Kuwafukuza uanachama Wanawake mashujaa 19 ni kujipiga risasi mguuni

Mangisandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,652
2,272
Chonde chonde kamati kuu ya CHADEMA, huu mtego utegueni kwa hekima.

Kuwafukuza wanawake 19, au 20, ambao Ndio Wanawake imara na wenye nguvu zaidi nchini kwa sasa, siyo tu kujipiga risasi mguuni, ni kumpa adui nafasi ya kujilinda na kukushambulia.

Sisiemu wana pandikiza mapandikizi kila leo, wale kina ‘Mamvi’, mzee ‘gusa unuke’, nk! Kwanini tusiwachezee mchezo wao huo huo? Unapata wapi fursa nyingine kama hii? Naomba suala la wamama tulimalize, alafu watu kadhaa vichwa kama Mnyika, na Catherine Ruge waunge juhudi mkono, waende jikoni mle, wakatulee mbinu. Kwa nini tutegemee njia moja tu? Huyu adui tunatumia njia hiyo tangu 1995, na tunapigwa? Ok, Lisu na Lema wamekimbilia uhamishoni, ni mbinu lakini isiwe ya mwisho.

Wacha watutukane, watubeze na kutudharau, lakini mwishoni tuwatoe madarakani! Lengo lao chama kisambaratike na kufa, lakini sisi tuamue kusambaratika na kuishi!

Kesho tokeni na agenda ya kukivunja vunja chama, Kama kawaida Mwamba Mbowe abebeshwe lawama ya kawaida ya kupenda ruzuku, kuwa ameteua 19 peke yake, alafu wajumbe wengine wakuu wajivue uanachama, waunge juhudi waingie Serikalini, ‘kimafia’ tufe ili kuishi, sambaratisha chama kiingie kila uwanja wa vita.

Kila tutakapo ingia tueneze u-CHADEMA wetu, kama Wakristo wanavyoeneza Ukristo wao China, chini kwa chini, tusitake mafanikio ya mda mfupi tu, tujipangeni ‘kimafia’ kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu.

Ni maoni yangu lakini nitaendelea kuunga mkono upinzani kwa hali na mali, hata kama ushauri wangu hautafuatwa.
 
Siyo kweli! CHADEMA imepita kwenye mitihani mingi mno lakini bado ni imara kabisa.Kwa sababu bado kinaaaminika kwa wananchi kama chama mbadala wa CCM.
Na wananchi wanajua kabisa kwamba kimehujumiwa katika uchaguzi huu na wanajua hujuma zinaendelea.

Kama kimefungiwa miaka mitano bila kufanya mikutano wala siasa zo zote lakini kikaishangaza CCM na ulimwengu kwa jinsi ambavyo kwenye kampeni wananchi walikuwa nyuma yake sina hakika kama chama hiki kitakufa! Bado Mungu ana makasudi nacho.
 
Chonde chonde kamati kuu ya CHADEMA, huu mtego utegueni kwa hekima. Kuwafukuza wanawake 19, au 20, ambao Ndio wanawake imara na wenye nguvu zaidi nchini kwa sasa, siyo tu kujipiga risasi mguuni, ni kumpa adui nafasi ya kujilinda na kukushambulia!

Sisiemu wana pandikiza mapandikizi kila leo, wale kina ‘Mamvi’, mzee ‘gusa unuke’, nk! Kwanini tusiwachezee mchezo wao huo huo?! Unapata wapi fursa nyingine kama hii!? Naomba suala la wamama tulimalize, alafu watu kadhaa vichwa kama Mnyika, na Catherine Ruge waunge juhudi mkono, waende jikoni mle, wakatulee mbinu! Kwa nini tutegemee njia moja tu? Huyu adui tunatumia njia hiyo tangu 1995, na tunapigwa?! Ok, Lisu na Lema wamekimbilia uhamishoni, ni mbinu lakini isiwe ya mwisho!

Wacha watutukane, watubeze na kutudharau, lakini mwishoni tuwatoe madarakani! Lengo lao chama kisambaratike na kufa, lakini Sisi tuamue kusambaratika na kuishi!

Kesho tokeni na agenda ya kukivunja vunja chama! Kama kawaida Mwamba Mbowe abebeshwe lawama ya kawaida ya kupenda ruzuku, kuwa ameteua 19 peke ake, alafu wajumbe wengine wakuu wajivue uanachama, waunge juhudi waingie serikalini, ‘kimafia’!! Tufe ili kuishi, sambaratisha chama kiingie kila uwanja wa vita.

