Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,107
Imekuwepo tabia katika nchi hii hivi karibuni, serikali au viongozi wakitaka kuungwa mkono na umma katika mambo kadha wa kadha wanakimbilia kwenye dini.
Tabia hii ya ajabu kwa kiasi kikubwa ilianzishwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda smbaye kila alipokuwa akipata msukosuko wa kisiasa, akitakiwa atoe majibu ya tuhuma zinazomkabili kama vile Vyeti feki, au kuvamia Studio za redio alikuwa immediately anakimbilia makanisani, kanisa moja baada ya jingine, amewahi kwenda pia kwenye hadhara ya masheikh ili wamuombee. Sasa kuombea mtu siyo tatizo, lakini hilo suala linapotumika mara kwa mara kiasi cha kuonyesha kuwa huyu mtu anatumia mgongo wa dini ili kufikia malengo ya kisiasa ni tatizo kubwa sana hilo.
Tabia hii ya Makonda bahati mbaya ilirithiwa na Rais Magufuli ambaye naye siku za Karibuni amekuwa akijiweka mbele kwenye mambo ya dini kiasi cha kuonyesha kuwa sasa naye anachanganya dini na siasa, kitu ambacho ni hatari sana kwa umoja na mshikamano na uneutral wa kiserikali pindi ikitakiwa kuwa neutral
Siku hizi Raisi Magufuli hata akienda kwenye Ibada binafsi za jumapili Taifa zima linapewa press release kuwa Magufuli leo kasali wapi na saa ngapi, Sisi kama Taifa kusali kwa Magufuli misa ya saa fulani. katika kanisa fulani inatuhusu nini? -—Mwalimu Nyerere alikuwa akisali kila siku misa za asubuhi na jumapili mbona hatukuwahi. kuona mambo hayo?
Lakini ukiachilia mbali hilo, siku za karibuni rais Magufuli amekuwa akitoa miongozo ya kisera ya serikali makanisani, mfano ni kipindi kile cha korona alipokuwa akitoa misimamo ya serikali juu ya hatua anazofanya au anakusudia kufanya mintaarafu ya suala hilo.
Sasa ukichunguza kwa makini utaona kuwa kuna siasa nyingi ndani ya matendo haya, ni utaratibu wenye lengo la kuifanya jamii ya watanzania ambayo asilimia kubwa ni waamini Mungu waseme "aah, ona kumbe tuna raisi mcha Mungu, aah tuna mkuu wa mkoa mcha Mungu" n. k
Sasa cha kusikitisha zaidi ni kuwa Jina tukufu la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema limekuwa likitumika kwa ajili ya manufaa binafsi ya kisiasa ya baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa dini ambao kwa hulka na matendo yao jamii inawajua kuwa ni watu wasanii, hawana usafi wowote wa kimaadili na kimatendo.
Just imagine, Hawa viongozi wanaitisha makongamano repeatedly ndani ya muda mfupi usiozidi siku 10 kuilink serikali na dini.
Hebu cheki hii:
Tarehe 15 TAG wanaitisha kongamano kumpa zawadi Magufuli alivyopambana na Korona
Tarehe 17 Viongozi wa dini wanaitisha kongamano la kusifu utendaji wa serikali wa miaka 5
Tarehe 24 Viongozi wa dini wanaitisha kongamano eti la kuombea uchaguzi litakalohudhuriwa na viongozi kedekede wa serikali wakiongozwa na Magufuli
Waislamu wana kitu kinachoitwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Maana ya hili jambo siyo tu kwenda kwa waganga na wachawi, bali inamaanisha kulitumia Jina la Mwenyezi Mungu na Utukufu wake kwa mambo binafsi ambayo si ya Kimungu huku ukijifanya kuwa yana baraka za Mungu kumbe kuna uwongo, ulaghai na hila ndani yake.
Tunayo sababu za kuamini kuwa viongozi hawa wa kidini wanasukumwa na masilahi yao binafsi na wala hawana dhati ya Kimungu kwa sababu tunafahamu kuwa baadhi yao wameanza kupata teuzi na wengine wameanza kupitishwa na vysma vya siasa kugombea nyadhifa za kisiasa.
Nawatahadharisha Wanasiasa na viongozi wa Dini wenye kutumia Jina La Mwenyezi Mungu kisiasa na ndivyosivyo, kuwa Mwenyezi Mungu anawaona, Hadhihakiwi, na ana uwezo wa kuwachapa kiboko wasijue kimetoka wapi!
Mwalimu alitahadharisha sana kuhusu suala la mtawala na ishu za dini, alisema hivi si vizuri mtawala kujiweka mbali na mambo ya dini lakini si vizuri mtawala kuegemea huko!
Tusimtanie Mungu, Kiboko chake ni kikali!