Kuuza pombe Zenj is a death sentence! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuuza pombe Zenj is a death sentence!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIM KARDASH, Jan 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]WAFANYABIASHARA YA POMBE WAPIGWA RISASI ZANZIBAR[/h]
  [​IMG]
  Mfanyabiashara Alvind Asawla aliyepigwa risasi katika paji la uso ikatokea shingoni na kumwagiwa tindikali Zanzibar, akiwa na mkewe Bimal katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatano iliyopita. (Na Yusufu Badi).

  WAFANYABIASHARA wawili mtu na mkewe, wamepigwa risasi na kumwagiwa tindikali huko Zanzibar kwa kuuza pombe.

  Katika uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita mwanamke Bimal Alvind (36) alinusurika kupoteza ujauzito wake wa miezi minne baada ya kupigwa risasi ya tumbo na kumwagiwa tindikali.

  Risasi hiyo ilitolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuathiri ujauzito huo lakini tindikali hiyo ilimjeruhi mwilini kuanzia usoni, kifuani kwenye matiti, mikono yote miwili na tumboni.

  Mumewe, Alvind Asawla (42) alipigwa risasi kichwani kwenye paji la uso katikati ya macho iliyotokea nyuma chini ya shingo na sasa amepooza upande mmoja.

  Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwa ndugu yake Upanga wiki hii, Asawla alisema walivamiwa Jumatano iliyopita saa 10:30 jioni katika Mtaa wa Hurumzi Mji Mkongwe.
  Alisema wakati wakivamiwa, yeye na mkewe aliyeishi naye kwa miaka 17 sasa na kujaliwa watoto wawili; Priyanka (14) na Nidh (12), walikuwa wakitoka katika biashara yao wakirudi nyumbani eneo la Kiponda.

  Alisema ghafla watu wawili walimvamia mkewe na kummwagia tindikali na yeye alipokuwa akijaribu kumsaidia, watu hao walimmwagia tindikali usoni.

  Kwa mujibu wa Asawla, wakati wakitaharuki kwa hali hiyo, ghafla alitokea mtu mwingine na kumpiga risasi katika paji la uso akadondoka chini huku damu zikimtoka.

  Alisema alijaribu kujikongoja kwa nia ya kuendelea kumsaidia mkewe lakini mtu huyo wa tatu alimpiga risasi ya pili mgongoni na mkewe akapigwa risasi ya tumbo.  Asawla alisema baada ya hapo hakujua kinachoendelea mpaka alipozinduka Kituo cha Polisi cha Malindi walipopatiwa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja walipopigwa picha za x-ray na kugundulika wana risasi mwilini.

  Baada ya kipimo hicho, Asawla alisema hospitali hiyo haikuwa na vifaa vya kutoa risasi hizo, ndipo ndugu zake waliwasaidia usiku huo na kuwasafirisha kwa ndege hadi Dar es Salaam ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Alisema mkewe alilazwa katika wadi ya Kibasila namba tatu na yeye akahamishiwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kipimo cha CT-Scan ambacho hakikupatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa Asawla, mke wake alitolewa risasi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na yeye kufanyiwa upasuaji wa kumtoa risasi ulifanyika katika Hospitali ya TMJ.
  Alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ni mzima hadi sasa kwani alipigwa risasi sehemu mbaya na kukaa nayo kwa saa zaidi ya 12 ndipo ilipotolewa kichwani jambo lililowashangaza hata baadhi ya wauguzi.

  “Nimepooza upande mmoja wa kichwa changu, sihisi jambo lolote lakini madaktari wameniambia nitarudi katika hali yangu ya kawaida polepole baada ya kufanya mazoezi,” alisema.

  Alisema aliambiwa kuwa risasi hizo hazikupita katika mishipa mikubwa ndiyo maana yuko hai hadi sasa na mshipa mdogo uliomwaga damu, umefanya jicho la upande uliopooza kuwa jekundu licha ya kuona vizuri.

  Mfanyabiashara huyo alisema kuwa watu hao wamempa ulemavu wa kudumu bila kutegemea huku akiamini siyo majambazi ingawa walichukua pochi ya mkewe iliyokuwa na fedha kidogo.

  Alisema hospitalini wameambiwa tindikali waliyomwagiwa ni aina ya asidi sulfuriki (sulphuric acid) inayotumika katika magari.

  “Unajua mwizi anataka fedha na siyo kumwagia tindikali au kukupiga risasi na sisi hatukuwa na silaha yoyote; nia ya watu hawa ni kutuua kwani tumekuwa tukipata vitisho vya mara kwa mara kutokana na biashara yetu ya kuuza pombe Zanzibar,” alidai.

  Alidai mara kwa mara wamekuwa wakipata vitisho ikiwemo kukuta karatasi inayomtaka kuacha biashara hiyo vinginevyo utauawa; na wamekuwa wakitoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na biashara zao.

  Alilalamika kuwa licha ya wafanyabiashara wengi wa pombe kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupiwa risasi na hata kuchomwa moto, hakuna aliyewahi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
  “Sisi tunafanya biashara na mahoteli makubwa ya kitalii na tunalipa kodi zote stahiki, Serikali iseme wazi kama haitaki biashara hii Zanzibar au wawadhibiti watu hawa,” alisema.

  Alidai kuwa matukio kama hayo ni ya muda mrefu na mwaka 2007 wakati wa Jumatatu ya Pasaka, baba yake mzazi, Ahandillal Asawla aliyekuwa akifanya biashara hiyo alimwagiwa tindikali usoni akafariki dunia.

  “Hata baba yangu aliuawa lakini hakuna hata mtu aliyekamatwa na Serikali haikufanya jambo lolote, sasa umefika wakati Serikali itulinde tunaofanya biashara hii au itangaze kusitisha kwa manufaa yetu,” alisema Asawla.

  Alisema cha kushangaza tangu ukoloni babu zake waliuza pombe kwa amani lakini sasa wanatumia pombe kama sababu za kisiasa ili kuangusha uchumi wa Zanzibar.

  Gazeti hili liliwasiliana na uongozi wa Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi bila mafanikio.
  Kwanza Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi, ACP Azizi Mohamed simu yake iliita bila majibu na simu ya Kamisha wa Polisi Zanzibar, CP Musa Musa haikupatikana pia.

  Baadaye gazeti hili lilifanikiwa kumpata Ofisa Uhusiano Polisi Zanzibar, Asha Mzule lakini alisema kuwa ni mgonjwa kwa muda kidogo hivyo hajui kinachoendelea na kutoa namba ya simu ya OCD wa Wilaya ya Mji Mpya.

  Hata hivyo OCD huyo alikataa kuzungumzia uvamizi huo wala kutaja jina lake lakini akashauri atafutwe ACP Azizi ambaye alidai yuko Uwanja wa Ndege akimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein anayetokea nje ya nchi.
  Namba ya ACP Azizi ilipopigwa kwa mara ya pili, haikupatikana kabisa.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mhhhh.... Siungi mkono pombe na siungi mkono walivyohatarisha maisha ya mama mjamzito . Si bora wangechoma baa .. hawa watu watakua na ugomvi mwengine issue sio pombe..
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kama hiyo ndiyo sera ya Zanzibar basi watangaze watu tujue. Otherwise ni uhalifu na waliofanya mashambulizi hayo waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
   
 4. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani tuwaacheni na mila zao
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  ndio sera za kina jussa hizo. Cuf kuikomboa na kuitetea zanzibar
   
 6. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili suala ni serious jamani tuache utani,zanzibar sio mbali na dar,imeanza zanzibar kesho dar!
   
 7. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,336
  Trophy Points: 280
  Hawa wa Zanzibar are uncivilized .
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kweli maana hata wajomba zake jussa wanawachoma moto mpaka kulazwa!!!
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi ndio maana sikuzote nasema tuwaachie hawa jamaa nchi yao hatuendani. Kwanini kulazimisha?
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  acha uoga kijana..
   
