Kuuza pombe Zenj is a death sentence!

Status
Not open for further replies.

Asawla alisema baada ya hapo hakujua kinachoendelea mpaka alipozinduka Kituo cha Polisi cha Malindi walipopatiwa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja walipopigwa picha za x-ray na kugundulika wana risasi mwilini.
Tanzania mgonjwa aliyezirai na bullet wounds za uso hakimbizwi emergency room, anapelekwa polisi kuchukua PF3! Jinsi akili yetu inavyo run kinyume nyume!

By the way, mhariri, sio kila msomaji wako anaelewa PF3 ni kitu gani, jaribu kuelimisha umma ili mtu ajue akijeruhiwa njiani lazima akimbie akapate Police Form 3 kwanza kabla hajaenda hospitali. Press letu bana, sijui nifungue chuo cha journalism?
 
hawana lolote si waende kwenye ile kambi ya jeshi migombani wakawapige risasi kwa zile bia zao za buku buku (1000) wamewaonea hao magabachori tu
 
Kama hiyo ndiyo sera ya Zanzibar basi watangaze watu tujue. Otherwise ni uhalifu na waliofanya mashambulizi hayo waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Wanataka amani ya nchi itoweke kabisa, kama muuza pombe anatakiwa auawe je sisi wanywaji? Mimi natamani sana Tujitenge na Wanzanzibar waendelee kuishi kiislam kwa raha zao, maana tukiendelea nao nahisi ipo siku watajitokeza waislam wenye msimamo mkali wa Bunju/Boko haram,
 
Eti unasema bora wangemchomea baa tu!, kwa hiyo wewe unamwonea huruma mjamzito tu!?

Mimi imani yenu hii naishangaa na ntaendelea kuishangaa!!!
Pombe iwe haramu duniani tu....lakini eti paradiso ya waislamu itajaa mito ya pombe ...na waislamu wataoenda huko watakuwa wanakunywa kwa kila wakati huku wakiwa na wanawake arobaini wenye bikra zisizoisha!!
Pombe ni haramu duniani lakini mbele ya Mungu wenu ni halali kabisa!!......waislamu fikirieni bwana!! mnapotea.

nyamaza ww unaujua uislamu wewe!!!??? Co lazma itangazwe, si mmeshajua kuwa pombe ni htr? Ss acheni kuuza muwe salama au uzeni ili muhatarishe maisha yenu.
 
WAFANYABIASHARA YA POMBE WAPIGWA RISASI ZANZIBAR



Mfanyabiashara Alvind Asawla aliyepigwa risasi katika paji la uso ikatokea shingoni na kumwagiwa tindikali Zanzibar, akiwa na mkewe Bimal katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatano iliyopita. (Na Yusufu Badi).

WAFANYABIASHARA wawili mtu na mkewe, wamepigwa risasi na kumwagiwa tindikali huko Zanzibar kwa kuuza pombe.

Katika uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita mwanamke Bimal Alvind (36) alinusurika kupoteza ujauzito wake wa miezi minne baada ya kupigwa risasi ya tumbo na kumwagiwa tindikali.

Risasi hiyo ilitolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuathiri ujauzito huo lakini tindikali hiyo ilimjeruhi mwilini kuanzia usoni, kifuani kwenye matiti, mikono yote miwili na tumboni.

Mumewe, Alvind Asawla (42) alipigwa risasi kichwani kwenye paji la uso katikati ya macho iliyotokea nyuma chini ya shingo na sasa amepooza upande mmoja.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwa ndugu yake Upanga wiki hii, Asawla alisema walivamiwa Jumatano iliyopita saa 10:30 jioni katika Mtaa wa Hurumzi Mji Mkongwe.
Alisema wakati wakivamiwa, yeye na mkewe aliyeishi naye kwa miaka 17 sasa na kujaliwa watoto wawili; Priyanka (14) na Nidh (12), walikuwa wakitoka katika biashara yao wakirudi nyumbani eneo la Kiponda.

Alisema ghafla watu wawili walimvamia mkewe na kummwagia tindikali na yeye alipokuwa akijaribu kumsaidia, watu hao walimmwagia tindikali usoni.

Kwa mujibu wa Asawla, wakati wakitaharuki kwa hali hiyo, ghafla alitokea mtu mwingine na kumpiga risasi katika paji la uso akadondoka chini huku damu zikimtoka.

Alisema alijaribu kujikongoja kwa nia ya kuendelea kumsaidia mkewe lakini mtu huyo wa tatu alimpiga risasi ya pili mgongoni na mkewe akapigwa risasi ya tumbo.



Asawla alisema baada ya hapo hakujua kinachoendelea mpaka alipozinduka Kituo cha Polisi cha Malindi walipopatiwa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja walipopigwa picha za x-ray na kugundulika wana risasi mwilini.

