Kuwaasi wazazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwaasi wazazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Nov 14, 2009.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  KUWAASI WAZAZI

  Baada ya dhambi ya ushirikina; kusema/kuitakidi kuwa kuna Mungu zaidi ya mmoja, dhambi kubwa kuliko zote ambayo Mwenyezi Mungu anasema: "HAKIKA MWENYEZI MUNGU HASAMEHI KUSHIRIKISHWA; NA HUSAMEHE YASIYOKUWA HAYA KWA AMTAKAYE. NA ANAYEMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGU BILA SHAKA AMEBUNI DHAMBI KUBWA". [4:48] Dhambi inayoifuatia hiyo na kushika nafasi ya pili ni kuwaasi/kutokuwatii wazazi. Kutowatii wazazi ni uovu/munkari ambao muislamu mkweli/mkamilifu wa imani hawezi hata kuufikiria au kuuwazia.

  Shukrani, wema na mwenendo mwema ni sifa kuu tatu zinazompa mtu sifa ya utu/ukamilifu. Mtu asiyeweza kujikusanyia na kuzihodhi sifa tatu hizi, utu wake hauwezi kukamilika. Mtu kama huyo ni nadra mno kuweza kupata rehema za Mwenyezi Mungu, kwa sababu hawezi kutekeleza wajibu wake kwa Mwenyezi Mungu Mola Muumba wake wala wanadamu wenziwe. Kwa maana hii basi, waislamu walio watiifu kwa Mwenyezi Mungu hawawezi abadan kuwaasi na kutokuwajali wazazi wao.

  Sayyidina Abu Bakarah ( Nafei Ibn Haarith)-Mungu amuwiye radhi-anasimulia kwamba siku moja Mtume wa Mungu-Rehema na Amani zimshukie-aliwauliza je, nisikuambieni juu ya dhambi kuu tatu? Wote kwa pamoja wakajibu: Kwa nini (usituambie), tuambie ewe Mtume wa Mungu! Mtume akasema: "Kumshirikisha Mungu, kuwaasi wazazi". Akainuka akakaa sawa kwani alikuwa ameegemea, akasema: "Kusema uongo au kutoa ushahidi wa uongo". Aliendelea kuyakariri maneno yake hayo kwa kitambo ambacho tulitamani anyamaze (kwa kumuhurumia)".

  ii.Waraka wa Mtume wa Mungu kwa watu wa Yemen:


  Ndani ya waraka (barua) muhimu mno waliotumiwa watu wa Yemen na Mtume wa Mungu-Rehema na Amani zimshukie-kupitia kwa swahaba wake Amrou Ibn Hazim-Mungu amuwiye radhi. Mtume Muhammad SAW aliwaonya juu ya dhambi zifuatazo:


  1.kumshirikisha Mungu,
  2.kumuua asiye na hatia,
  3.kukimbia katika jihadi,
  4.kuwaasi wazazi,
  5.kuwasingizia machafu wanawake wacha-Mungu,
  6.kujifunza sihiri (uchawi),
  7.kula riba na
  8.kudhulumu mali ya yatima".

  iii.Ushauri wa Mtume wa Mungu kwa uma:


  Sayyidina Muadh Ibn Jabal- Mungu amuwiye radhi-alikuwa ni miongoni mwa maswahaba mashuhuri wa Mtume wa Mungu-Rehema na Amani zimshukie. Sayyidina Umar; khalifa wa pili wa Mtume wa Mungu - alikuwa akisema kuwa bila Muadh kuangamia kwake kulikuwa ni dhahiri. Mara kwa mara Sayyidina Muadh alikuwa akipewa nasaha na Mtume wa Mungu, siku moja Mtume alimnasihi:

  "Kamwe usimshirikishe Mungu hata kama utauawa au kuunguzwa hai. Na katu usiwaasi wazazi wako hata kama watakuamuru kuitupa mali yako au kuiacha familia yako (mkeo)".


  iii.Kuwatukana wazazi:

  Sayyidina Abdullah Ibn Amrou-Allah amuwiye radhi-alimsikia Mtume wa Mungu-Rehema na Amani zimshukie-akisema: "Kuwatukana wazazi pia ni miongoni mwa madhambi makubwa". Watu waliokuwepo pale wakauliza kwa mshangao: "Ewe Mtume wa Mungu! Mtu anawezaje kuwatukana wazazi wake mwenyewe?", Mtume akajibu: "Naam (anaweza), wakati mtu anapomtukana baba wa mwenziwe, kwa kurudishia huyo mwingine nae atamtukania baba yake. Atamuita jina baya mama wa mwenziwe, nae atamrudishia kwa kumtukana mama yake".

  Hivi ndio kusema kuwa kumtukana mzazi wa mwenzio ni sawa kabisa na kuwatukana wazazi wako mwenyewe. Kwani utakapomtukania wazazi wake, kisilka nae hatakubali ila awatukane wazazi wako, kwa hiyo ni wewe ndiye utakayekuwa umesababisha wazazi wako kutukanwa. Ili kuliepuka hili, basi hakikisha kuwa huutumii ulimi wako kuwatukana wazazi wa wenzio. Leo hili ni suala lisilopewa umuhimu mkubwa, mtu haoni vibaya kufanya jambo au kutamka neno litakalosababisha kutukaniwa wazazi wake. Katika kisa mashuhuri cha Israa na Miiraji tunasoma: "Kisha (Mtume) akapandishwa mpaka Mustawaa akasikia (hapo) sauti ya mkokoto wa kalamu. Na akamuona mtu amezama katika nuru ya Arshi. (Mtume) akauliza: "Huyu ni nani, je ni malaika?", akajibiwa: Hapana. Akauliza (tena): "Je, ni mtume", akajibiwa: Hapana. Akauliza (mara ya tatu): "Ni nani huyu basi?", akajibiwa: "Huyu ni mtu alikuwa duniani (siku zote), ulimi wake laini kwa (wingi wa) kumtaja Mungu. Na moyo wake ulikuwa umefungamana na misikiti, wala katu hakupata kuwatukanisha wazazi wake". Hizo ndizo fadhila na daraja adhimu za mtu atakayejiepusha na dhambi hii ya kuwatukanisha wazazi wake.
   
 2. M

  Mandago JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 238
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Asante ndugu Mahmoud Kwa post yako hii nzuri sana.
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  no comment!
   
 4. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Thank you.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Shukran na Mola atujaalie tuwe wenye kusikia maneno kufuata njia sahihi.
   
 6. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Thank you mahmoud.
   
 7. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Amin
   
Loading...