Ukitumia YouTube kujifunza ufundi wa kompyuta nasi Kuwa makini sana na aina ya site unayopata mafunzo hapa ninamaana Kuna site wanaelekeza vitu lkn malengo Yao ni kukufanya uharibu Ili uwatafute. Wengine wanafundisha kwa taaluma ndogo na usipokuwa makini unaweza kujikuta unaharibu kifaa chako. Kama umepata mafunzo vyema basi ni vema uanze na kompyuta mbovu Ili iweze kupona au ya kwako mwenyewe, baada ya hapo unaweza kutengeneza za watu. Angalizo ukishaitwa fundi wa kompyuta fahamu Kuwa sio lazima Kila kompyuta utakayoletewa ipone. Ukishindwa sio lzm ung'ang'anie kukata nayo unaweza kumtafuta fundi mwenzako na mka share uzoefu. Kwa fundi anayejifunza kutengeneza kompyuta, kompyuta mbovu isyowaka inaamani sana kutengeneza kuliko inayowaka alafu ikazimia kwako.
Kubadili/kushusha windows katika computer ni kipengele kidogo sana ktk dhana ya ufundi wa kompyuta. Muhimu jitahidi kuzifahamu sehemu muhimu za compyuta na ufanyaji wake wa kazi. Pia jitahidi kujifunza Tabia za ubora au udhaifu wa vifaa vya kompyuta. Mfano kama kompyuta Haina RAM inakuwaje? Ikiwemo lkn ni mbovu inakuwaje? Je Nini maana ya baadhi ya milio ya kompyuta? Kwa Leo tuishie hapo