Kuvunjiwa vioo vya magari na kuibiwa Laptops | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvunjiwa vioo vya magari na kuibiwa Laptops

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by landless, May 2, 2012.

 1. landless

  landless Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani,nipo stranded kama wiki tatu sasa zimepita tangu wamespray na kunivunjiwa kioo cha gari,ilikuwa siku ambayo sunami ingetokea,siku ambayo mvua ilinyesha sana hapa mjini,mida ya saa tatu usiku,maeneo ya UPANGA,NYUMA YA SCOUT WANAPAITA COCONUT PUB,nahisi jamaa walikuwa na Tax nyeupe,wameniibia begi langu,likiwa na laptop mbili(HP pavilion dv5 {imekufa display ya inch 14.5),toshiba),external harddisk aina ya SEAGATE(250MB),original driving licence,kadi 2 za benki(NBC and CRDB),camera (Sony)ya pink,documents za office,kazi za consulting nilizotakiwa kudeliver a week before sijaibiwa.Worse enough ni external HDD niliyokuwa naitumia kama the only back up,ambayo nilitembea nayo ili nikahifadhi data zangu nyingine toka kwa office ina back up of almost four years works done.Im almost broke!!!.Nimejaribu kufuatilia nimeambiwa kuna jamaa wanaweza kunipatia taarifa nzuri maeneo ya kariakoo au posta.Nimefuatilia kupitia jamaa yangu mmoja(1) ambaye alifanikiwa kupewa namba ya hao jamaa wa mishemishe(2) wa kariakoo,wakamwambia watampatia jibu,last time wamemjulisha kuwa huo mzigo upo kinondoni wanapouza/kuhifadhia vifaa vya dili kama hivi,hivyo wakamjulisha(1) kuwa wanafuatilia huko nijiandae kwenda kugomboa,lakini hii sasa ni wiki ya pili jamaa(2) mda mwingine hapatikani,mara ya mwisho alimjulisha jamaa huyu (1)yangu kuwa mda mwingine inabidi azime simu kwa sababu ya inshu zake zinamfanya anatafutwa sana.Hivi jana nimepita maeneo hayo nikaiona ile Tax nliyokuwa naihisi,ikiwa inaodoka nikaanza kuikimbiza,lakini ghafla ikakata kona na kuingia mitaani,nimeifuatilia usiku,kuna mahali ikawa imepotelea sikufanikiwa kushika namba za gari,sasa naona kama uwezekano wa kuvipata unazidi kuwa mgumu.So wadau plz anyone mwenye ushauri namna gani ya kufanya au mwenye experience kwenye hili au na maeneo haya ya COCONUT PUB naomba ushauri kitu gani kingine naweza kufanya nikavipata hivyo vitu,muhimu zaidi ni ile external HDD.
   
 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dah pole sana ndugu yangu,hao Jamaa wanatia hasira sana kwakweli,waliwahi kumpiga Bro wangu Laptop 2(1 ilikuwa yangu) Modem 2,Xternal na zagazaga zingine za office muhimu kweli,tulijaribu kuwafuatilia sana kwa lengo la kuvilipia,hadi hiyo mitaa ya Kino tulielekezwa lkn hatufanikiwa kuvipata....lkn kwa ushauri wangu kwa jinsi unavyokwenda nao hao Jamaa usijaribu kutumia nguvu sana au hata kuonyesha dalili kuwa ukivipata utachukua hatua labda kwenda Polisi au vipi,wewe inabidi uwe mpole sana fatilia kwa nidhamu huku ukiwaahidi kuvilipia na kuishia zako unaweza ukavipata...eeh bwana hii ndo Tz yetu kuibiwa uibiwe wewe hlf kuvinunua hivyohivyo vitu ulivyoibiwa inabidi ubembeleze....am tired of this Country jamani.
   
 3. landless

  landless Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks mkuu,ntafanya hivyo,unaweza nielekeza maeneo hayo ya Kinondoni ni wapi?
   
 4. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kama ni wiki mbili czani kama utavipata hivyo vitu,pia je una evidence yeyote ya kukusuport police?
   
