Kutumia ict kutatua matatizo halisi ya jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutumia ict kutatua matatizo halisi ya jamii

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Apr 8, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi tukiongelea vikwazo kwenye sekta ya ICT serikali imeonekana ni kikwazo katika mambo mengi.

  Wakati nakubaliana kuna mambo serikali inatakiwa kuyaweka sawa bado kuna wataalam wengi kwa nafasi taasisi , majukumu au uwezo wa maamuzi waliyonayo wanaweza kyafanya na kuifanya ICT kuyoa mchango.

  Nitatoela mfano taasisi au maaumizi mabali mabli ambayo hayahitaji gharama kubwa na yana mchango wa kuleta mabadilliko endelevu.

  I Elimu

  Hili Nimeliandika sana hapa. Kuna shule hazina maabara,kama maabara ziipo basi hazina vifaaa . kuna shule hazina waalimu wa sayansi . ICT ina toa fursa za kufukia mapungufu haya
  How?
  Ni kiasi cha wizira au Idara, NGO au Mbunge au hata shule binafsi au hata mtu binafsi anayejihusiha na elimu kutafuta mwalimu mzuri wa somo fulani na watalmu wa kurekodi video, Kurekodi video akifunidisha au akifanya practical ya somo fulani. Then kutoa kuuza copi ya DVD kwa shule na wanafunzi. Shule zitahitajika kununa TV na DVD player kwa ajili hii. Naamini shule nyingi zinavyo hivi vifaa . One time cost inafanya kazi kwa miaka kadhaa. Wanafuzi na wazazi wanatkiwa kujua video sio lazima iwe ya kanumba . Waleweshwe unaweza kutazama video ya Laws of motion of balancing chemical equation.
  Faida zake nini
  • Tatizo la maabara litakuwa limekiwisha na hakuna ulazima shule kuwa na maabarabadla yake wanaweza kuwa video room ya wanafuzi kuona kila practical inafanyikaje. kama shule haina mwalim au zile topic ngumu practical. One time cost. na hivyo ufanisi na matoek ya mwnaafunzi kuboreka.

  • kwa mwanafuzi itasaidia akiwa nyumbani anaweza kuona zaidi ya video ya anumba. anaweza kuona video ya lawas of motion.zaidi kuelew kama hakuelewa mwalimu darsani. mwnafuzi kuuliza maswali na kuongeza ubora wa elimu.
  Wito
  Tuwaombe wabunge tunaowajua na tuwashawishi watumie japo kias fulani cha pesa za mfuko wa jimbo kufanya kitu hiki. Mbunge atakeyajribu kufanya hivi ataona serikali inaiga siku si nyingi. Binafis najua hili linawezekana lakini sina uwezo wa kuorangise resources, na sina access ya kuwapa idea hii wale wenye uwezo wa kufanya maamuzi. So tusaidiane.

  Nawaombeni muwaambie waheshimiwa vijana wenzetu kina myika, zitto,january makamba, etc. Na hata kina Mbowe , Dr slaa prof lipumba mawaziri na maktibu wa jk waje wasome uzi huu kama wataona yanafaa wayafanyie kazi .. kama watataka maelezo zaidi tutawafamisha na kueleza option zilizopo kwa upana zaidi


  NB.
  Nitaendela kutaja opportunities za iCT zinazoweza kufanyika kwenye sekta au tasisi mbali mbali. kutatua matatizo .
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Idea nzuri sana hii,lakini atleast ungepatikana mkoa wa kujaribishia pale watakapo ridhia kufanya hivi na sio kuanza tu ghafla kwa nchi nzima,wanaweza kuanzia kwa mkoa kama mbeya hivi,then kama ulivosema,wanafunzi wana kua wanaangalia practical kwanza,...baadae wanaenda kufanya,...sio hivo tu,ziwepo na session za maswali kwamba kama mwanafunzi hakuelewa wakati anaangalia au kufanya practical basi anaandika kile ambacho hakukielewa na atauliza kwenye session ya maswali!

  zaidi ya yote,vitu visio vinakaa sana kwenye akili,hii nahisi itapunguza nguvu kubwa wanayo tumia wanafunzi kwenye kujifunza!
  Tatizo ni je,...Kuna kiongozi yeyote tanzania mwenye mtazamo wa kwenda mbele ya hapa tulipo au tulipofikia kwa wanafunzi 80% kufeli ndio mission ya serikali?

