Kuwa meneja bora wa ICT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa meneja bora wa ICT

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Aug 18, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Post hii imenukuliwa toka AfroIT - Karibu Kijiji cha ICT-Elimika kwenye ICT kupitia E learning,webcast,podcast,blogs,forums na download

  Kipindi nipo chuo kikuu nimewahi kushiriki au kuongoza project mbalimbali za IT na zisizo za IT,kuna baadhi ya project hakuna mtu aliyewahi kudhani kuwa inaweza kufanikiwa,hii ni kutokana na ugumu wake.Kwa kipindi hicho chote nimekuwa nikipata mafunzo mengi ya jinsi gani ya kuwa mamager mzuri sio tu wa IT bali hata nyanza nyingine mbalimbali.Kitu kikubwa sana nilichojifunza ni jinsi gani ya kuchagua watu husika(right people) kwa project husika,jinsi ya kumaliza kazi kwa wakati ndani ya bajeti nk.Kuwa manager mzuri mara nyingi inategemea sana ni jinsi gani unavyoshirikiana na wana member wako.Kitu kikubwa nilichojifunza nikiwa China ni kuwa bosi ataendelea kuwa bosi na mfanyakazi ataendelea kuwa mfanyakazi ila kati yao mahusiano ni mazuri mno,bosi hana kujidai au kudharau walio chini yake,ukiwa nje ya ofisi ya bosi kuna kipindi unaweza usijue nani ni bosi,hawana yale mambo ya mimi ni bosi bwana.Hii inasaidia sana na kuongeza malali wa wafanyakazi.Hivyo basi leo hii nitakupa mambo machache tu ya jinsi gani unaweza kuwa IT manager mzuri.

  1: Sikiliza wafanyakazi wako

  Kitu cha msingi sana ni kuwasilikiza wafanyakazi wako,pata ushauri toka kwao na ufanyie kazi iwezekanavyo.Kwani wao ndio wanaojua hali halisi ya kampuni au project husika.Kuna kipindi niliwahi kuchukua project moja nzito,binafsi nikafungua milango kwa wafanyakazi wote kutoa maoni muda wowote,nikaondoa ukingo kati yangu na wafanyakazi,hivyo nilikuwa napata mawazo mengi mno na tulifanikiwa kuwashinda wapinzani wetu na kuwaacha wakibaki midomo wazi.Epukana na uongozi wa kizamani wa kusema mimi ni bosi bwana,hii iytakufanya utengeneze uhasama na kuondoa molali wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wako. Jamani kumbuka kuwa sio lazima ufuate kila ushauri unaopewa,ila kuwa tarayi kupokea ushauri halafu ufanyie kazi.
  Kitendo cha kuwasiliza wafanyakazi wako kitakusaidia kuwajengea moyo kuwa mchango wetu unathaminika ndani ya kampuni.

  2: Kuwa mwerevu


  Kitu kingine nilichojifunza kama IT manager ni kuwa msikivu,project nyingi za IT huwa zinachukua muda mrefu mno,muda mwingi inalazimika hata kupitisha muda wa kazi,chukulia mfano muanadevelop programu fulani na ghafla kunatokea matatizo kibao,hali kama hii ni kitu cha kawaida kwenye ulimwengu wa IT,hivyo basi unatakiwa kufikiria katika uhalisia wake.Kwa mfano kuna kipindi munatakiwa kufanya kazi zaidi ya muda ila akaja mfanyakazi na kuomba ruhusa anakwenda kupokea mtoto toka shuleni.Kama IT manager lazima uwe mwerevu wa jinsi ya kusikiliza maombi mbalimbali.Hii itasaidia kuongeza ufanisi wa kazi.Ila kumbuka lazima uwe mpambanuaji ili kupunguza mategeo.

  3: Endeleza ufahamu wako


  Kama tumeona mara nyingi maCIO au mameneja wengi hutumia muda mwingi mno kwenye vikao na semina mbalimbali,hii huwafanya kusahau au kutupilia mbali kabisa fani zao au ufahamu wao kiteknolojia(IT).Hawana tena muda wa kuconfigure server au kutatua matatizo ya kiufundi hii huwapelekea kupoteza maarifa ya kiufundi.Kuna sababu zinazoweza kukupelekea wewe kufaidika kutokana na kujiendeleza kiufundi hata kama wewe ndio manager.

  Moja:Usiwape picha wafanyakazi wako wafikirie kuwa wewe hakuna kitu,hii inaweza kupelekea kukudharau au kukuongopea.Kumbuka kama hunaelimu ya kutosha ya IT halafu ukawa IT manager wa IT,wafanyakazi wako ni nadra sana kukuheshimu,hapa simaanishi kuwa ni lazima uwe geek,inatakiwa kujua mambo ya msingi tu.Mabosi wengi wa nchi zetu zinazoendelea wanakabiliwa na hili.Mfano mzuri tu,angalia mavyuoni,kama Mhadhiri anajiamini na mwenye ufahamu wa kutosha,ni nadra sana kuona anawakamata watu kwenye mitihani au kutopendwa na wanafunzi,ila wale wenzangu na mimi huwa na tabia ya kuwakamata watu kwenye mitihani ili kujenga uoga kitu kitakachopelekea wanafunzi kujenga uoga na kutomshambulia au kumuliza maswali ya kiufundi zaidi.

  Pili:Nani anayejua nini kitatokea muda gani,inawezekana mupo katikati ya project halafu mfanyakazi mmojawapo akaugua au kusafiri,je mutaahirisha project kipindi munasubiria mtu mwingine kuajiriwa? Kama una ufahamu kidogo unaweza kushikiria kwa muda fulani kipindi muaendelea na kazi,Hii imewahi kunitokea,tulikuwa na project moja halafu baadhi ya washiriki wakajitoa,kutokana na ukweli kuwa nilikuwa na uwezo wa kufanya kama alichokuwa anafanya mfanyakazi aliyejitoa hakunaathari iliyotokea,nilichukua nafasi kipindi tunaangalia mtu mwingine wa kumuajiri.Hii sio tu kwenye mambo ya IT bali project zote.

  4: Jua wapi pa kupata msaada wa ziada


  Ukweli unabaki palepale hakuna anayejua kila kitu kwenye uwanja wa IT. Unapokuwa kama maneja kumbuka kuwa kila mfanyakazi ana anachokijua kwa undani na kuna asivyovijua kabisaa. Kuna kipindi unaweza kupokea project ambayo hakuna mfanyakazi wako mwenye uwezo wa kuifanya,kwa wale wenye uzoefu hapa watajua nini ninamaanisha,vijana wa siku hizi tunasema hakuna kuacha project,ipokee halafu utaangalie mbele kwa mbele. kama IT manager hautakiwi kuogopa kuipokea project eti kwa sababu wafanyakazi wako hawana uwezo wa kuifanikisha.

  5: Pata mapumziko ya kutosha

  Ukweli usiopingika ni kuwa kazi za IT ni mojawapo ya kazi zinazochosha na kutumia ubongo mno, kipindi tunamalizia project ya AfroIT kuna kipindi tulikwa tunalala kwa masaa mawili hadi matatu,ukiamka unakutana na makosa kibao huku kalenda ikionesha kuwa muda umekwisha. Nikiwa kama CO kuna siku kadhaa sikulala kabisa,huwezi amini. Hivyo basi ukiwa kama IT manager inatakiwa kutafuta muda wa kupumzika na kuondokana na uchovu na msongo wa mawazo. Bila ya hivyo unaweza kujikuta unakimbia barabarani, au kukufanya kupoteza mahusiano mazuri kati yako na wafanyakazi,je haukuwahi kuona ni mara ngapi bosi amekuwa akifoka kila kitu? Hii ni kutokana na misongo ya mawazo,kitu kitakachopelekea kupunguza ufanisi wa kazi.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kaka unanikumbusha mbali - enzi hizo na kibarua changu cha kwanza kwa ISP mkubwa hapa jijini - nishalala ofisini mara kibao - Jmosi na Jpili ofisi inakuwa yako - hapo unapata matatizo mengi tu hasa haya ya maisha ya kijamii na mahusiano - sababu muda mwingi upo ofisini.

