Kuvaa nusu utupu natangaza brand - Vanessa Mdee

Mtanzania Mkenya

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
238
387
Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye anafanya poa katika anga za kimataifa Vanesa mdee, amefunguka sababu ya yeye kupenda kuvaa nguo za nusu utupu.

Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Radio na EATV, Vanessa Mdee amesema anapenda kuvaa mavazi hayo ambayo hayakubaliki kwa jamii, kwa sababu anatangaza brand yake, na hatimaye impe dili la matangazo kwa wabunifu wa mavazi.

“Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao, mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Louis Vuitton, nataka designers wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nna malengo , na if im gonna offend anybody im sorry”, alisema Vanessa Mdee.

Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameachia video yake mpya ya Niroge, amesema ana mipango ya kufika na kutambulika dunia nzima katika kazi zake za muziki, kama alivyochora ramani ya dunia kwenye mkono wake.
 
Ukuwa uchi ni kutangaza brand? Unaweza kuvaa vizur na ukajitangaza tuu km kina YemiAlade
 
Japo Picha wadau plz mimi sipendagi Mabonge
Hiki hapa, na hapo kipo na anayependa vimifupa vyake.
images
 
mbona Yemi Alade anavaa nguo ndefu lkn zina mpasuo mpaka kwenye mapaja kuna tofauti gani na anayevaa vimini?
 
Au mimi ni mshamba, sioni shida km mtu akiwa anatembea barabarani mtupu, mbona hata machizi hufanya hivyo, lakini honestly, let kila awe vile anataka kuwa.
Wewe ulitembea lini njiani ukiwa mtupu!

Kwanza tabia ya kutembea uchi umeitoa wapi wakati babako ni mchungaji!
 
Back
Top Bottom