"Kutumbua Majipu" na "Hapa Kazi Tu" Zinakosa Dira

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Usipokuwa na dira, kwa maana ya Katiba mpya, Sheria mpya, kanuni mpya na taratibu mpya, unakosa dira juu ya uelekeo sahihi, na kinachobaki ni kufanya maamuzi kwa kufuata mkumbo na umaarufu wa kisiasa kwenye luninga.

Yanayofanyika sasa katika serikali ya awamu ya tano Tanzania, kwa maana ya "kutumbua majipu" na "Hapa Kazi Tu" ni mambo mema, lakini yasipowekwa kisheria (kama ilivyoainishwa hapo juu) yatabaki kuwa maamuzi na utashi binafsi, yanayotegemea mawazo na fikra za mtu mmoja ambaye kesho haijulikani ataamua nini.

NI MATUMAINI YANGU KUWA MH. RAIS MAGUFULI ATAISOMA THREAD HII NA ATAZINGATIA UANZISHWAJI WA KATIBA MPYA PAMOJA NA SHERIA KANUNI NA TARATIBU MPYA ZA KIUTENDAJI ZENYE KURUDISHA MAMLAKA KWA WANANCHI AMBAPO HAYO ANAYOYAWAZA NA KUYAKUSUDIA KUYAFANYA YATAKUWA NDANI YAKE.
 
Tajirijasiri, naona kwamba, maelezo yako sio sahihi na yanapotosha wasomaji wa JF wasiojua maana ya dira. Unachokiongelea sio dira, kwani, unaweza kuwa na vyote hivyo ulivyovitaja lakini isiwemo dira yoyote. Napendekeza tuelimishane kidogo:

Fikiria uko Dar unataka kwenda Kigoma kwa usafiri wa nchi kavu. Hii ni safari ya kilometa zipatazo 1368 kabla ya kukutana na kibao kilichoandikwa-Kigoma Bus Stand. Katika hatua ya kwanza ni lazima kutambua vipande vya barabara vinavyoweza kuunganishwa kwa magari, au pikipiki, au baiskeli, au mchanganyiko wa vyombo hivi, lakini hatimaye ukafika Kigoma.

Kwa ajili ya kivitambua vituo hivi lazima kufanya safari ya kimawazo ukianzia Kigoma (mwisho wa safari ambao tuuite dira) kuelekea Dar (mwanzo wa safari). Kwa mfano mnyororo ufuatao wa vituo ni route mojawapo inayoweza kutufikisha Kigoma: Kigoma--Tabora--Dodoma-Mlandizi-Dar.

Katika hatua hii, kilichofanyika kinaitwa ORDER OF PLANNING.Na mpaka hapo tumejibu maswali manne muhimu: Tunataka kwenda wapi? (Kigoma); Tuko wapi? (Dar); Tunawezaje kutoka tuliko nakufika tunakotaka kwenda? (Kwa kusafiri kupitia vitua vilivyoorodheshwa); na tutajuaje kwamba tumefika Kigoma? (kibao kilichoandikwa-Kigoma Bus Stand).

Katika hatua ya pili, utekelezaji wa mpango unaanza. Tunaanza safari kutoka Dar, kituo hadi kituo kuelekea Kigoma. Tutafika Kigoma baadaya kuvitembelea vituo vifuatavyo, hatua kwa hatua: Dar-Mlandizi-Dodoma-Tabora-Kigoma. Utekelezaji wa safari hatua kwa hatua namna hii tunauita ORDER OF EXECUTION.

Kuna tofauti kubwa moja katiya order of planning na order of execution. Hebu angalia haya mawili:

ORDER OF PLANNING: Kigoma--Tabora--Dodoma-Mlandizi-Dar.
ORDER OF EXECUTION: Dar-Mlandizi-Dodoma-Tabora-Kigoma.

Unagundua nini? Ni hiki: unachoanza nacho wakati wakupanga, ndicho unamaliza nacho wakati wa utekelezaji.