 5. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Aisee pole sana mdau! Kwa kweli inauma sana.... Tena ndo back up yenyewe wamebeba. Jaribu kufuata ushauri wa mdau hapo juu ili lengo lako litimie.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu kwanza nakushauri usitumie nguvu kuvitafuta vitu vyako kuwa mpole nenda nao taratibu wala usitumie polisi ukitumia polisi uwezekano wa kuvipata utakuwa mdogo jaribu kwenda pale round about ya upanga na jamhuri pale Azzam take away kuna vijana pale ndio dili zao town ongea nao taraatibu waambie mie tanunua tena huo mzigo.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pole sana, inauma sana hii kitu.

  Saidi Mwema na vijana wako najuwa wanapitia humu.

  Songoro, najuwa kuwa wewe upo huko jikoni, ingawa huhusiki na hizi jinai, lakini huwezi kuwaambia hao manjagu wenzako?
   
 8. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,021
  Trophy Points: 280
  Mkuu, umechukua namba ya hiyo gari?
   
 9. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,107
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  pole mkuu,wiki mbili ni muda mrefu kidogo,hao jamaa kwa njaa zao sijui kama watakua bado na huo mzigo,ila usichoke, huwezi jua..
   
 10. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana kwa mkasa uliokusibu ambao kwa kweli unaweza kumpata yeyote yule, ila nakutahadharisha uwe mwangalifu wakati huu unapoendelea kufatilia vitu vyako. Uwe macho na matapeli wanaoweza kujitokeza wakautumia muda huu kujifanya wanawajua wahusika waliokuibia na kwa hivyo kuendelea kuzitafuna pesa zako kwa ulaghai. Mfano utaambiwa kuwa wezi tumewasiliana nao wanataka Shs.milioni moja, lete pesa tukavigomboe vitu, kumbe vile unaendelea kulizwa tu. Hamna kinachofanyika zaidi ya kuendelea kukulia pesa zako na kukupotezea muda tu. Waswahili hutuambia Mjini shule.
   
 11. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu,imeniuma utafikiri ndio mm. Jaribu kufata ushauri wa Ritz na Anselm,nenda nao taratibu. Pitia pitia hiyo mitaa ya Kinondoni na gari ingine sio ile waliyoivunja kama utaweza kuipata hata hiyo tax uliyoihisi uchukue hata no za gari. Cheki na wale jamaa wa pale Azam town wanaweza kukusaidia.
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  awaambie nini sasa hapo!!!!!!!!!
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole sana Mkuu, siku nyingine usiweke External Hard Drive pamoja na Laptop. Ni sawa na kuweka mayai yote kwenye kapu moja!
   
 14. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ngoja tuwawekee nyoka kwenye mabegi ndo watakoma. Haswa lile eneo la Tumaini hospt. upanga. Ndio sana wanaiba.
   
 15. landless

  landless Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks mkuu kwa ushauri mzuri,appreciate
   
 16. landless

  landless Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks kaka,mitaa ya kinondoni bado sijaijua ni wapi,ila ngoja niwacheki hawa jamaa wa Azam round about.
   
 17. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,857
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  p ole sna mkuu,i cn feel the pain that ur going through. next time ucweke HDD Pamoja na laps. hyo ni back up yako ambayo itakusaidid pind laps yako iharibikapo na co kuharibika tu na kuibiwa km hvo. pole sana!
   
 18. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  i ni muathirika wa kuibiwa maeneo ya hapo apo upanga mbaya zaidi mimi wameniliza vyeti vyote mpaka leo sijapigiwa simu wala nini
   
 19. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Pole. Tusitembee na vitu vyote muhimu. Back ups zibaki home. Its risky thing to do. Pole sana
   
 20. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,825
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 280
  Mimi najua hawa watu wapo na wanajulikana kabisa na serikali imeamua kuwaacha kabisa yani hapo ndio napata hasira sana na hii serikali chovu...pole kaka mimi nakuombea upate tu
   
Loading...