choupa moting
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 1,508
- 2,577
Wakuu naomba kuuliza. Takribani wiki moja sasa nchi ya Tanzania imekumbwa na msiba wa bilionea maarufu Dr. RA Mengi lakini katika hali isiyo ya kawaida sijaona bwana nywele nyeupe. Huyu ndugu kwa kawaida hakosagi misibani au popote penye huzuri hutokea kufariji watu lakin safari hii imekua tofaut na hata ukizingatia ni mtu wa njia moja na marehem, amekumbwa na nini huyu mzee? Lakini je yupo nchini kweli? Maana toka ameenda kupokelewa kule kijijini kwake baada ya kurudi CCM hajaonekana tena si kwenye gazeti wala kipeperushi. Yuwap huyu mzee? Je mzima huko aliko?