Kwa hiyo, ukisema "HapaKazi Tu" ya magafuli haiambatani na DIRA unajaribu kusema kwamba, Magufuli anaanza utekelezaji kabla ya kupanga. Kwamba anakuwa kama dereva anayeendesha gari bila kujua anakwenda wapi. Hilo ndilo unamaanisha? Sidhani.

Kwa hiyo, inawezekana unalo wazolakini hujalieleza sawasawa. Magufuli anayo dira, ila wewe hujaielewa, au unaielewa lakini huikubali kwa sababu maalum. Ukisoma mpango wa maendeleo wowote unakuwa na dira ambayo itakuwa ni sehemu ya mwisho ya mnyororo ufuatao:

Kiingereza: INPUTS->ACTIVITIES->OUTPUTS->OUTCOMES->IMPACT.
Kiswahili: RASILIMALI->KAZI->MATOKEO->MAJALIWA->DIRA

Huu ni mnyororo wa thamani (value chain) unaoanzia tulipo kuelekea tunakotaka kwenda. Hii ni nadharia ya mabadiliko (theory of change au roadmap). Usomaji wa mnyororo huu kutoka kushoto ni kama ifuatavyo:

IKIWA rasilimali "V" zitapatikana, BASI kazi "W" zitafanyika; IKIWA kazi "W" zitafanyika, BASI matokeo "X" yatapatikana; IKIWA matokeo "X" yatapatikana, BASI majaliwa "Y" yatakuja; na IKIWA majaliwa "Y" yatakuja, BASI dira "Z" itakuwa imefikiwa. Utaona kwamba huu ni mnyororo wa sentensi kadhaa zinazohusisha maneno "IKIWA hivi/BASI vile." Hivyo, ndivyo dira iliyo katika maandiko au maneno ya mtu inavyobainishwa.

Tukitumia misamiati ya IKIWA/BASI kwenye mfano wetu wa Dar-Kigoma, tunapata sentensi zifuatazo:

Ikiwa nauli itapatikana, basi tutapanda gari la Dar-Mlandizi na hatimaye kufika Mlandizi; ikiwa tutafika Mlandizi, basi tutapanda gari la Mlandizi-Dodoma na hatimaye kufika Dodoma; ikiwa tutafika Dodoma, basi tutapanda gari la Dodoma-Tabora na hatimaye kufika Tabora; na ikiwa tutafika Tabora, basi tutapanda gari la Tabora-Kigoma na hatimaye kufika Kigoma.

Kwa Kiingereza, maneno 'inputs,' 'activities,' 'outputs,' 'outcomes' na 'impact,' yanazo fasili zifuatazo:

(a) Inputs: all the resources that contribute to the production and delivery of outputs. Inputs are "what we use to do the work". They include finances, personnel, equipment and buildings.

(b) Activities: the processes or actions that use a range of inputs to produce the desired outputs and ultimately outcomes. In essence, activities describe "what we do".

(c) Outputs: the final products, or goods and services produced for delivery. Outputs may be defined as "what we produce or deliver".

(d) Outcomes: the medium-term results for specific beneficiaries that are the consequence of achieving specific outputs. Outcomes relate clearly to an institution's strategic goals and objectives set out in its plans. Outcomes are "what we wish to achieve".

(e) Impacts: the results of achieving specific outcomes, such as reducing poverty and creating jobs

Je, tukijaribu kuchambua kauli na mipango inayotekelezwa na Magufuli kwa kutumia nyenzo hizi za kifikra hatuoni mnyororo wa thamani wa aina hii? Kama mnyororo unaonyeshwa, basi anayo dira. Kama hauonyeshwi, basi Magufuli hana dira. No reserach no right to speak! Tutafakari pamoja.
 
Wanafanya maamuzi bana tukikorofishana tu wanaita vyombo vya habari alafu unaitwa jipu,ukitaka kumzibua pembeni kuna polisi inabidi ubaki mnyonge
 
Kwani anayofanya Magufuli si tumeambiwa yapo kwenye Ilani yao? Wakati wa kampeni si alikuwa anazungumzia haya yanayofanyika sasa kasoro uchelewaji wa mahakama ya mafisadi? Angewezaji kutuaminisha hadi tumpe kura zetu kama hakuwa na Dira? Inamaana na sisi tuliomchagua tulikosa Dira pia!
 
jamani mbona kuna wizara haziguswi kwani watendaji wake walikua ni malaika au zenyewe ni special sana kwa mfano wizara ya fedha maliasili na utalii wizara ya UJENZI na zingine
 
Tajirijasiri, naona kwamba, maelezo yako sio sahihi na yanapotosha wasomaji wa JF wasiojua maana ya dira. Unachokiongelea sio dira, kwani, unaweza kuwa na vyote hivyo ulivyovitaja lakini isiwemo dira yoyote. Napendekeza tuelimishane kidogo:

Fikiria uko Dar unataka kwenda Kigoma kwa usafiri wa nchi kavu. Hii ni safari ya kilometa zipatazo 1368 kabla ya kukutana na kibao kilichoandikwa-Kigoma Bus Stand. Katika hatua ya kwanza ni lazima kutambua vipande vya barabara vinavyoweza kuunganishwa kwa magari, au pikipiki, au baiskeli, au mchanganyiko wa vyombo hivi, lakini hatimaye ukafika Kigoma.

Kwa ajili ya kivitambua vituo hivi lazima kufanya safari ya kimawazo ukianzia Kigoma (mwisho wa safari ambao tuuite dira) kuelekea Dar (mwanzo wa safari). Kwa mfano mnyororo ufuatao wa vituo ni route mojawapo inayoweza kutufikisha Kigoma: Kigoma--Tabora--Dodoma-Mlandizi-Dar.

Katika hatua hii, kilichofanyika kinaitwa ORDER OF PLANNING.Na mpaka hapo tumejibu maswali manne muhimu: Tunataka kwenda wapi? (Kigoma); Tuko wapi? (Dar); Tunawezaje kutoka tuliko nakufika tunakotaka kwenda? (Kwa kusafiri kupitia vitua vilivyoorodheshwa); na tutajuaje kwamba tumefika Kigoma? (kibao kilichoandikwa-Kigoma Bus Stand).

Katika hatua ya pili, utekelezaji wa mpango unaanza. Tunaanza safari kutoka Dar, kituo hadi kituo kuelekea Kigoma. Tutafika Kigoma baadaya kuvitembelea vituo vifuatavyo, hatua kwa hatua: Dar-Mlandizi-Dodoma-Tabora-Kigoma. Utekelezaji wa safari hatua kwa hatua namna hii tunauita ORDER OF EXECUTION.

Kuna tofauti kubwa moja katiya order of planning na order of execution. Hebu angalia haya mawili:

ORDER OF PLANNING: Kigoma--Tabora--Dodoma-Mlandizi-Dar.
ORDER OF EXECUTION: Dar-Mlandizi-Dodoma-Tabora-Kigoma.

Unagundua nini? Ni hiki: unachoanza nacho wakati wakupanga, ndicho unamaliza nacho wakati wa utekelezaji.

Kwa hiyo, ukisema "HapaKazi Tu" ya magafuli haiambatani na DIRA unajaribu kusema kwamba, Magufuli anaanza utekelezaji kabla ya kupanga. Kwamba anakuwa kama dereva anayeendesha gari bila kujua anakwenda wapi. Hilo ndilo unamaanisha? Sidhani.

Kwa hiyo, inawezekana unalo wazolakini hujalieleza sawasawa. Magufuli anayo dira, ila wewe hujaielewa, au unaielewa lakini huikubali kwa sababu maalum. Ukisoma mpango wa maendeleo wowote unakuwa na dira ambayo itakuwa ni sehemu ya mwisho ya mnyororo ufuatao:

Kiingereza: INPUTS->ACTIVITIES->OUTPUTS->OUTCOMES->IMPACT.
Kiswahili: RASILIMALI->KAZI->MATOKEO->MAJALIWA->DIRA

Huu ni mnyororo wa thamani (value chain) unaoanzia tulipo kuelekea tunakotaka kwenda. Kwa Kiingereza, tunazo fasilizifuatazo za maneno hayo hapo juu:

(a) Inputs: all the resources that contribute to the production and delivery of outputs. Inputs are "what we use to do the work". They include finances, personnel, equipment and buildings.

