ona mimi nilichokifanya
Sikumoja nilikosea nikatuma Tsh.250,000 kwa *wrong number*, baada ya kuona hilo, niliamua kujaribu kutuma sms ya kutisha alieipokea hela hiyo...
Text hiyo niliiandika hivi,
_*Habari yako rafiki, naitwa Otiko, ni balozi wa kanisa jipya la Shetani hapa Tanzania. Ni tumaini langu umeiona posho yetu uanachama ya Tsh.250,000 tumekutumia TIGOPESA ili kujiunga na kanisa letu la Shetani. Huo ni mwanzo tu wa mambo mazuri yanakuja. Usiku wa leo tuna mkutano ambapo tutachinja watu watatu kwa ajili ya kafara. Tumekubaliana kufanya kafara hii katika viwanja vya nyumbani kwako mida ya saa nane za usiku na unatakiwa uchague mmoja wa watu unawapenda ili tunywe damu yake pia. Lakini kama hungependa kujiunga katika kanisa letu hili la Shetani, rudisha hiyo pesa kwa namba yangu hii hii"*

_
Baada kama ya dk 10, nikapokea sms inasema, _*"Oyoo bro, kama vp tuma Tsh.250,000 nyingine kuna mshikaji wangu nae kavutiwa na kanisa lenu"

*_
Kidogo nizimie

🤣
Yaani watu vyuma vimekaza kiasi kwamba wako tayari kwa lolote
Sent using
Jamii Forums mobile app