Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Katibu wa kamati iliyoundwa na Nape Nnauye kuchunguza sakata la uvamizi Clouds Media, Deodatus Balile amesema yeye kama mwanahabari na mwanasheria ameshtushwa na taarifa ya Dkt. Mwakyembe kuwa taarifa yao haikuwa na mizania kwa kutohoji upande wa pili.
Balile amedai wanakumbuka uchunguzi wake kwenye kamati ya Richmond mwaka 2008 ambapo alipata fursa ya kwenda hadi Marekani lakini akashindwa kwenda Magogoni kwenda kuhoji mtuhumiwa mmojawapo kati ya aliokuwa akiwahoji.
Balile amesisitiza wao walifanya juhudi za dhati kwa kwenda hadi ofisi za mkuu wa mkoa, anadai Mwakyembe anatumia nguvu kubwa kuonyesha kamati yao haikuwa na weledi lakini anashangazwa kwani hakuonyesha walau hata juhudi mwaka 2008 na amemuomba aache kudhalilisha kazi iliyofanywa na kamati hiyo.