  Jibu ni gumu mno,na tunaweza kuishia kubaki na idea kama hizi ila hazina implementation,serikali haijawekeza,haitaki kuwekeza na haitawekeza kamwe kwenye sayansi na teknolojia vitu ambavyo ni chachu kubwa kwa maendeleo ya nchi yoyote ile!

  Tuombe Mungu mawazo yao yabadilike,itakuwa lini hiyo?
   
 3. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii idea ni nzuri sana, lakini tukumbuke kuwa elimu ni biashara na/au siasa. Kufeli wanafunzi na % kubwa kama tulivyoshuhudia mwaka jana ingekuwa changamoto kubwa kutafuta suluhisho la hili janga, lakini, naona ishu za uongozi zipo kwingine kabisa. Loliondo ndio usukani katika ishu zinazojadiliwa na wenzetu.
  Solution hapa ni moja tu. Wazazi na wanafunzi wenyewe wanajua umuhimu wa elimu, basi, solution kama hizi ziwalenge hawa watumiaji na sio kusubiri uongozi utimize hii ishu. Mtazamaji, nadhani tumeshabadilishana mawazo katika hili, nakupongeza sana kwa kukumbushia jamii kuwa solutions zipo na zinawezekana.
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  binafsi naipenda sana kompyuta lkn cjui nianzie wapi mpaka na mimi niweze kudesign web kwa program ya php na nyingine nyingi kama kungekuwa na dvd ya program mbalimbali php,java,asp n.k ningenunua na mie nikawa mjuzi
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ndio ttizo sababu wenye idea wanaweza kuwa hawana resources na wenye resouces may be wana priority na mitazamo tofauti ya kutatua mambo.

  Lakini tuna wabunge wengi tunawasifia vijana. Tunajua wabunge wana pesa kwa mfuo wa wa maendelo wa jimbo. ambao serikali haina say. So ni opportinity kwa mbunbe yeyote kujaribu hii hasa wale wa mijini.
  Ni aibu mapaka sasa watoto wa shule tena hata za mijini anasoma practical ya chemistry kwa notice kwa kisingizo cha hakuna maabara au vifaa. kama ulivyosema hata visual labaratory ya kuona video ya practical inaweza kuleta mabadiliko.

  Binafsi sioni ugumu kama kuna mbunge mwenye nia. Akatafuta mwalimu mzuri wa somo fulani. Akatafuta kampuni nzuri ya kurekodi akaomba UDSM wawape chance ya kurekodi kutumia reouces zao. Mwalimu akashootiwa akifundsha au akionyesha practical fulani. may be za masomo ya chemistry Then CD zikiwepo msukumo unakuja kwa wazazi na wanfuzi kuwa. Ni mwezi mmoja tu unaweza uwa umetayarisha full DVD ya somo fulani kwa wanafunzi wa kidato fulani

  Hata watu binafsi kama mama rwakatare au wenye shule binafsi wanaweza kuambiwa hili na kulifnyia kazi.

  Ingawa sitaki kuongelea siasa siku si nyingi JK kasema watatumia Mkonga kufundisha. Ni kama vile bila kuwepo mkonga basi hakuna solution za iCT ambazo zinaweza kutumika kutatua tatizo la uhaba wa walimu na vifaa. This is wrong nadhani inabidi wenye idea tuwaambie decison makers na wanasiasa waht ICT is capable of doing. Ni wachache wanaelewa sana.

  Hata shule isiyokuwa na mabaara wakipewa TV, wakapewa DV player na DVD za masomo tayari wanakuwa na.lab.

  Tukiacha hata yakutayarisha inayoweza kuchukua miezi michache. Kuna taasisi kama BBC . zina documentary nyingi za kufundisha mamboya science , na geography . lakini si wanafuzi wengi na wazazi wanajua umhuhimu wa documentary hizi. Wabunge au decison makers wangapi wanshindwa kuongea na BBC kuomba haki ya kuzitumia hizi documentary katika training ya mashule. je Wamejaribu wameshindwa. au wamekataliwa.

  Wanafuzi wanajifunza kwenye geography rain forest au desert. wakiona documentary ya life in the rain forest au desert baada ya kufundishwa itawasaidia sanaaaaaa. Hizi documentary nyingine zimerekodiwa nchini kwetu yet haziko accesible na wanafunzi wengi. ni aibu.

  Pia kuna video ziko available online kama Khan Academy. Sio wanafunzi wengi wana access na internet tanzania . Kinachweza kuanyika ni wahusika kama wabunge kuafuta wataalam kuzirekodi video za masomo muhimu au yale magumu na kuziweka kwenye DVD au CD na kuziuza kwa wanafunzi.

  Inasikitisha kuona bado mwanafunzi anafundishwa kama tulivyofundishwa miaka ya nyuma wakati kuna pportunities kibao za ICT za kufukia mashimo.

  May be niulize what sould we do As JF members wa technology? Tuchukue video chache kwenye hiyo website ya khan tuweke kwenye DVD tukagawe kwa shule kama tambaza jangwani.
   
 6. D

  Developer JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 285
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Mkuu mtazamaji, mawazo yako ni mazuri sana, hongera kwa hilo. Watanzania tuna tatizo moja kubwa mno, uthubutu. Tunabaki tu kulalamikia decision makers. Yes wana mchango mkubwa sana katika kutatua matatizo ya jamii, kutuletea maendeleo. Lakini sisi pia twatakiwa tujifunze ku take chances, kupambana katika wakati mgumu, kwa ajili ya maendeleo yetu. Sisi sote tunajua jinsi ndugu zetu wakenya walivyo tushinda katika hili: wana nguvu kubwa sana ya uthubutu na ushindani ukikompare na sisi. Story nyingi za watu waliofanikiwa sana duniani ni uthubutu na kujiamini. Watu wengi wanakuwa na idea/mawazo mazuri sana ila yanakufa kwa sababu ya pesa: ili maisha yaende sawa vinahitajika vitu vitatu: wazo, pesa, watu. Watu wengi wanakuwa na cha kwanza lakini wanaogopa kupush/press on wakisubiri vyote vitatu vikamilike. Infact unawaza kupress hard wazo lako na on the way desion makers wakakusaapoti. Ni juzi katika pitapita yangu katika majukwaa ya JF nimeona UN wanatoa up to $25000 kwa NGO zinazodili na maswala kama haya. Sasa mkuu unahitajika kuthubutu kutafuta media/njia ya ku implementia mawazo yako na itakuwa nzuri zaidi ukijikusanya watu wenye interest moja and then you push forward to start your own organization. Ngoja nimkoti jamaa mmoja aliwahi kusema "Worriers take chances. Like any other they fear failing, but they refuse lo lert fear control them" be a worrier brother and move on.
   
 7. mdeesingano

  mdeesingano Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nashauri tuiache serikali na wabunge pembeni kwanza, sisi kama sisi wanaICT tufanye jambo hili... Tusisubiri wabunge kwani kwao wao ukiwaeleza hilo yaweza kuwa kama ndoto labda washuhudie ikiwa imekamilika ndipo wataweza nao kufanya hivyo...

  Tatizo ninaloliona kwa sisi wanaICT ni kua, we don't know or we don't want to join our forces and advertise ourselves... We don't sacrifice money and time for the sake of advertising the good things ICT can do... We are always looking for the return we will get for doing something good in ICT.

