Kuvunja Muungano ni kujichimbia Kaburi- Asema Shamhuna | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvunja Muungano ni kujichimbia Kaburi- Asema Shamhuna

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by i pad3, Apr 8, 2012.

 1. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [h=1]Kuvunja Muungano ni kujichimbia Kaburi- Asema Shamhuna[/h] [​IMG] Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar (SMZ), Ali Juma Shamuhuna, amesema kuwa na mawazo ya kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sawa na kujichimbia kaburi.
  Shamuhuna alitoa tamko hilo katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Wizara yake na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Serikali ya Muungano, mjini hapa juzi.
  Alisema kwamba kama Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una kasoro dawa yake ni kuzitatua kwa maslahi ya pande mbili za Muungano na sio kuwa na fikra za kuuvunja kwani umeleta amani na umoja wa kitaifa kwa Watanzania.
  “Kuwa na mawazo ya kuvunja muungano sawa na kujichimbia kaburi,…Sisi tuliouganishwa katika muungano tunapaswa kulinda na kuuendeleza muungano wetu,” alisema Waziri Shamuhuna.
  “Mawaziri tuna jukumu kubwa sana mie sikubaliani na wale wanaosema muungano hauna faida yoyote,” alisema Waziri Shamuhuna ambaye pia mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa.
  Aidha, alisema kwamba Wizara yake itafanyakazi kwa karibu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Muungano ili kuharakisha kiwango cha ubora wa elimu kinaendelea kuimarika Tanzania Zanzibar.
  Tangu kuanza mijadala ya katiba mpya kumeibuka kikundi cha wanaharakati Zanzibar ambao wanashawishi wananchi kuvunja Muungano na kutoa lugha chafu dhidi ya waasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar na viongozi wa kitaifa Zanzibar.
  Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Muungano, Dk Shukuru Kawambwa, alisema wanafunzi 12,269 wameshindwa kupata mikopo ya elimu ya juu kutokana na Serikali ya Muungano kukosa fedha za kugharamia elimu katika mwaka wa fedha 2011/12.
  Dk Kawambwa alisema jumla ya wanafunzi 38,541 walifanyiwa udahili na kuonekana wanazo sifa na vigezo lakini wanafunzi 26,272 tu ndio walionufaika na mikopo ya elimu ya juu. Aidha alisema kwamba serikali imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa kutokana na ufinyu wa bajeti yake.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  big up kwa hicho kikundi kinachotaka muungano ufe. Tutengane tu
   
 3. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndoa ambayo baba wala mama hajulikani, siyo ndoa na mwisho wake ni kuvunjika tu......Tanganyaka yetu ilishamezwa, Zanzibar yao bado ipo, tena ina serikali.....nani mjinga.....jibu moyoni mwako....
   
 4. EBENEZA MT

  EBENEZA MT JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kero za muungono zitaisha chadema itakapokuwa chama tawala.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Shamhuna hayo ni mawazo yake na mawazo ya wenzake walioko serikalini. Lakini mioyoni mwa Wazanzibar asilimia kubwa na Watanganyika asilimia kubwa muungano haumo kabisaa. Hasa kwa Tanganyika ni hasara tupu na hakuna faida yoyote.
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Mzanzibari yeyote anayesema anautaka muungano basi ujue anataka kufaidika nao, na si vinginevyo.
  Shamhuna tnaye mfahamu, site tnayemsikialeo.

  Hebu tujikumbushe nukuu zake toka Gazeti la Mwanahalisi, mwaka 2008,

  "Lipo kundi la Watanzania, wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, linalosisitiza kuwa Zanzibar si nchi. Hoja hapa ni kwamba nchi ni moja tu - Tanzania.

  Hivyo, Zanzibar ni sehemu ya Muungano, hivyo ni sehemu ya nchi. Kundi la pili linaongozwa na Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Shamhuna, likidai kwamba iwe iwavyo, Zanzibar ni nchi. Ina katiba yake, Rais wake, Baraza la Wawakilishi (Bunge), ina wimbo wake na bendera yake.

  Mvutano na mjadala huu si mpya, bali umekuwapo miaka mingi iliyopita, na umekuwa ukiendelezwa chini chini, hasa baada ya kushindikana kwa hoja ya Zanzibar kujiunga katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (IOC) ikifuatiwa na hoja ya kufufua serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano, mwanzoni mwa miaka ya 1990.