(b) Activities: the processes or actions that use a range of inputs to produce the desired outputs and ultimately outcomes. In essence, activities describe "what we do".

(c) Outputs: the final products, or goods and services produced for delivery. Outputs may be defined as "what we produce or deliver".

(d) Outcomes: the medium-term results for specific beneficiaries that are the consequence of achieving specific outputs. Outcomes relate clearly to an institution's strategic goals and objectives set out in its plans. Outcomes are "what we wish to achieve".

(e) Impacts: the results of achieving specific outcomes, such as reducing poverty and creating jobs

Je, mipango inayotekelezwa na Magufuli haionyeshi mnyororo wa thamani wa aina hii? Kama mnyororo unaonyeshwa, basi anayo dira. Kama hauonyeshwi, basi Magufuli hana dira. No reserach no right to speak! Tutafakari pamoja.
Narudia tena, Katiba Mpya. Sheria Mpya. Kanuni Mpya. Taratibu mpya. Aziangalie ili hayo anayoyataka kwa nchi hii ambayo ni mema yaweze kufanikiwa.
 
Hujajibu concern yangu. Jifunze kuendesha mabishano ya hoja ili jukwaa hili liwe na faida kwa wasomaji wake
 
Umeeleweka sana mkuu. Wala sikubishii. Katiba mpya, sheria mpya, kanuni mpya na taratibu mpya pamoja na hayo uliyafafanua, yatajenga Tanzania Mpya.
 
Learn to accept challenges, learn to accommodate what comes different from what you believe.
Arguments are not supposed to be premised on mere beliefs, but justified true beliefs. And that the reason for debating issues. Surrender into mere dogmas is a sin.
 
Believe what u believe coz u r right. But what provokes the ego is what stands longer. Don't take it personal.
 
Usipokuwa na dira, kwa maana ya Katiba mpya, Sheria mpya, kanuni mpya na taratibu mpya, unakosa dira juu ya uelekeo sahihi, na kinachobaki ni kufanya maamuzi kwa kufuata mkumbo na umaarufu wa kisiasa kwenye luninga.

Yanayofanyika sasa katika serikali ya awamu ya tano Tanzania, kwa maana ya "kutumbua majipu" na "Hapa Kazi Tu" ni mambo mema, lakini yasipowekwa kisheria (kama ilivyoainishwa hapo juu) yatabaki kuwa maamuzi na utashi binafsi, yanayotegemea mawazo na fikra za mtu mmoja ambaye kesho haijulikani ataamua nini.

NI MATUMAINI YANGU KUWA MH. RAIS MAGUFULI ATAISOMA THREAD HII NA ATAZINGATIA UANZISHWAJI WA KATIBA MPYA PAMOJA NA SHERIA KANUNI NA TARATIBU MPYA ZA KIUTENDAJI ZENYE KURUDISHA MAMLAKA KWA WANANCHI AMBAPO HAYO ANAYOYAWAZA NA KUYAKUSUDIA KUYAFANYA YATAKUWA NDANI YAKE.

Ulikuwa na idea njema lakini topic uliyochagua kubandika hapa inakuzidi scope! Huwezi kumshawishi mtu makini kwamba yule Chuwa wa WMA aliyefunga flow meters kwa miaka 5 badala ya kuzirekebisha au kuagiza mpya model tofauti; au mkurugenzi wa halmashauri aliyewaonga wakaguzi wa CAG wagushi hati wampe hati safi badala ya hati chafu anayostahili au watu walioruhusu makontena yachukuliwe bila kulipa ushuru nk; kwamba wanahitaji katiba mpya ili wachukuliwe hatua!! Hii topic huiwezi kajipange upya!
 
Nimekusoma sana mkuu, hata uuzaji wa nyumba za serikali, meli chakavu ya 1970+ kwa bilioni 8, na ripoti ya CAG juu ya Wizara ya Ujenzi nalo liangaliwe upya kwenye uongozi huu wa Magufuli.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Back
Top Bottom