Kuuelewa Mgogoro wa CHADEMA na Kuumaliza Kuuelekea 2015

EMT, asante kwa mchango huu. I wish ningekuwa nimeisoma hii kabla lakini it just confirms your point.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mzee Mwanakijiji

Shukrani kwa bandiko lako,
Ninasubiri sehemu ya nne na tano, lakini mpaka katika sehemu hii ya tatu nimeanza kuona makosa ambayo kwa gwiji wa mambo ya siasa kama wewe lazima unafahamu na umeamua kwa maksudi kutoyachambua na kwa kufanya hivyo, ninaona pia itakuwa ni kutowatendea haki wanaJf ambao hawafahamu nadharia nzima ya nidhamu katika vyama vya siasa (Tanzania). Hasa ikuchukuliwa kuwa nidhamu ni matokeo ya mfumo wa uendeshaji ndani ya taasisi.

Katika makala zako nyingi ambazo nimezisoma, kila mara huwa una jaribu kuwakosoa wanabodi katika msisitizo wa fallacious argumentation ambao unatokea kwenye makosa ya msingi wa hoja (proposition) ambapo pasi na shaka hata kwenye hitimisho (conclusion) kutakuwa na makosa.

Katika makala yako hii umesema,
Matumaini yangu ni kuwa hoja nitakayoiweka hapa itatoa pendekezo bora zaidi la kumaliza mgogoro CDM (na wengine wanaweza kujifunza) kuliko mapendekezo mengine yote yaliyowahi kutolewa na wengine kabla.

Mgogoro wa CHADEMA hauwezwi kumalizwa na mapendekezo ya utatuzi wa matokeo ya mfumo (nidhamu) bila kutatua mfumo unaojenga nidhamu katika taasisi. Viongozi wa chama na nidhamu zao ni matokeo ya mfumo wa chama.

Mwl. Nyerere alishawahi kusema, chama legelege huzaa Serikali legelege, kwa maana kwamba, chama kinakuwa legelege (utovu wa nidhamu) kutokana na ubovu wa mfumo wake. Huwezi kutegemea kupata nidhamu kwa viongozi legelege na viongozi legelege ni chachu ya mifarakano katika chama kwa sababu wanakuwa hawana nguzo za kiuongozi mathubutu.

Kuponya mfumo wake ndiyo kuponya tatizo la nidhamu ndani ya chama, kwa sababu mfumo mathubuti huzaa viongozi mathubuti.

Nimekubaliana na wewe 100% uliposema,
Nimesema hapo juu kuwa tatizo hili au chanzo hiki cha mfumo na muundo wa chama kinasababisha tatizo la pili ambalo wote tunaliona. Hili la kwanza linahitaji kutulia na kulichambua kwa kina kuweza kuona jinsi gani linasababisha migogoro lakini hili la pili ni rahisi kulionesha kuwa linasababisha migogoro kwa sababu wahusika wamesimama kwenye mfumo mbovu wa chama; mfumo ambao ulitakiwa ubadilishwe mara tu ya uchaguzi wa 2010; mfumo ambao sidhani kama utabadilika wakati wowote sasa hivi hasa kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mitaa mwakani. Mfumo huu unasababisha tatizo lisilokoma la Utovu wa Nidhamu (Indiscipline).

Kwa mtazamo wangu bila kuongelea kwa kina jinsi mfumo ulivyo mbovu wa chama na kutoa mapendekezo ya kuurekebisha, hata haya mapendekezo yako ya tatizo la pili (nidhamu) yatakuwa ni sawa na kumpa mgonjwa dawa ya kupunguza maumivu kwa muda na siyo kupona.

Fikra zangu zinaniambia umeamua kutogusia kwenye hii mada muhimu ya mzizi wa tatizo ambao ni ubovu wa mfumo wa CHADEMA kwa sababu mada yako ina malengo fulani fulani ambayo utayabeba kwenye hitimisho (conclusion) lako sehemu ya tano ambalo ninaamini litakuwa pia na makosa kwa sababu ya kukosa hoja ya msingi wa hoja yenyewe (mfumo wa CHADEMA).

Anyway, macho yangu bado nimeyafungua kusubiri sehemu ya nne na tano huku nikijiuliza, kama inawezekana kuweka jeshi na vyama vya siasa katika mzani mmoja wa nidhamu hasa ikichukuliwa kuwa nadharia ya nidhamu ya jeshi huwa inabebwa na nidhamu ya uoga (jeshini unatakiwa kutii amri kwanza harafu swali ni baadaye) wakati nidhamu ya kidemokrasia inabebwa na nidhamu ya hoja (unauliza swali kwanza kabla ya kutenda).
 
Wana JF, Salaam!

Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nje ya jukwaa hili! Kuna mambo mengi sana yamenipita na ambayo sikuweza kutoa michango yangu ili na mimi nionekane kuwa ni mtanzania halisi ndani ya tanzania yangu. ila kwa wale wote ambao wamechangia kwa njia moja ama nyingine katika kuepusha kimbunga hiki kisibomoe kuta zetu za CDM, kwa kweli nawapeni hongera sana.

Ninachotaka kusema hapa, ni kwamba haya yote yanayotokea kwa sasa ndani ya chadema si kwa bahati mbaya, bali ni mipango mikakati ya CCM ambayo kwa mtu yeyote anayejua jinsi siasa za kimafia zinavyoendeshwa na hivi ndivyo ilivyofanyika. Na vurugu zote hizi za Zitto amezifanya kwa malengo ya kutaka kukisambalatisha chama ili agawe kura za CDM kusudi CCM wabakie na kura zao zilezile ambazo zitaendelea kukipa ushindi.

Cha msingi hapa, Kama tumeweza kumvumilia mbunge mashuhuri wa misemo ya pwani wakati yeye ni msukuma, basi tuangalie na njia nyingine ya kuweza kuenda pamoja na watu hawa bila kuathili chama chetu na hatimae watadondoka wenyewe siku ikifika.

HIZONDIO SALAAM ZANGU KWAO
 
Zitto huwezi muweka kundi moja na shibuda ni dharau kubwa sana mnaendelea kuonyesha wanaCHADEMA kwa Zitto licha ya yote aliyofanya kwenye hichi chama

Nishasema humu kama kuna mtu anaushahidi juu ya huo unaoitwa uhaini na usaliti wa Zitto na auweke wazi hapa!!....HAKUNA!!!
 
Mzee Mwanakijiji

Kwa mtazamo wangu bila kuongelea kwa kina jinsi mfumo ulivyo mbovu wa chama na kutoa mapendekezo ya kuurekebisha, hata haya mapendekezo yako ya tatizo la pili (nidhamu) yatakuwa ni sawa na kumpa mgonjwa dawa ya kupunguza maumivu kwa muda na siyo kupona.

Fikra zangu zinaniambia umeamua kutogusia kwenye hii mada muhimu ya mzizi wa tatizo ambao ni ubovu wa mfumo wa CHADEMA kwa sababu mada yako ina malengo fulani fulani ambayo utayabeba kwenye hitimisho (conclusion) lako sehemu ya tano ambalo ninaamini litakuwa pia na makosa kwa sababu ya kukosa hoja ya msingi wa hoja yenyewe (mfumo wa CHADEMA).

Nina uhakika hujasoma yote niliyoandika hapo juu kwani nimetumia muda mrefu kuelezea tatizo la muundo na mfumo wa CDM.
 
Sehemu ya nne ya hoja yangu ya kuuelewa Mgogoro wa CDM na hatimaye kuupatia ufumbuzi wa kudumu inaendelea. Angalia posti ya kwanza.
 
Wana JF, Salaam!

Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nje ya jukwaa hili! Kuna mambo mengi sana yamenipita na ambayo sikuweza kutoa michango yangu ili na mimi nionekane kuwa ni mtanzania halisi ndani ya tanzania yangu. ila kwa wale wote ambao wamechangia kwa njia moja ama nyingine katika kuepusha kimbunga hiki kisibomoe kuta zetu za CDM, kwa kweli nawapeni hongera sana.

Ninachotaka kusema hapa, ni kwamba haya yote yanayotokea kwa sasa ndani ya chadema si kwa bahati mbaya, bali ni mipango mikakati ya CCM ambayo kwa mtu yeyote anayejua jinsi siasa za kimafia zinavyoendeshwa na hivi ndivyo ilivyofanyika. Na vurugu zote hizi za Zitto amezifanya kwa malengo ya kutaka kukisambalatisha chama ili agawe kura za CDM kusudi CCM wabakie na kura zao zilezile ambazo zitaendelea kukipa ushindi.

Cha msingi hapa, Kama tumeweza kumvumilia mbunge mashuhuri wa misemo ya pwani wakati yeye ni msukuma, basi tuangalie na njia nyingine ya kuweza kuenda pamoja na watu hawa bila kuathili chama chetu na hatimae watadondoka wenyewe siku ikifika.

HIZONDIO SALAAM ZANGU KWAO

hili ni jukwaa la GT, uliyoaandika hapa ni invalid kama hauna evidence, weka evidence please
 
images
 
Back
Top Bottom