  Nguvu pekee iliyozima hoja hizi kitaifa ni ushawishi mkubwa wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Kwa wakati huo, Mwalimu Nyerere aliwashangaa wana CCM kuanzisha hoja za kuigawa na kuiua Tanzania huku wakijua kuwa si sera ya chama chao. Aliwaeleza kuwa kama sera hiyo ingekuwa inashabikiwa na wapinzani, lisingekuwa tatizo kwake, maana ni sera mbadala.

  Fimbo yake kwa waliokuwa wanataka kuiendeleza hoja hiyo wakiwa ndani ya CCM ilikuwa moja: "Ondokeni kwenye chama, mjenge hoja mkiwa nje ya CCM, maana hii si sera yetu."

  Wakanywea, wakaachaa nayo si kwa kukerwa nayo bali kwa kulinda maslahi yao ndani ya CCM. Lakini upinzani umekuwa ukiifufua hoja hii kwa maelezo mbalimbali, na kimsingi, karibu vyama vyote vya upinzani vinaungana katika sera kwamba Muungano unaofaa ni wa serikali tatu: Tanganyika, Zanzibar na Muungano.

  Tume kadhaa za rais, ikiwamo iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga kuhusu muungano ilipendekeza juu ya umuhimu wa serikali tatu. Serikali ilipuuza ushauri huo, lakini haikujibu hoja.

  Mvuto wa suala hili kwa Wazazibari uko wazi. Linapojadiliwa suala la hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano, Wazanzibari hawaendekezi tena itikadi za vyama.

  Wanakubaliana kwamba Zanzibar ni nchi inayostahili kusimama peke yake, na Tanganyika ikitaka isimame peke yake, ndani ya Muungano.

  Kinachoshangazwa ni kwamba watawala wameziba masikio. Hawasikii kauli za Wazanzibari wala za wataalamu wengine wa msauala ya kikatiba. wanachong'ang'ania wao (watawala) ni kauli za vitisho kwamba wanaopinga muundo wa sasa wa Muungano wanataka kuua Muungano.

  Wamesema wengi, lakini katika siku za hivi karibuni amejitokeza mmoja wa waasisi wa CCM, Mzee Peter Kisumo, akatoa kauli kali dhidi ya kina Shamhuna na wenzake.

  Alisema: "Kama Wazanzibari wanadai Zanzibar iwe nchi, wasiliseme kwa soni wala wasimbane Pinda. Shamhuna kama Shamhuna hatoshi kuitoa Zanzibar kwenye Muungano uliodumu kwa zaidi ya miaka 40."

  Lakini hakuna popote ambapo Shamhuna alisema anataka Zanzibar ijitoe kwenye Muungano. Shamhuna na wenzake kama yeye, wanachosema ni kwamba Zanzibar ni nchi. Iliungana na nchi nyingine (Tanganyika) kuunda Jamhuri ya Muungano.

  Muungano haukuua nchi, bali uliziunganisha kuunda jamhuri. Kinachogomba hapa ni muundo wa Muungano na tafsiri ya neno nchi.

  Binafsi nawaona akina Shamhuna kama wana CCM walioongoka na sasa wanaona kwa mtazamo mpya. Chama chao kinapaswa kuwasikiliza na kuweka mazingira ya kuingiza hoja za Wazanzibari katika uboreshaji wa muundo wa Muungano.

  Kisumo anapotosha Watanzania anaposema kwamba wanaojadili suala hili wana lengo la kuvunja Muungano.Katka umri alionao, Mzee Kisumo anapaswa kuwa amejifunza mengi katika historia, kwamba si lazima muundo wa Muungano wa leo ubaki kama ulivyokuwa wakati unaundwa mwaka 1964.

  Kama mahitaji ya wakati ule yalihitaji tuwe na serikali mbili si lazima mahitaji ya sasa yabaki hivyo.

  Akumbuke pia kwamba wakati Tanganyika ilipoteza hadhi ya kuwa serikali ndani ya Muungano, Zanzibar ilibaki na nafasi yake; na hata Mwalimu Nyerere alilizungumzia hilo akisema kwamba kwa mtazamo wao wakati huo, alikataa kuunda nchi moja ili kuepuka hisia za ubeberu (kwamba ameifuta na kuimeza Zanzibar).

  Akasema ilikuwa zaidi kwake kuifuta Tanganyika kwa sababu, kutokana na ukubwa wa sehemu moja, ingekuwa vigumu kwa Zanzibar kuimeza Tanganyika.

