Kuwa mbunifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa mbunifu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 15, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja.

  Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanza kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena.

  Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja.

  Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa.

  Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenzi wako ilikuwa ni kulala saa sita au nane usiku kwani mlikuwa mnapigiana simu na kutumiana sms kiasi ambacho hamkulala hata hivyo baada ya kuoana sasa kila mmoja anakuwa sehemu ya maisha ya mwenzake kila siku inayipita duniani.

  Sasa unalala naye, unaamka naye na kula chakula naye. Mnamiliki sebule moja, chumba cha kulala kimoja na kitanda kimoja, frji moja nk. Unajifunza tabia zake kwa undanim, unajifunza nini anapenda na nini anachukia, unajifunza udhaifu wake na uimara wake unajua nini anapenda kwenye TV na zidi rafiki zake watakuja kwenu upende usipende na kufanya au kuongea mambo yao.

  Simu za rafiki zake zitapigwa kwenu, utakuwa domesticated man au domesticated woman.

  Unapoishi na mtu mwingine taratibu hubadilika, masuala ya sex yatabadilika kwani utalazimika kufahamu hisia zake kimapenzi (feelings/emotions) mahitaji na kile anapenda siku zote na wewe kuwa mbunifu maana unaye kila siku.

  Pia unatakiwa kuripoti kila siku kama utachelewa kurudi nyumbani utalazimika kumwambia mapema. Lazima utambue kwamba sasa utakuwa na mtu ambaye ana hofu na wewe kuchelewa au kutokupata habari zako ndani ya saa 6 mchana na huruhusiwi kwenda kimya hadi sita usiku bila yeye kujua upo wapi na kama ni salama.

  Pia kuishi pamoja ni kujifunza kuwa kitu kimoja (coexist) na usiopokuwa makini unaweza kujikuta excitement zote za nyuma zinaisha na maisha yanakuwa tofauti na yale kabla ya kuishi pamoja.

  Unahitaji kuwa mmbunifu wa namna ya kufanya kila siku inayokuja duniani inawapo mambo mazuri yanayofanya kila mmoja kuwa excited na mwenzake la sivyo badala ya kuishi kama wapenzi mtaishi kama dada na kaka wanaolala pamoja na ambao moto wa mapenzi umezima.

   
 2. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Unajua Pdidy thread zako nzuri kweli ila unazifumuaga nyingi sana mpaka unachanganya watu, Mambo hubadilika baada ya kuanza kuishi pamoja sababu ya kukosa ubunifu, kama mbunifu kila siku utafurahia maisha yako ya mahusiano
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kaka leo umezi-post za kutosha ,....nafikiri haujaenda kibaruani
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pdidy zile simu za Hillary Clinton zimepatikana?
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Mkuu one thing at the time!
   
 6. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  at least to give us time aisee
   
 7. s

  sparkville Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ubunifu na mawasiliano ndio nguzo, unaweza ukawa mbunifu lakini kumbe mwenzio akawa hajapenda ubunifu uliuongeza ikawa kero tena, mawasiliano muhimu
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ehh chaudaku
   
 9. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  bos wake kafa
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hili somo limesimama, linafaa sana ktk kuboresha mahusiano! Big up didy!
   
Loading...