Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Kuku-kupatana.jpg

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
Aksante kwa madini haya yamenihamsha akili
 
Maboresho kidogo ya uzi,
1. (Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300) si kuku 10 bali ni kuku 11 hivyo ni gramu 1430 kwa chakula chetu kitatupeleka tabribani siku 95.

2. (Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240) wastani wa hutagaji kwa kuku wa kienyeji nahisi kuna shida sina uhakika na utagaji wa zaidi ya siku 15, naomba ufafanuzi kwa hili? Matarajio yangu ni mayai 120-180 kwa mwezi.
 
Mtoa mada nakuunga mkono!! Kuna fursa kwenye kwenye ufugaji pamoja na kwamba mambo yanaweza yasiende sawa kama ulivyoandika maana haujaconsider risk
 
>Kuku wa kienyeji kufika uzito wa kuweza kuuzwa ni miezi 8 hadi 12.

>Kuku wa kienyeji uwa hatagi kila siku na ni wachache sana wanaweza taga hata mayai 20 katika mzunguko mmoja.

>Kuku wa kienyeji uwa anapumzika kutoka mzunguko mmoja wa kutaga hadi mwingine.

>Utunzaji wa vifaranga bila kutumia mama kuku una gharama mf chanzo cha joto, madawa, chanjo.

>Kuku wa kienyeji hata akiwa anakula chakula cha kuku wa kisasa ukuwaji wake ni ule ule kulingana na mfumo wake wa vinasaba

>Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara una changamoto nyingi sana ndio maana ni kazi sana kumkuta mtu mwenye kundi la kuku hata mia tatu wa kienyeji.

>Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara una changamoto sana ndio maana miradi yote ya kufanya ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara lazima uje na mpango wa kuboresha ufugaji kwa kuingiza kuku chotara. Mfano RLDC na RIU

Taarifa:
Mwaka wa 8 huu nipo ktk ufugaji wa kuku, hakuna changamoto ambayo sijakutana nayo na sijafika hata robo ya ndoto yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni simple kulingana na eneo husika mfano iringa upatikanaji wa maeneo ni rahisi unaweza pata hata ekari 1 kwa 250,000 na karib na mjini pia materials kama mabanzi ni sawana bure tuu!! Kwa sehem nyingine ni tofauti so inayofautiana kulingana na sehem uliyopo!
Sasa Iringa utamuuzia nani kuku 18000?
 
be
i ya jumla ni 8000 braza
Yaani kilimo bwana ndo hapo kinapokuwaga kitamu. Wewe ushahangaika ukapiga hesabu ila mnunuzi akija anakupangia bei. Mbona kwenye nyanya mwaka jana wanunuzi walichemka, mpaka yule jamaa wa Iringa akavuna milioni 400 ndani ya mwezi mmoja!
 
Ila we jamaa ni muongo au hujawahi fuga kuku wa kienyeji.
Yani kuku kumi tu kwa siku uokote mayai nane 🙄. Mi nafuga kuku zaidi ya Mia wa kienyeji na sijawahi okota mayai 50 toka nimeanza kufuga mwaka 2014.
Nyie ndo huwa mnafanya watu wanaingia wanatupangia Bei za kununua mayai or kuku kwa kudhani tunavuna Sana kumbe wenzetu mnafugia kwenye madaftari🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom