Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
- Thread starter
- #101
EMT, asante kwa mchango huu. I wish ningekuwa nimeisoma hii kabla lakini it just confirms your point.
Matumaini yangu ni kuwa hoja nitakayoiweka hapa itatoa pendekezo bora zaidi la kumaliza mgogoro CDM (na wengine wanaweza kujifunza) kuliko mapendekezo mengine yote yaliyowahi kutolewa na wengine kabla.
Nimesema hapo juu kuwa tatizo hili au chanzo hiki cha mfumo na muundo wa chama kinasababisha tatizo la pili ambalo wote tunaliona. Hili la kwanza linahitaji kutulia na kulichambua kwa kina kuweza kuona jinsi gani linasababisha migogoro lakini hili la pili ni rahisi kulionesha kuwa linasababisha migogoro kwa sababu wahusika wamesimama kwenye mfumo mbovu wa chama; mfumo ambao ulitakiwa ubadilishwe mara tu ya uchaguzi wa 2010; mfumo ambao sidhani kama utabadilika wakati wowote sasa hivi hasa kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mitaa mwakani. Mfumo huu unasababisha tatizo lisilokoma la Utovu wa Nidhamu (Indiscipline).
Wana JF, Salaam!
Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nje ya jukwaa hili! Kuna mambo mengi sana yamenipita na ambayo sikuweza kutoa michango yangu ili na mimi nionekane kuwa ni mtanzania halisi ndani ya tanzania yangu. ila kwa wale wote ambao wamechangia kwa njia moja ama nyingine katika kuepusha kimbunga hiki kisibomoe kuta zetu za CDM, kwa kweli nawapeni hongera sana.
Ninachotaka kusema hapa, ni kwamba haya yote yanayotokea kwa sasa ndani ya chadema si kwa bahati mbaya, bali ni mipango mikakati ya CCM ambayo kwa mtu yeyote anayejua jinsi siasa za kimafia zinavyoendeshwa na hivi ndivyo ilivyofanyika. Na vurugu zote hizi za Zitto amezifanya kwa malengo ya kutaka kukisambalatisha chama ili agawe kura za CDM kusudi CCM wabakie na kura zao zilezile ambazo zitaendelea kukipa ushindi.
Cha msingi hapa, Kama tumeweza kumvumilia mbunge mashuhuri wa misemo ya pwani wakati yeye ni msukuma, basi tuangalie na njia nyingine ya kuweza kuenda pamoja na watu hawa bila kuathili chama chetu na hatimae watadondoka wenyewe siku ikifika.
HIZONDIO SALAAM ZANGU KWAO
Mzee Mwanakijiji
Kwa mtazamo wangu bila kuongelea kwa kina jinsi mfumo ulivyo mbovu wa chama na kutoa mapendekezo ya kuurekebisha, hata haya mapendekezo yako ya tatizo la pili (nidhamu) yatakuwa ni sawa na kumpa mgonjwa dawa ya kupunguza maumivu kwa muda na siyo kupona.
Fikra zangu zinaniambia umeamua kutogusia kwenye hii mada muhimu ya mzizi wa tatizo ambao ni ubovu wa mfumo wa CHADEMA kwa sababu mada yako ina malengo fulani fulani ambayo utayabeba kwenye hitimisho (conclusion) lako sehemu ya tano ambalo ninaamini litakuwa pia na makosa kwa sababu ya kukosa hoja ya msingi wa hoja yenyewe (mfumo wa CHADEMA).
Wana JF, Salaam!
Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nje ya jukwaa hili! Kuna mambo mengi sana yamenipita na ambayo sikuweza kutoa michango yangu ili na mimi nionekane kuwa ni mtanzania halisi ndani ya tanzania yangu. ila kwa wale wote ambao wamechangia kwa njia moja ama nyingine katika kuepusha kimbunga hiki kisibomoe kuta zetu za CDM, kwa kweli nawapeni hongera sana.
Ninachotaka kusema hapa, ni kwamba haya yote yanayotokea kwa sasa ndani ya chadema si kwa bahati mbaya, bali ni mipango mikakati ya CCM ambayo kwa mtu yeyote anayejua jinsi siasa za kimafia zinavyoendeshwa na hivi ndivyo ilivyofanyika. Na vurugu zote hizi za Zitto amezifanya kwa malengo ya kutaka kukisambalatisha chama ili agawe kura za CDM kusudi CCM wabakie na kura zao zilezile ambazo zitaendelea kukipa ushindi.
Cha msingi hapa, Kama tumeweza kumvumilia mbunge mashuhuri wa misemo ya pwani wakati yeye ni msukuma, basi tuangalie na njia nyingine ya kuweza kuenda pamoja na watu hawa bila kuathili chama chetu na hatimae watadondoka wenyewe siku ikifika.
HIZONDIO SALAAM ZANGU KWAO
Naona watu wanasubiri umalize na wewe ndio kwanza unaleta nusunusu.