  Ndugu wanakutenga - sababu huwatembelei, wakija kwako haupo.
  Marafiki - Wanakuona unajali kazi sana kuliko wao, kuna muda unaweza kuwapoteza

  Ni vizuri kwa namna nyingine kuwa occupied this much, inakusadida kujiepusha na mambo ya anasa hasa kipindi hiki ukiwa bado damu moto, kipindi hiki unatumia akili yako yote na ikishindikana unalala kwenye makochi ya ofisi ukiamka bado unafikiria solution ya problems ulizokwama kwenye project yako ambayo una implement. Uzuri wa ICT lazima kuna solution ya problem zako so unasoma na kufikiri zaidi. In ICT huwa hakuna solution ambayo haipo, ni wewe tu kutafuta alternative ways of doing it.

  Yeah i really enjoyed that time, siwezi kuisahau maishani.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kaka aisee pia na wewe umenikumbusha mbali niliishafanya kazi kwenye ISP moja sasa siku moja tunafunga sattelite dish na wakati huo tulikuwa tunapata link kutoka ISRAEL kuna kampuni moja inaitwa GILAT basi siku hiyo nakumbuka tulianza kuhangaika kuanzia jioni hadi karibia saa saba za usiku kila tukipewa parameters tukiweka kwenye DVB modem ngoma haikubali inabidi tuanze kutafuta direction mpya at the same time hapo clients wetu wako down ilikuwa hectic sana nakumbuka nilienda kulala nyumbani saa 9 usiku but it was a good experience.
   
 5. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu asilimia 90% nimeandika kutokana na experience niliyopata hivyo hakuna haja ya acknowledge.

  Elnino na Finest,hiyo ndio marejesho ya ICT,ila kama alivyonena mkuu hapo juu,kwenye ICT hakuna kinachoshindikanika,ni wewe mwenyewe.Ila kuna wakati ngoma inakuwa nzito,unaona kama mbingu inashuka,Ila katika sehemu zote kazi ninayooona inatesa ni ISP,hii kazi we acha.Ila suluhisho la hii kama utaona umezidiwa ni kuiweka simu offline so kila wakikupigia wanaambia The number you are calling can't be connected at moment,please try again later"halafu landline unaweka mkonga chini akipiga anaambiwa namba busy,kesho yake bosi akija unalo la kujitetea.hehe
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kilongwe umelenga zaidi mameja wa ICT lakini nadhani ni vitu inabidi watu wote regarless na nafasi yake kwenye ICT wanatakiwa waviishi.

  Changamoto kubwa ninayoona tunakosa ni UBUNIFU wa kuangalia new and producive ways of doin things

  Juzi juzi nimendika thread moja upande hasa wa serikali. Pale wizara ya elimu kuna Mkurugenzi wa Kompyuta na chini wake ana graduate wamemaliza Chuo Kikuu na vyuo vingine na wamefuzu.

  Inawezekana Director wa ICT wizaa ya elimu hajui youtube lakini je walio chini yake hawajui youtube inaweza kutumika kama nyezo ya kufundisha na kuwaonyesha wanafunzi shule amabazo zina uhaba wa vifaa vya maabara.

  Elimu ya visual inasadia kuwafanya wanafuzi waelewe hasa ukija kwenye suala la practical. Je wahitimu wa chuo kikuuu walio idara ya kompyuta waliopo wizara ya elimu hawajawi kujiuliza wanawezaje kutumia elimu yao, ujuzi wao na uzoefu wao kuwashauri maboss wao njia ya kuboresha elimu?