  Bado tunatakiwa tuhangaike kuwafanya watanzania wasio na ujuaji kuhusu ICT wajue kua ICT is very powerful and can do lots of interesting and development things... Na kuwajuza wananchi hili ni kwa njia moja to ya SOLVING REAL WORLD PROBLEMS FACING TANZANIANS kwa kutumia ICT na hapa kwa sasa tusiweke masilahi mbele mpaka field yetu ikomae jina kwanza...
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MkuuUko sahii kwa yale liyoeleza tatizo linakuja nafasi ,nyezo au wenye nia walipo. Unaweza kuwa na

  • idea nzuri lakini ukawa porini au huna coneection na mwalimu au wahusika wa kumu itroduce hii issue.
  • Inawezekana kuna watu wana nyezo wana access na walimu shule labda pia hawajui jinsi ICT can turn things?
  • Piak kuna wana ICT wapo au tupo kwenye maofisi tuna degree tunajua na tuna idea nzuri lakini hawajawai kuwashauri decison makers.
  Ndio maana sometime tunaishia kuandika tu. But kama ulivyosema tunaweza kushirikiana kwa nafasi tulizonazo tuone tunaweza kufanya nini kwa majaribio.Mfano tukichukua video za topic fulani za phycisau hesabu tukatengeneza wenye CD kama 20. then tukagwa kwa shule na wanafuzi fulani wachache tutayochagua.

  Nikiangalia video ya algebra, Linear equation mfano nasema ningepata nyenzo kama hizi enzi nasoma may be nisingepata D ya hesabu form four. teh teh teh teh.

  Ingawa video na CD zilizopo mtandaoni sasa sio za walimu wa tanzania but Tukiwachokoza kwa hizi video itachochea sasa zitengenzwe za watanzania. nadhani CD ya video ya mwalimu wa kimarekani anayelezea WORK, ENEGY au PROBALILITY ataeleweka tu hata kwa watanzania.

  mfano nini tunahitaji kuweka video kama hii kwenye CD. ili ipiatikane kwa wanafuzi wengi.


  Ningekuwa siko porini hili ningelifanya hili. kama una mtu anaweza bado nashuri ajribu bila kusubiri wanasiasa.

  kama kuna mtu anhitaji ushauri jinsi ya kuconvert hizo video katika format iinayowez kuchekezeka kwenye DVD au CD player basi tutabadilishana ujuzi. Hii kitu tujitoleee wana ICT kama mlivyosema. Sababu niko porini Zaidi ya kuchagia Idea naweza kuchangia Gharama ya CD au DVD chache zitazogawiwa bure kwenye shule itayochaguliwa.

  Kwa wale wana ICT wenye ndugu wanaosoma watengenezeeni CD au DVD mziburn na muwape zawadi. Taratibu tutafika. wanafunzi wengi wa tanzania hawana acess a internet lakini wanafuzi wengi wana acess na TV na majumbani hasa mijini kuna DVD player.

  Kama ulivyosema lets make this as a service.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtazamaji,

  Tunaweza?

  Educator.com - #1 Trusted e-Learning Service Site - Start Today

  Iwe na http://tanzania.educator.com

  Hii ni commercial venture na service zipo mtandaoni peke yake. Lakini idea for Tanzania bado itabidi offline ndio iwe main driver ndio mwanafunzi aweze kutumia PC (bila internet) au DVD equipment na TV.
  Muhimu tukumbuke kuwa kuna costs nyingi katika kutayarisha syllabus materials zozote ziwe full nondo katika kumuelimisha mwanafunzi. Jinsi ya ku'offset hiyo cost ni kufanya huu mradi in a commercial way, hata kama ni biashara isiyolenga kupata faida. La sivyo, itakuwa ni vigumu sana kuweza kuifanikisha bila ya kuwa na mfadhili.

  Kama wewe Mtazamaji, mimi najiuliza, je,kama ningepata hizi CD's za hesabu nk, kweli labda foundation yangu kielimu ingenipeleka kwingine kabisa.
   
Loading...