BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 5,717
- 3,573
Naombeni Msaada. Siku ya Jumanne kuna Mbunge wa Upinzani alisimama na kutoa hoja akihoji juu ya Kampuni ya Simu ya VodaCom kupewa likizo nyingine kulipa kodi. Kwa bahati mbaya sikusikia jina la Mbunge mwenyewe wala tarakimu za Mabilioni yaliyotajwa. sikuwa na wasiwasi, nikasubiri kesho yake ili kuisoma kwa undani taarifa ile. Kwa Mshangao wangu, hakuna hata gazeti moja lililoandika kuhusu habari ile ambayo mimi nilidhani kuwa ingekuwa 'front page news'!! Mpaka leo Jumamosi ninapoandika habari hii, hakuna hata gazeti moja ambalo limeiandika habari ile. Wakati nikiomba mtu mwenye uwezo wa kupata Hansard za Bunge atuwekee hapa hoja ile tuisome vizuri, bado nimeshangazwa na unafiki wa magazeti ya Tanzania wa kupigia kelele mafisadi lakini yenyewe kwa kuogopa kupewa matangazo ya Vodacom yameacha kuandika habari ile muhimu...!!HUU SI UFISADI???
Last edited: