Kutumia PC Mwangani au Gizani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutumia PC Mwangani au Gizani?

Discussion in 'JF Doctor' started by Boflo, Mar 17, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hamjambo wadau, Nina kawaida ya kutumia laptop usiku huku nikiwa nimezima taa, Nimewahi kusikia juu juu kuwa ukitumia computer gizani kuna madhara kwa macho, Kuna ukweli juu ya hili? Ninaomba ufahamisho kwa faida ya wote..
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa unaonaje afya ya macho yako ukilinganisha na kile kipindi cha nyuma kabla hujaanza kutumia laptop yako gizani?
  Kwa ushauri wa kitaalamu zaidi nenda kwa wataalam wa macho, watakupima na kukushauri nini cha kufanya na kipi cha kuacha.
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  SAfi sana leo Bwabwa kaja na swali la heshima kwa wote. Du! Kaokoka siku hizi au? Inapendeza sana, maana ilikuwa ninajiuliza mara mbilimbili kufungua, kwani title inaweza kuwa nzuri lakini kilichoko ndani ukashangaa ni tofauti utadhani gazeti la Alasiri ambalo kichwa na yaliyomo ndani hayafanani kabisa.

  Back to business. Bwabwa, kama unasoma kitu chochote tu hata kitabu kwenye mwanga finyu unayastrain sana macho yako kwa sababu visual acuity yake huwa mbaya, optic nerves zako zitafanyishwa kazi ya ziada kuhakikisha emage ya unachokisoma inachukuliwa kwa usahihi ili brain itafsiri na kukuwezesha upate maana halisi ya unachokisoma. Mwanga mkubwa unarahisisha image hiyo kuchukuliwa haraka na kwa wepesi, akili yako nayo itaunganisha ulichokiona ili kukupatia tafsiri ya emage hiyo bila nguvu nyingi.

  Ukilazimisha kuangalia vitu gizani ndiyo maana unajikuta unaminya macho kusharpen the focused emage, kiasi cha kujikuta unatumia calories za ziada ambazo zingetumika kwa kazi zinginezo. Huwezi kusoma kwa muda mrefu na kwa ufnisi kama unatumia kibatari ukilinganisha na mwanga wa umeme au mwanga wa jua. Ndio maana tube lights zinafaa zaidi kusomea kwa sababu ya brightness that is almost equating to natural light ambayo ndio reference point ya ideal reading light.

  Source of light pia inatakiwa isiwe karibu na macho yako. Ndio maana unashauriwa kupunguza mwanga wa screen yako kwa screen filters ili sharpness ya light rays ipunguzwe kufanana-fanana na natural intensity. Usiku ukizima taa ina maana surounding environment ni black, mwanga unakuwa focused through your pupils na kukuumiza kwa kuwa utabaki kurekebisha lens zako wakati wote kupata emage safi. Ukiwasha taa zingine una-neutralize mwanga wa laptop na ule mwingine, na kujiongezea usalama zaidi wa macho yako. wanaozima taa kuona kideo ni kwa sababu kwanza screen ni kubwa na emage unazoziona ni kubwa vilevile. halafu unakaa zaidi ya metre tatu.

  Hayo ni maelezo ya kawaida bila kuingia more kwenye scientific reasoning ambako pengine itakuchanganya tu.
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana Lekanjobe kwa maelezo yako murua na mwanana, Ubarikiwe sana kwa faida kubwa sana uliyotupa
   
 5. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli umeuliza swali la msingi sana....na nimependa sana majibu Lekanjobe
   
Loading...