Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,956
KUWA MKE MWENYE MAFANIKIO KATIKA NDOA:
Ama katika kukupa njia za ziada za kulifikia lengo la kuwa mke bora, ninakushauri uzingatie nukta zifuatazo.
1. Maelewano baina yako na mume wako na kutumia lugha nzuri unapozungumza naye.
2. Kusamehe makosa yake na kutoyakuza mambo madogo madogo.
3. Kutomchunguza chunguza mume kupita kiasi. Ukaanza kumfuatilia anapoingia na kutoka.
4. Kuwa makini sana na unadhifu wa nyumba na mavazi pamoja na kutofanya khiyana dhidi ya mali za mumeo.
5. Kutumia manukato mazuri na kuvaa mavazi nadhifu na yenye kupendeza kwa ajili yake, sio mavazi ghali.
6. Kumuonesha upendo na shauku kubwa ya kuishi naye daima, hilo litamfanya akupende na kuwa na imani na wewe.
7. Kumuuliza kuhusu wasiwasi zinazomkabili na kumtaka akufunulie yaliyo moyoni mwake kama anataka kufanya hivyo, lakini usimlazimishe wala kumkasirisha kama hataki kukwambia siri zake.
8. Kuwa mwema na usiyekuwa na makuu kwa ndugu na jamaa zake.
9. Kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kila hali na kutokasirika au kuhuzunika unapokumbana na tabu na shida mbalimbali.
Pamoja na hayo niliyokuambia, kumbuka kuwa ushuri huo utazaa matunda ikiwa utazitekeleza tunu hizo kwa moyo mmoja bila kujiongopea.
Ninakutakia mafanikio mema