Kutubu - Ujinga Wetu ni Kaburi Letu

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,223
40,458
Tangu ilipotolewa kauli kuwa viongozi, akiwemo Rais wanatakiwa kutubu siku ya Noeli, kauli nyingi za ajabu, ambazo bila shaka zinatoka kwa Roho zisizo na Mungu zimetolewa. Nawaasa wale wanaoujua ukristo kutoangukia kwenye mtego huo wa ujinga wa neno la Mungu.

Kwa Wakristo, kutubu ni neema maana ni kwa kutubu ndipo tunapomkaribia Mungu. Huwezi kumfikia Mungu bila toba. Kama viongozi na kama Taifa tunastahili kutubu. Kuna matukio makubwa mabaya ambayo yanamchukiza Mungu yametokea:

1) Viongozi wa serikali wameshindwa kuishi na kutenda kwa kadiri ya viapo vyao. Waliapa kulinda katiba lakini wakatenda tofauti

2) Viongozi waliapa kutenda usawa, kuwatumikia watu wote kwa usawa, lakini wanatenda tofauti

3) Viongozi waliapa kuwalinda Watanzania wote na mali zao lakini wakatenda tofauti

4) Kama watu tunamjua Mungu, tunatambua kuwa Mungu hugawa karama mbalimbali lakini viongozi wanajiona ni wao tu ndio wenye akili na uwezo

5) Lakini Watanzania wengine wote, tuna wajibu wa kuuzuia uovu katika Taifa letu ikiwemo kuzuia viongozi kutenda uovu dhidi ya kundi lolote hata kama kundi hilo hulipendi. Je, tulitenda nini? Hatukutimiza wajibu wetu, tunatakiwa kutubu

6) Viongozi wa dini, kati ya majukumu yao, mojawapo ni kukemea uovu bila ya kujali unatendwa na nani. Kukemea uonevu hasa unaotendwa dhidi ya watu wasio na mamlaka. Je, nanyi mlitimiza wajibu wenu? Mnatakiwa kutubu.

7) Viongozi kwa kutumia nafasi zao vibaya, wamewafukarisha watu kutokana na chuki za kisiasa, kinyume cha utawala bora. Wanatakiwa kutubu.

Kwa wale wakristo (hata waislam naamini kutakuwa na aya za kuthibitisha umuhimu wa kutubu), biblia imeongea maeneo mengi juu ya toba (kutubu):

Warumi 2:5
Lakini unao ugumu na moyo usiotaka kutubu, na hivyo unajirundikia adhabu kwa siku ya ghadhabu wakati hukumu ya Mungu itakapodhihirishwa.

Ufunuo 2:5
Basi pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Ufunuo 3:3
Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyosikia, uyatii na kutubu. Usipoamka nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutajua saa nitakayokujia.

2 Wakorinto 7: 9
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu.

Matendo 3:19
Basi tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Matendo 11:18
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, 'Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai'.

Kuna aya nyingi katika biblia zinaongelea kutubu kama ndiyo mlango wa kumkaribia Mungu.

Nini Maana ya Kutubu
Neno tubu katika imani lina maana ya 'geuka au badilika'. Katika toba kuna mambo makuu mawili, moja ni kugeuka au kuukana uovu, na ya pili ni kugeukia njia ya kweli yaani njia ya haki. Mara 3 Ezekiel aliwaambia Wayahudi, 'Tubuni, jitengeni na miungu na matendo yenu mabaya, badilikeni, badilikeni kutoka kwenye njia zenu za uovu.

Katika agano jipya, kutubu kunaelezwa kuwa lazima kuendane na mabadiliko ya fikra, na chuki dhidi ya uovu. Mtume Marko na Matayo wanaanza kuhubiri kwa kusema, 'Tubuni', na Paulo anasema, 'mgeukieni Mungu kwa kutubu'.

Toba ni lazima iendane na kuhuzunika kuwa upo au ulikuwepo katika upungufu, upungufu wa kuyaishi maagizo ya Mungu. Wakatoliki tunaamini kuwa kutubu au toba au kitubio ni sakramenti ambayo Mungu ametupatia. Kiufupi ni zawadi.