 11. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nyerere hakujua tu, bora tungejipendekeza kwa rwanda na Burundi kuliko hawa wapuuzi wa zanzibar, makelele tu hawaeleweki eleweki, pombe hawataki lakini wanakunywa, wanakunywa kweli kweli si mashehe, si walimu wa dini yao ya uislamu,wanataka nini hawa? pumbavu zao
   
 12. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sema natumia simu, ingekua natumia computer ungepata like kama mia hivi.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Asilimia kubwa ya VAT inayokusanywa Zanzibar inatokana na mauzo ya pombe. Kwa maneno mengine pombe inachangia sana kwenye mapato ya ndani Zanzibar. Serikali kila siku inakusanya kodi ya pombe, sasa kama hawataki iuzwe kwa nini wanakusanya kodi?

  Pili, utalii na pombe ni kama chanda na pete. Wanasiasa (ambao wengi wao wanamiliki mahoteli ya kitalii) wanaweza kukaa kimya lakini haya matukio ya watu kupigwa risasi au baa kuchomwa moto yatakula kwao. It is only a matter of time kabla hili bomu wanalonyamazia halijalipuka. Kama mtu haunywi pombe kwa nini uingilie uhuru wa mwenzio? Huu utakatifu wanataka watu waamini ni upi? Kuna sehemu yenye tatizo la uasherati kama Zanzibar? Hivi kumuuiza mtu nako sio kutenda dhambi?
   
 14. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  na ivi wanavyolilia muungano ufe, hapo itakuwa heri yetu. ntauza kiwanja changu mapema huko iwe ni ishara ya kuwahama. pia wasije wakanipora au kama wanavyodai nilipe kodi ya ardhi kwasbabu natoka tanganyika. ivi na huku tanganyika wanalipia?
   
 15. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu sina uoga wowote ila napenda tu ustaarabu na uelewa.... Kila nkiangalia tunachofaidika na huu muungano sikioni zaidi ya wapemba na waunguja kuwa magavana kule bungeni na kwingineko kwenye serekali ya muungano. Wamejazana kila mahali hapa dar wanaendesha maisha yao bila bugudha tena kwa kuwabagua wabara ambao hata ni majirani zao..... (arabic culture). Wao kuongoza wizara na maeneo yasiyo ya muungano ruksa. Wamewachomea vibanda Watanganyika wenzetu na wanawafanyia kila ufedhuli sisi ndo kwanza tupo usingizini... Sheria zao za kitumbafu kabisa kuwabagua Watanganyika ndio sera yao kutaka wawe nchi huru ndani ya muungano ndicho wanachowaza kila kukicha.... nahisi wabara watakapoamka usingizini huu muungano utaishia pabaya.
   
 16. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kafiri hachagui maneno ! Ndio maana Wayahudi walimwambia Musa A.S amlete Mwenyezi peupe uwanjani !
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ulitaka tujue kama una kiwanja huku Zanzibar? :focus:
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kusema Zanzibar nje ya muungano ni Somalia nyingine baadhi ya wanajamvi wakakataa leo wakiaangalia kinachoendela bila shaka watabadili misimamo yao.
   
 19. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Miaka ileee walipojaribu kuvunja mabucha ya nguruwe walifanywaje? Mimi huwa kila siku najiuliza...ni Mungu gani anayefurahia matendo wanayofanya wenzetu?
   
 20. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  [/QUOTE]  Nenda na wewe ukaibe.... Mtabaki kupiga kelele tu. Hayo ndo madhara ya kujifunza kusoma kwa kuanzia kulia kwenda kushoto. Matokeo yake hata mawazo na hoja zako zinakuwa kihivyo. Huwezi kuwa mbunifu na kuwaza maendeleo badala yake unawaza kuwa ...tunaonewa.... wanapendelewa..... endeleeni na ukenge huo sasa tunaingia kwenye jumuiya ya Africa Mashariki ushindani nje nje halafu tuone mtampigia nani kelele.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...