  Na mtu anayechunguza mjadala huu unavyoendelea sasa, lazima ajue kuwa Shamhuna hasemi hayo anayoyasema kama mtu binafsi. Anakisemea kikundi cha walio madarakani Zanzibar. Ni kikundi kinachotaka kuiona Zanzibar ikiwa na mamlaka zaidi katika masuala yanayoihusu. Ni kikundi kinachotamani kuona rais wa Zanzibar akiwa rasi kweli kweli."


  Mwanahalisi 29 Julai 2008

  Huu ulikuwa mjadala wa Zanzibar ni Nchi.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  mjinga ni Tanganyika na watanganyika
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  tatizo la wazanzibar ni elimu dunia na udini mbele. watoke zao.
   
 9. k

  karafuu Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zanzibar elimu ni nature,dini yetu inaelimu tosha ya kidunia kila kitu kimo,muungano hatuutaki nyerere ametulazimisha tu,na hao kina SHAMHUNA hawana tena nguvu mbele ya umma ama kweli people power.na safari hii inakwenda zanzibar katika kudai nchi yetu hoja yake haina meno, tokea miaka mingi nyuma kero zipo na haziondoki.ACHA TU UVUNJIKE.
   
 10. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Muungano ni ajenda ya CCM, sijui faida yake kwangu kama Mtanganyika na wala sitaki kujua.
  Nnachoendelea kuomba ni Wazenji wauvunje wasepe zao. Hapa Tanganyika ndani ya CCM hakuna mwenye guts za kuuvunja.
   
 11. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekaa nikatafakari mwisho wa siku sijapata jibu. Hivi ni kwanini inakua vigumu kuuvunja huu Muungano? Hivi ni kweli kwamba sisi watu wa bara tunawaonea huruma sana watu wa Zanzibar kwamba hawataweza kujitawala? Je kuvunjika kwa muungano kuna athari zozote kwa usalama wa bara? Au kuna maslahi gani katika huu muungano?

  Kwanini tunaking'ang'ania kitu ambacho wengine hawakitaki?

  Kwa kadiri hoja za muungano zinavyoendelea, napata mawazo kwamba Wazanzibari sio kwamba wanataka mambo fulani kwenye muungano yarekebishwe, ni kwamba wanataka uvunjike kabisa. Je sio busara kuwaacha waende zao kuepusha machafuko yasiyo na maana.

  Naomba great thinkers mnisaidie kutegua kitendawili hiki. Ni kwanini tunaung'ania Muungano?

  Nawakilisha.
   
 12. z

  zanzibar huru Senior Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hana akili huyu
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Muungano hautavunjika, zidumu fikra za mwenyekiti.
   
 14. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kawaulize Wakenya kuhusu Al Shabaab, utapata jibu!
   
 15. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua huu muungano ni vigumu kuuvunjwa angalie mabalozi wa nchi za nje walivyowahi kwenda kule nadhani jibu unalo.Wakiongozwa na balozi wa Marekani na Canada mzee kuvunja muungano ni kama kuota iko siku mtu atapaa.
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,580
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Utavunjika tu Boko Kharamu wa Zanzibar siyo mchezo ati.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  hawa mashehe ina maana hawajui?
   
 18. N

  Nambombe Senior Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama muungano wenyewe haueleweki bora uvunjike
   
 19. A

  Albimany JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45

  Wewe mgeni wa siasa sakimagharibi. alshabab hawakuwahi kuivamia kenya kabl ya kenya kuivamia somalia ugomvi ulikua ni wao wenyewe wasomali.

  kenye ilivyojipendekeza ndio hayo leo wanayakuta walioyatafuta.

  lakini pia hujui kua Obama alifikiria njia ya urahisi ya kuwasaidia wakenya bila ya kulaumiwa na wamarekani wenzake, ndio alipowashauri wakenya kuingia vitani ili wapate misaada.

  Ukiangalia historia utagundua kua wamarekani waliingia katika vita vya somalia na walishindwa kwasababu wasomali huondoa tafauti zao zote wanapowaona wamarekani ndani ya ardhi yao.(husema wamarekani wanainajisi ardhi yao)

  Sasa wakatafuta watu wasio na akili wakawaingiza vitani ambao ndio kenya. Musisome habari za jamiiforam tu someni na habari za nje ya hapa mutajivunza sana dunua inavyoendeshwa.
   
 20. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa anasema hautaki Muungano. Kaamua kubaelezea bajamaa kupitia mtandao kwa kutumia uhuru wake wa kikatiba!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...