  Ukija kwenye maabara zetu za mikoa na taifa ziko hoi.lakini kuna fursa ya ICT kuzifanya za kisasa kwa gharama nafuu.

  Nawaomba wana ICT hasa wa serikali wajiulize na kuwashauri wakubwa wao officialy njia za kutatua matatizo mbali mbali. Sio lazima matatizo yote yaishe kwa kuandika pogram au database. Sio lazima slution zitoke juu.
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtazamaji heshima mbele.

  Umeeleza mambo mawili muhimu sana ambayo bila hayo hatutafika mbali.

  Kwanza ni ubunifu (creativity) hii inaanzia kwa mwalimu mpaka mwanafunzi kuwa mbunifu. Hii inahusu kulinganisha maisha halisi na somo lenyewe ambalo mtu anasoma. Kwa mfano utamwambia mwanafunzi atengeneze presentation kwa kutumia MS Powerpoint. Mwanafunzi ambae ni mbunifu, kwa kutumia materials ambayo mwalimu alikuwa akimpatia kupitia lecture darasani ni lazima atengeneze presentation nzuri labda kuhusu "planning LAN infrastructure" katika shule yake.

  Hapo watu watakaosikiliza presentation hio wataona kwamba mwanafunzi huyu ameelewa somo hilo na pia ni mbunifu kutokana na mtindo atakaotumia kuwasilisha mada yake hiyo.

  Pili umeongelea elimu ya "Visual" hili ni moja ya mambo ambayo ni lazima mwanafunzi na mwalimu washirikiane kujiendeleza. Kwa mfano kwenye ICT tena utataka wanafunzi wajifunze kuunganisha maneno na picha ili kutengeneza hadithi labda tuseme Abdul Adventures. Sasa hapo wanafunzi wataelekezwa kuunganisha maneno sambamba na picha mbalimbali za huyo Abdul na adventure zake.

  Lakini hatujachelewa ICT imeingia Tanzania na inabidi kila mtu aizingatie. Wizara yenyewe ya elimu itabidi iangalie upya mitaala ya shule zote.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli hatujachelewa lakini tuko nyuma. Tatizo lingine utakuta Meneja wa ICT wizara ya elimu kazi zake hazihusiani kwa vyovyote vile na maendeleo ya elimu.

  Lakini suala la kutumia youtube , au video kwa ajili ya practical za masomo ya sayansi kwanza litaokoa gharama wakati huo huo likiinua viwango vya elimu.

  Hata kwa mtaala iliyopo kinachotakiwa ni Wizara ya elimu kuwa na VISION ya kuwaelimisha walimu wa sekondari juu ya nyenzo za kisasa kufundishia.

  Inachekesha hata wanafunzi wa sekondai dar mwanza ,arusha na shule za mjini hawajui process ya condesation, fermentaion, principle za wave ,etc kwa practical wakati kuna video kibao mtandaoni .
  Wanafunzi wanatumia effort kubwa kukariri maelezo . Hapa ndipo napoona bado hatujawa CREATIVE vya kutosha.

  Au Kwa nn Wizara isitumie kiasi kidogo chapesa kuwakusanya walimu fulani ikatengeneza video za practical muhimu za masomo ya biology,chem,Phy,Geo . Then maelezo ya walimu hao yakatawanywa shule zote za sekondari. Wizara inaweza kutoa projector na laptop kwa kila shule.

  Kama kuna uhaba wa fedha za laptop na projector basi maktaba za mikoa zitumike. Mwalimu akitaka kuwaonyesha practical fulan wanafuzi anawapeleka maktaba wakaone video.

  Wizara ya elimu shule zinaweza kubadlisha maabara za shule kuwa inforation center zitazokuwa na Authorised video zilizopitishwa na wizara kwa masomo mbali mbali.

  Ndio maana bado naona mameja wengi wa ICT kwenye taasisi za umma bado wanafanya kazi kwa mazoea.
   
Loading...