Baada ya kipimo hicho, Asawla alisema hospitali hiyo haikuwa na vifaa vya kutoa risasi hizo, ndipo ndugu zake waliwasaidia usiku huo na kuwasafirisha kwa ndege hadi Dar es Salaam ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alisema mkewe alilazwa katika wadi ya Kibasila namba tatu na yeye akahamishiwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kipimo cha CT-Scan ambacho hakikupatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa Asawla, mke wake alitolewa risasi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na yeye kufanyiwa upasuaji wa kumtoa risasi ulifanyika katika Hospitali ya TMJ.
Alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ni mzima hadi sasa kwani alipigwa risasi sehemu mbaya na kukaa nayo kwa saa zaidi ya 12 ndipo ilipotolewa kichwani jambo lililowashangaza hata baadhi ya wauguzi.

“Nimepooza upande mmoja wa kichwa changu, sihisi jambo lolote lakini madaktari wameniambia nitarudi katika hali yangu ya kawaida polepole baada ya kufanya mazoezi,” alisema.

Alisema aliambiwa kuwa risasi hizo hazikupita katika mishipa mikubwa ndiyo maana yuko hai hadi sasa na mshipa mdogo uliomwaga damu, umefanya jicho la upande uliopooza kuwa jekundu licha ya kuona vizuri.

Mfanyabiashara huyo alisema kuwa watu hao wamempa ulemavu wa kudumu bila kutegemea huku akiamini siyo majambazi ingawa walichukua pochi ya mkewe iliyokuwa na fedha kidogo.

Alisema hospitalini wameambiwa tindikali waliyomwagiwa ni aina ya asidi sulfuriki (sulphuric acid) inayotumika katika magari.

“Unajua mwizi anataka fedha na siyo kumwagia tindikali au kukupiga risasi na sisi hatukuwa na silaha yoyote; nia ya watu hawa ni kutuua kwani tumekuwa tukipata vitisho vya mara kwa mara kutokana na biashara yetu ya kuuza pombe Zanzibar,” alidai.

Alidai mara kwa mara wamekuwa wakipata vitisho ikiwemo kukuta karatasi inayomtaka kuacha biashara hiyo vinginevyo utauawa; na wamekuwa wakitoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na biashara zao.

Alilalamika kuwa licha ya wafanyabiashara wengi wa pombe kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupiwa risasi na hata kuchomwa moto, hakuna aliyewahi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
“Sisi tunafanya biashara na mahoteli makubwa ya kitalii na tunalipa kodi zote stahiki, Serikali iseme wazi kama haitaki biashara hii Zanzibar au wawadhibiti watu hawa,” alisema.

Alidai kuwa matukio kama hayo ni ya muda mrefu na mwaka 2007 wakati wa Jumatatu ya Pasaka, baba yake mzazi, Ahandillal Asawla aliyekuwa akifanya biashara hiyo alimwagiwa tindikali usoni akafariki dunia.

“Hata baba yangu aliuawa lakini hakuna hata mtu aliyekamatwa na Serikali haikufanya jambo lolote, sasa umefika wakati Serikali itulinde tunaofanya biashara hii au itangaze kusitisha kwa manufaa yetu,” alisema Asawla.

Alisema cha kushangaza tangu ukoloni babu zake waliuza pombe kwa amani lakini sasa wanatumia pombe kama sababu za kisiasa ili kuangusha uchumi wa Zanzibar.

Gazeti hili liliwasiliana na uongozi wa Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi bila mafanikio.
Kwanza Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi, ACP Azizi Mohamed simu yake iliita bila majibu na simu ya Kamisha wa Polisi Zanzibar, CP Musa Musa haikupatikana pia.

Baadaye gazeti hili lilifanikiwa kumpata Ofisa Uhusiano Polisi Zanzibar, Asha Mzule lakini alisema kuwa ni mgonjwa kwa muda kidogo hivyo hajui kinachoendelea na kutoa namba ya simu ya OCD wa Wilaya ya Mji Mpya.

Hata hivyo OCD huyo alikataa kuzungumzia uvamizi huo wala kutaja jina lake lakini akashauri atafutwe ACP Azizi ambaye alidai yuko Uwanja wa Ndege akimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein anayetokea nje ya nchi.
Namba ya ACP Azizi ilipopigwa kwa mara ya pili, haikupatikana kabisa.

Any assault/violence against a person is evil. If it's done in the name of religion is devolish!
 
Ndo maana nawapeleka wanangu shule za maana, make najua ustarabu ni zao la kuelimika. Ku analyse mambo kwa kufanya fujo ni dalii ya jamii yenye utata wa shule.
 
Huyajui madhara ya Pombe ndio maana unaleta maneno yako mbofu mbofu hapa.Uislam uliyajua madhara yake na ndio maana ilikatazwa.
 
Na hawa Wahindi nao machizi, hao.

....Yaani wamekosa sehemu zote za kuuzia Pombe, hadi wakauze Zanzibar? Kisha wanauzia mitaa ya wenyeji? Hawajui kwamba kuna tofauti ya mila na mifumo ya maisha kati ya sehemu na sehemu?. Mbona hao wazungu wenye hoteli za kitalii hawauzi pombe maeneo ya wenyeji?:A S 13:
 
mtu ambayeanajifanya kujua dini sana huyu sio mdini bali hujazwa na roho ya kishetani akijifanya kutetea dini , mtu anayejua dini kiasi hufundishwa huruma, ukarimu na upendo, hawa ni zaidi ya shetani, bora dini zote zifutwe kwani tumeshindwa kusoma na kuelewa vizuri vitabu hivi wanavyosema ni vitakatifu, upi utakatifu wa kunyofoa roho ya mtu.? Zanzibar ni Nigeria ya Pili naapa siendi huko kwa kuwa siwezi acha ka kinywaji kangu ka kesteri
 
Tangu lini ubaya ukalipwa kwa ubaya. Je hatufundishwi kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayepaswa kuhukumu?
 
ndio maana nasema siku zote, hakuna haja ya kumchagua mzanzibari kuwa raisi wa tanzania. madawa ya kulevya yanauzwa nje nje zanzibari lakini sijasikia hata siku moja muuza madawa ya kulevya kachomwa moto huko znz. madawa ya kulevya ni hatari sana kuliko pombe, lakini kwa sababu wauzao ni waislamu, hawafanywi lolote. jamani tuwafukuze bara wazanzibari wote!
 
Drugs zimejaa Znz na ndo njia kubwa ya kupitishia drugs.

Wao wanaona pombe ndiyo mbaya.
 
Wewe Ndunilakuwili, kitabu chenu kinajikanganya Yesu mnasema ni mtume alafu sadahivi unamtukana, hivi Wewe ni mwehus au kichaas maana natafakari nashindwa nikuweke group gani, yaani kwanza ni kichekesho.....ushoga yes, pombe no. hapo kaazi ipo.

Unajua kusoma sawa sawa au pombe zako ndio zinakutuma! Hapo nimeonyesha mfano kwa kusema: kama ungeambiwa yesu aliku ......ungejisikiaje?. Nikaachia swali hapo. Nimesema hivyo kwa sababu kwa akili yangu mbovu unaamini yesu ni Mungu. Kwa hiyo nilikuwa nimaana angejisikiaje kama angeambiwa Yesu ni ......... Halafu una uhakika gani kama kilichofichwa hapo ni tusi na wala siyo sifa? Nikikwambia hakuna tusi hapo bali ni sifa utabisha?
 
Mona Kati mahoteli pome zinauzwa Hugo Zanzibar.,, na kwa mini sijasikia mzungu kachomewa moto hoteli au baa za kizungu. Kwa nini raisi aw znz anapofungua mahoteli au sherehe Hugo znz Mbona hatangaz Kuwait pome haitanywewa ktk sherehe.?
 
Mkuu Sweke, umenikumbusha kitu, hivi unajua walivunja bucha ya nyama ya nguruwe kisha wakabeba nyama na vifaa vyote vya kuuzia nyama?!, nadhani kwao la muhimu ni wivu wa kibiashara maana wanaona jinsi wauza pombe zanzibar wanavyovuna mpunga wa nguvu wakati wao hawawezi kuingia kwenye ujasilia mali huo ndo maana wanamaua kuwaumiza ili waondoke.
Miaka ileee walipojaribu kuvunja mabucha ya nguruwe walifanywaje? Mimi huwa kila siku najiuliza...ni Mungu gani anayefurahia matendo wanayofanya wenzetu?
 
Quran 47: 15 “Mfano wa pepo walioahidiwa wacha Mungu (itakuwa hivi) : imo mito ya ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa; tena humo watapata matunda ya kila namna, na samahani kwa mola wao. Basi wao watakuwa sawa na wale watakao kaa motoni na kunyweshwa maji ya chemkayo yatakayokata chango zao.” Mwisho wa kunukuu…

Sasa hapa tunaona Allah akbar yeye ameandaa mito kabisa ya pombe wala siyo chupa wala glasi!!!!!!!!!!

Angalia nahii…Quran 56:20-22 “ Na matunda (namna kwa namna) kama watavyopenda. Nanyama za Ndege kama watavyotamani(wenyewe). Nawanawake wenye macho mazuri na makubwa, (ya vikombe)”

Mkuu la wanawake 40 wasioisha bikra huku dhakari zikiwa hazisinyai…..naendelea kulitafuta……kitabuchao kigumu sana …lakini naendelea kuchakura ntawajuvya wooote….
Mnaobisha na kuniona mzushi.. mjionee kituko mnacho kiamini....

Angalizo: kuna tabia ya kuondoa post zilizonukuu quran naoma anaefanya hivyo hii aieche kwani huu si uzushi ni andiko kamili, mwenye hoja apinge kwa hoja.

Unapokuwa unashusha aya hizo kwa mbwembwe usisahau kuwa kila aya ina maelezo ya ufafanuzi pale chini. Hayo ndiyo yanayomfunulia msomaji maana ya kilicho andikwa. Angalia usiende mbio ukawapotosha watu. Nukuu aya uwawekee na ufafanuzi wake.
 
naona humu kuna waislamu wakorofi...mmepewa aya sasa cha kufanya tupeni maana yake ugomvi uishe...kumbukeni wote sisi ni ndugu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom