wangu tu. Naangalia nafasi za wote wawili.
mama aliyemlea na kumsomesha hata kufika chuo kikuu na akapata mtaji wa kumpa mkewe na mke aliyemsaidia katika maisha. Wote ni muhimu lakini pia kama mwanaume ajue ku-handle situation bila kusababisha mgawanyiko
 
Back
Top Bottom