stubborn wa Njombe
Member
- Dec 8, 2016
- 79
- 170
Habari za wakati huu,
Baada ya ukimya wa muda mrefu sana leo nimerudi tena kwa ajili ya kuwapa mrejesho wa maendeleo ya afya yangu kwa ujumla wake.
Kwa ambao hawakumbuki ni kuwa mara ya mwisho nilikuwa nasumbuliwa na typhoid na bawasiri, nashukuru Mungu kwa ushauri wa wanaJF nilitumia dawa nilizoelekezwa bawasili ilipona na typhoid ilipona ila bado uzito wangu ukawa unashuka chini kwa kasi ya ajabu sana. Nikaenda hospitali yetu ya rufaa ya wilaya na kuwaeleza kwa sababu nilikuwa bado na yale maumivu ya upande wa kulia chini ya mbavu.
Tabibu niliyemkuta alishauri nipige picha ya X ray tu hivyo nilipopata majibu ikagundulika nina TB ya nje ya mapafu ndio maana sikuw nikikohoa ingawa baadhi ya dalili nilikuwa ninazo kama vile kutoka jasho jingi sana wakati wa usiku na kuwa na homa za jioni kila siku.
Kabla ya kuanza dawa za TB nilipima tena maambukizi ya VVU nikaonekana sina hayo maradhi ingawa nilikuwa nina uzito wa Kilo 42 kwa wakati ule.
Nilianza dawa na kufuatilia masharti yote muhimu nashukuru Mungu mwezi uliopita 19/10 ndio nilimaliza kumeza dawa na afya yangu inaendelea vizuri yale maumivu chini ya mbavu hayapo tena na uzito wangu sasa hivi ni kilo 61 ambazo ni uzito wangu wa kawaida ninapokuwa sina maradhi yoyote.
Natoa wito kwa wapendwa wangu wa JF kuwa pale unapohisi shida ndani ya mwili wako wahi haraka hospitalini kwa ajili ya vipimo na ushauri kwani maradhi mengine yakichelewa kutibiwa yanakuwa sugu na tiba yake inakuwa ngumu zaidi. TB inatibika kwa uhakika zaidi hospitalini hasa ukimeza dawa kwa usahihi na kuzingatia lishe bora wakati wote wa matababu na baada ya matibabu.
Nahitimisha kwa kuwashukuru wana JF wote mlionichangia mawazo yenu mpaka leo nipo hai na kuweza kuandika tena uzi kwenye forum yetu pendwa.
Nawatakia siku njema.