Kuumbeee, hata magazeti ni mafisadi...!!

Hivi ndivyo watanzania wanavyowajaza mapesa mafisadi

Viwango vilivyokuwa vinatumika
Mapato na kodi kwa mwezi

Shilingi 0 mpaka Shilingi 80,000 -Asilimia sifuri
Shilingi 80,001 mpaka Shilingi 180,000 -Asilimia 15 ya kiasi kinachozidi Shilingi 80,000
Shilingi 180,001 mpaka Shilingi 360,000 -Shilingi 15,000 kuongeza asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Shilingi 180,000
Shilingi 360,001 mpaka Shilingi 540,000 - Shilingi 51,000 kuongeza asilimia 25ya kiasi kinachozidi Shilingi 360,000
Zaidi ya Shilingi 540,000 - Shilingi 96,000 kuongeza asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Shilingi 540,000

Viwango Vipya
Mapato na kodi kwa mwezi

Shilingi 0 mpaka Shilingi 100,000 - Asilimia sifuri
Shilingi 100,001 mpaka Shilingi 360,000 - Asilimia 15 ya kiasi kinachozidi Shilingi 100,000
Shilingi 360,001 mpaka Shilingi 540,000 - Shilingi 39,000 kuongeza asilimia 20ya kiasi kinachozidi Shilingi 360,000
Shilingi 540,001 mpaka Shilingi 720,000 - Shilingi 75,000 kuongeza asilimia 25ya kiasi kinachozidi Shilingi 540,000
Zaidi ya Shilingi 720,000 - Shilingi 120,000 kuongeza asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Shilingi 720,000

Wengine wetu tunalipa kodi mpaka laki tatu na zaidi mtu unashangaa kwa nini kampuni kubwa kama Voda isilipe kodi.

Shilingi 0 mpaka Shilingi 80,000 -Asilimia sifuri (HATA HILI KUNDI HULIPA KODI KUPITIA BIDHAA WANUNUAZO DUKANI NA KWINGINEKO ILI KUKIDHI MAHITAJI YAO YA KILA SIKU)
 
Sidhani kama huyo mbunge amesema makampuni mengine ya simu yanalipa kodi. Najua kampuni kama Tigo inastahili kuwemo kwenye "tax holiday". Mbunge amezungumzia urefu wa tax holiday. Hoja yake ameijenga vizuri baada ya kuweka figures ambazo zinaonyesha ni kiasi gani Vodacom wanapata kutokana na tax holiday. Kama faida wanayopata ni kubwa kuliko kiasi cha fedha wanachopata basi hawastahili extension ya tax holiday. Kwa upande wangu bila kuangalia ni kiasi gani cha faida wanachopata au uhusiano wao wa kibiashara na RA, leo hii kama Vodacom ikifa, sehemu nyingi za nchi yetu huko vijijini zitakosa mawasiliano ya simu na niwajibu wa serikali kuilinda kwa sababu ina cover moja ya wajibu wake wa kuhakikisha kuna mawasiliano sehemu yote ya nchi. Ningependa sana kujua mawazo ya Mnyika wa CHADEMA kwenye hili kwa maana yeye anatumia Voda for years.

Si kweli kwamba voda ikifa sehemu nyingi zitakosa mawasiliano! Kumbuka celtel imeenea kila sehemu aliko voda huko vijijini hata kijijini kwenu. Watu watahamia celtel na mawasiliano yataendelea.
 
bubu Ataka Kusema,
Hivi Kweli Watu Wenye Kipato Kidogo Wanalipa Kodi Tanzania? Naomba Uziorodheshe Kodi Wanazolipa Na Viwango Ili Tuanze Kuzipigania Hapa.
Halafu Kuna Jambo Jingine Hapa Inabidi Tuwe Wazi, Unapokuwa Mfanyabishara Lengo Lako Kubwa Ni Kupunguza Gharama Na Kuongeza Kipato. Kama Umeweza Kupunguza Gharama Kama Vodacom Basi Wewe Ni Mfanyabishara Mzuri. Kwa Mawazo Yangu Hapa Wa Kulaumiwa Ni Aliyotoa Msamaha Huo. Jambo Jingine La Kuangalia Ni Faida Gani Taifa Limepata Kutokana Na Msamaha Huo Wa Kodi. Kama Vodacom Isingekuwepo Taifa Lingepata Faida Gani Au Hasara Gani. Lazima Tukumbuke Ili Kuendelea Kiuchumi "communication" Is No.1 Factor.

Yaani Wewe Unataka Kusema Sisi Masikini Hatulipi Kodi???????? Na Hiyo Paye Ni Nini??? Kumbe Vibwengo Wa Mabepari Mmefika Huko? Hujui Faida Ya Voda Kulipa Kodi?

Leo Nimeumia Sana Ndugu Yangu; 30% Ya Income Yangu Hadi Aloowance Ya Daladala Nakatwa "pay As You Earn" Na Voda Ina Maana Hawa-"earn"????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom