Kutumia picha ya watu bila ridhaa zao

Kutumia picha ya watu bila ridhaa zao

Wisest man

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
993
Reaction score
333
Wakuu habari nawasalimu sana kabla sijaleta hoja hapa ijadiliwe.

Ujio wa simu za kisasa na camera ndogo umerahisisha upigaji picha kama wengi tunavyojua kwa sababu baadhi yetu tunamiliki vifaa hivyo, hivyo ni jambo zuri sana kama hatua ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Jambo lilinifanya nilete mada hii kwenu ni kuona baadhi ya watumiaji wa mitandao ya internet hasa, instagram, facebook na whatsapp kuamua kutumia picha ya mtu mwingine labda ni marafiki, ndugu, mfanyakazi mwenzake, jirani, au mtu yeyote tu wasiyemfahamu pasipo kupata ridhaa yake.

Sasa huwa najiuliza vipi unajuaje kwamba, mwenzako angependa kusikia picha yake ipo instagram ikipigwa likevna watu asiowafahamu? Kuna watu wanapenda sana privacy zao na hawapendi kutumia mitandao kuweka picha zao, je kufanya hivyo si kuingilia uhuru wa mtu?

Sasa hivi matumizi yq mitandao imekuwa mikubwa na watu wamekuwa wakiathiriwa na baadhi ya watu wenye picha zao, je tuite ni utoto, ulimbukeni au ni dharau tu? Picha nyingi zinazotumika kama vichekezo unaweza kuta mhusika alipigwa tu bila kujijua na baada ya hapo mtu anaiweka mtandaoni na watu wengine hutumia kufurahisha wenzao huku wakisahau kwamba mhusika hakupanga kufanya hivyo.

Wapo watu wanaopenda na wasiopenda picha zao kutumika mitandaoni, hii nikishawahi kuambiwa na watu fulani, hakuna asiyelijua.

Hii sio uhalifu wa mtandao kweli kwa sababu unakuwa unaingilia uhuru wa myu mwingine?
 
Kama vipi huyo mtu asipige picha abadani.

attachment.php
 
kama hapendi si atakuambia tu, kila mtu ana njia zake za kumjali mtu, mwengine unapoweka profile photo ya picha yake ndio anahisi unamjali sana
 
kama hapendi si atakuambia tu, kila mtu ana njia zake za kumjali mtu, mwengine unapoweka profile photo ya picha yake ndio anahisi unamjali sana

Ni vizuri Kabla hujaiweka umuulize kama its okay kwa wewe kutumia picha yake jibu atakalokupa ndo litakalokupa maamuzi
 
kama hapendi si atakuambia tu, kila mtu ana njia zake za kumjali mtu, mwengine unapoweka profile photo ya picha yake ndio anahisi unamjali sana

Kwahiyo asipokuambia maana yake anapenda? Hivi ukimwambia mtu upige naye picha ili uiweke fb, badoo au insta atakuelewa kweli? Labda ni utoto tu.
 
Hili lina wahusu wanawake <Baadhi> maana wengi wanaweka picha za watu example humu jf.(sorry for this)...
 
Back
Top Bottom