Kila tutakapo ingia tueneze u-CHADEMA wetu, kama Wakristo wanavyo eneza Ukristo wao China, chini kwa chini! Tusitake mafanikio ya mda mfupi tu, tujipangeni ‘kimafia’ kwa ajili ya mafanikio ya mda mrefu!

Ni maoni yangu lakini nitaendelea kuunga mkono upinzani kwa khali na mali, hata kama ushauri wangu hautafuatwa!
Watanzania wanazaa vijana mashuhuri kila leo katika watanzania milioni 60 umeona wanawake imara 19 tu ?

Je wakifa ina maana na chama na chenyewe kinakufa ?

Wakiacha siasa na chama na chenyewe kinakufa ?

Wakihamia vyama vingine na chama na chenyewe kinakufa?

Hebu acheni utoto
 
Chonde chonde kamati kuu ya CHADEMA, huu mtego utegueni kwa hekima. Kuwafukuza wanawake 19, au 20, ambao Ndio wanawake imara na wenye nguvu zaidi nchini kwa sasa, siyo tu kujipiga risasi mguuni, ni kumpa adui nafasi ya kujilinda na kukushambulia!

Sisiemu wana pandikiza mapandikizi kila leo, wale kina ‘Mamvi’, mzee ‘gusa unuke’, nk! Kwanini tusiwachezee mchezo wao huo huo?! Unapata wapi fursa nyingine kama hii!? Naomba suala la wamama tulimalize, alafu watu kadhaa vichwa kama Mnyika, na Catherine Ruge waunge juhudi mkono, waende jikoni mle, wakatulee mbinu! Kwa nini tutegemee njia moja tu? Huyu adui tunatumia njia hiyo tangu 1995, na tunapigwa?! Ok, Lisu na Lema wamekimbilia uhamishoni, ni mbinu lakini isiwe ya mwisho!

Wacha watutukane, watubeze na kutudharau, lakini mwishoni tuwatoe madarakani! Lengo lao chama kisambaratike na kufa, lakini Sisi tuamue kusambaratika na kuishi!

Kesho tokeni na agenda ya kukivunja vunja chama! Kama kawaida Mwamba Mbowe abebeshwe lawama ya kawaida ya kupenda ruzuku, kuwa ameteua 19 peke ake, alafu wajumbe wengine wakuu wajivue uanachama, waunge juhudi waingie serikalini, ‘kimafia’!! Tufe ili kuishi, sambaratisha chama kiingie kila uwanja wa vita.

Kila tutakapo ingia tueneze u-CHADEMA wetu, kama Wakristo wanavyo eneza Ukristo wao China, chini kwa chini! Tusitake mafanikio ya mda mfupi tu, tujipangeni ‘kimafia’ kwa ajili ya mafanikio ya mda mrefu!

Ni maoni yangu lakini nitaendelea kuunga mkono upinzani kwa khali na mali, hata kama ushauri wangu hautafuatwa!
Ushujaa wameupata wakiwa chadema, namaanisha Chadema imeatengeneza, pia naamini wapo wengi na watakaokuwa bora kuliko hao. Natamani wafukuzwe leo, ili wengine wapate nafasi. Huwezi kuwanyamazia wasaliti eti umaarufu wao. Ccm kuna watu Walipingana na miongozo ya chama walifukuzwa, unakumbuka akina mama sita. Wafukuzwe alafu kama inawezekana wateuliwe wengine, hao wafikishwe mahakamani kwa kughushi nyaraka za chama
 
Tatizo ni kwamba hata ukiwafukuza, ccm watakingia kifua na wataendelea kuwa bungeni!
 
Watu lazima waheshimu taratibu zilizowekwa; chadema iwafukuze haraka sana hao wanawake. Wajukuu wetu watakuja kujenga chama.

Tena msamahaa wowote usitolewe;
Ni bora kuanza upya kulisuka baraza la wanawake kuliko kuvumilia usaliti wa kiwango hicho! Wakiachwa,next time wanaweza kufanya makubwa zaidi ya hayo!

Swali la Msingi:Kwa Serikali na Bunge,mmeahidiwa nini na akina Halima Mdee mpaka mkashiriki kuwawezesha kuapishwa bila taratibu za kikatiba kufanyika?Mmewapa masharti gani akina Mdee?

Sio afya kwa chama kukaa na hao wanawake wasaliti!
 
Kuwafukuza sio jawabu la matatizo, tatizo ni mfumo unaozaa huo unaoitwa usaliti, lazima kila siku mtakuwa na wasaliti. Yawezekana mfumo upo ndani ya chama au nje ya chama.
 
Back
Top Bottom