Kuwa milionea sio ndoto

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Kama unataka kuwa milionea badilika ufwate mfumo huu wa maisha​
Ni furaha kila unapo pokea mshahara au ujira wowote baada ya kazi Fulani, lakini kila ukitazama idadi ya madeni yanayokusubiri unaweza kupata kichaa, kwani unaweza ukagawa pesa hiyo na usibaki na shilingi ama la unabaki na pesa ya nauli na chakula, lakini nini cha kufanya kujiongezea kipato, watu ambao ni mamilionea hufanya mambo haya yafwatayo.

1459145660x3738746583.png

Jipangie Bajeti na Mpango wa kifedha

Ili uendelee lazima ujue, unatumia nini unaingiza nini? hii itakusaidia pia katika akiba zako na itakusaidia kama utachukulia swala hilo kwa umakini, kama kuna bili za kulipa kila mwezi na lazima uziweke katika mtiririko mzuri wa malipo ili bajeti zako siziingiliane na akiba zako wala matumizi yako binafsi.

Uwe na Vyazo Vingine Vya Kukuingizia Kipato

Hakikisha mshahara wako sio pesa pekee unayoitegemea, lazima utengeneza mifereji mingine ya kukuingizia kipato, fanya kazi mwenyewe kama bosi wa biashara yako au ofisi yako, uza bidhaa zako kwa mitandao ya kijamii, anza kujitangaza taratibu sio lazima uanze na mtaji mkubwa. ukiwa na vyanzo vingi vya mapato ni rahisi kuweka akiba na kuwekeza.

Akiba,Akiba,Akiba weka Akiba

Watu walioendelea waliweka akiba, punguza vitu unavyofanya visivyo vya maana au visivyo na umuhimu, punguza kutoka sana na kutumia pesa kwa starehe, fanya mambo ya muhimu tu acha kununua vitu ambavyo hauvihitaji, anza kwa kuweka akiba ndogo, ukiweka akiba nyingi ndiyo utaweza kuwekeza zaidi. wasichana wengi wanatabia ya kununua vitu wasivyo vihitaji kama viatu vingi,Nguo,Mikoba na vifaa vya Urembo. Jiwekee kiwango cha wastani kulingana na mahitaji yako.

Punguza Matumizi

Watu wengi wakipata pesa kidogo wanakimbilia magari ya bei kubwa na kufanya manunuzi ya vitu vya gharama kama nguo,saa na viatu kwenye maduka maarufu mjini, lakini kama ungetumia pesa kuwekeza katika mambo ya muhimu kama biashara lazima baadae ikulipe kuna usemi mmoja unasema “Buy the best Car but Own the Best House” na usinunue kitu ambacho haukihitaji sababu tu ni bei rahisi,

Kutana na Watu wenye Utaalamu

Kutana na watu walio kuzidi ujuzi,utaalamu na Uzoefu katika Biashara au shughuli unayotaka kuifanya hii itakusaidia kujifunza vitu kutoka kwao tembelea mikutano mbalimbali ya wataalamu na masomo mbalimbali ya muda mfupi kujiongezea utaalamu, jiunge na wafanya biashara au wajasiriamali walio endelea katika kujifunza mambo ya kuhifadhi fedha, kuweka akiba na kuwekeza katika biashara.
 
Mbona tunakuwa milionea kila mwezi na hiyo milioni inayeyuka ndani ya mwezi husika?
 
Mbona tunakuwa milionea kila mwezi na hiyo milioni inayeyuka ndani ya mwezi husika?
naona unatakiwa kubadilika mtindo wa maisha , yaani kukuza tabia nzuri ya kusaving pesa kidogo, na kuepuka kununua vitu visivyohitajika;) Jaribu kwa miezi kadhaa
 
Back
Top Bottom