Kama hii ndiyo maana halisi ya kutubu katika mtazamo wa imani, kwa nini Askofu Kakobe alipomtaka Rais atubu, watu wamehamaki sana? Wamehamaki kwa sababu ya ujinga, ujinga wa kutolijua neno.

Mimi binafsi, naamini Rais, viongozi wa serikali, viongozi wa dini na hata wananchi wa kawaida, tukiacha makosa ya kila mmoja katika maisha yake, kama Taifa inatubidi kutubu. Rais anahitajika kutubu kwa yale aliyoyatenda kimakosa kama kiongozi mkuu ikiwemo kutokutimiza wajibu. watendaji mbalimbali wanatakiwa kutubu. Wananchi wa kawaida wanatakiwa kutubu. Kila mmoja kwa nafasi yake.

Kama sisi ni watakatifu sana, inakuwaje katika Taifa letu:
1) Watu wanapigwa risasi hadharani, hakuna anayeweza kuzuia, kukamata wala kuzuia? Niambieni ni maandiko gani yanaruhusu haya? Kama ni uovu, lazima awepo wa kutubu.

2) Wajane maskini wanavunjiwa nyumba zao zilizojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita? Kuwafanya maskini wajane na watoto wasiishi, kuna mafundisho yoyote ya Mungu yanayoelekeza hivyo? Kama sivyo, lazima kuwepo na mtu au watu wa kutubu.

3) Watu wanakamatwa na kusweka mahabusu ovyo ovyo kama vile uwezo na uhuru wa kusema upo kwa watu wachache tu? Kuna imani inayofundisha kuwa Mungu hupenda uonevu? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

4) Watu wananunuliwa kusaliti matakwa ya waliowachagua ili waweze kuwahadaa wananchi? Kuna imani inayofundisha kuwa kumhonga mtu ni utakatifu? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

5) Polisi wanatumika kulazimisha ushindi wa CCM kwa kuwakamata wapinzani, kuwatesa, kuwateka, n.k.? Kuna utakatifu ambao unatamkwa na dini yoyote kuwa unaweza kupatikana kwa kulazimisha matakwa yao wakati kukiwa na sheria ambazo mliapa kuzisimamia, na nyinyi hamtaki? Kama hakuna, kuna watu wanatakiwa watubu.

6) Vyombo vya habari vinavyoelezea tofauti na matakwa ya watawala vinafungiwa ili viwepo vyombo vya habari vinavyosifia tu? Kuna dini inayolekeza kuwa kiongozi hata akitenda jambo baya kiasi gani hastahili kukosolewa? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

7) Watu wanafukuzwa kazi bila kufuata taratibu, na wakati mwingine kwa kuonewa au kutokana na imani zao za kisiasa?
8) Watu wanapotea, haijulikani kama wapo hai au wamekufa
9) Maiti za binadamu zinaokotwa ovyo kwenye viroba, bila ya wale wanaofanya hivyo kukamatwa au kuadhibiwa?
10) Kunakuwa na ubaguzi wa kufanya shughuli za kisiasa. CCM wanaruhusiwa kufanya mikutano, vyama vya upinzani vinazuiwa?
Na mingine mengi.

Wakatoliki tunaposali ile sala ya toba huwa tunasema ....... kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. Hivi tunafahamu kuwa kutubu kule hakuna maana yoyote mbele ya Mungu kama hakuna dhamira ya dhati ya kuacha uovu?

Kutokana na haya, kama Taifa tunastahili kutubu (kugeuka) na kuyakana haya yaliyo ya shetani. Rais anastahili kutubu, au kutokana na yeye mwenyewe kuagiza, au pengine kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhakikisha wale waliopo chini yake hawafanyi chochote kinyume cha katiba na hekima ya Mungu. Lakini shetani anafanya kazi usiku na mchana, anawatumia mawakala wake, hao ndio wanaojifanya wanampenda Rais, na kutaka akubali uovu uliopo uendelee. Hawa ni mawakala wa shetani. Rais atafakari maeneo yote ambayo ametenda sivyo, amwombe Mungu amsaidie kumjalia hekima ili azitambue na hizi roho za shetani zinazokuja mbele yake na kujifanya wanampenda kuliko hata Mungu aliyemwumba. Rais atende kadiri ya Roho ya Mungu itakavyomwongoza.

Viongozi wa dini wanatakiwa kutubu kwa kushindwa kukemea uovu kwa dhamira ya moyo, na kuwa wakweli kama alivyokuwa nabii Mika na Yesu mwenyewe ambapo kuna wakati aliwakaripia watawala wa Kiyahudi (Mafarisayo na Wanasheria) akiwaambia ole wenu mafarisayo na waandishi wa sheria kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopambwa kwa nje kumbe ndani yamejaa uchafu.

Wananchi wa kawaida tunatakiwa kutubu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wetu kama raia wema, yaani kukemea uovu kwa nguvu zetu zote bila ya kuogopa chochote maana Mungu ametupatia roho ya ujasiri ya kunena UKWELI.

Wale wanaotaka kufanya toba wasali pamoja nami kwa dhamira:

Bwana Mungu wetu, Mungu wa msamaha, nashukuru kwa msamaha wako. Nashukuru kwa kunivumilia katika uovu wangu. Kama Kiongozi wa nchi/Kiongozi wa Dini/raia wa nchi, nimekutenda dhambi wewe na ndugu zangu kwani kwa kushiriki au kwa kutotimiza wajibu wangu, nimesaidia uovu uendelee kutendeka katika Taifa lulilonijalia.

Naomba roho yako ya ujasiri juu ya Kweli yako ikae ndani yangu ili nisiogope chochote mahali popote kuunena ukweli kwa kadiri ya mapenzi yako hata kama nitapuuzwa au kuteswa. Nitakapopuuzwa au kuteswa, ukuu wako ukazidi kudhihirika zaidi na zaidi.

Naomba uipokee sala yangu, sala ya toba, sala ya kugeuka kutoka kwenye njia ya uovu kuelekea kwenye njia yako. Bwana ulisema, 'ombeni mtapewa', nami kwaajili ya ahadi yako hii, daima nasimama katika tumaini la haya nikuombayo.
 
Magu alikosea kujipa ushindi wa 100% uchaguzi wa mwenyekiti. Watu wenye akili wamegundua akiachwa afanye analotaka atatupeleka pabaya.
Anapaswa kutubu kwa Mungu wake kwamba alidanganya wana ccm na taifa.
 
Tangu ilipotolewa kauli kuwa viongozi, akiwemo Rais wanatakiwa kutubu siku ya Noeli, kauli nyingi za ajabu, ambazo bila shaka zinatoka kwa Roho zisizo na Mungu zimetolewa. Nawaasa wale wanaoujua ukristo kutoangukia kwenye mtego huo wa ujinga wa neno la Mungu.

Kwa Wakristo, kutubu ni neema maana ni kwa kutubu ndipo tunapomkaribia Mungu. Huwezi kumfikia Mungu bila toba. Kama viongozi na kama Taifa tunastahili kutubu. Kuna matukio makubwa mabaya ambayo yanamchukiza Mungu yametokea:

1) Viongozi wa serikali wameshindwa kuishi na kutenda kwa kadiri ya viapo vyao. Waliapa kulinda katiba lakini wakatenda tofauti

2) Viongozi waliapa kutenda usawa, kuwatumikia watu wote kwa usawa, lakini wanatenda tofauti

3) Viongozi waliapa kuwalinda Watanzania wote na mali zao lakini wakatenda tofauti

4) Kama watu tunamjua Mungu, tunatambua kuwa Mungu hugawa karama mbalimbali lakini viongozi wanajiona ni wao tu ndio wenye akili na uwezo

5) Lakini Watanzania wengine wote, tuna wajibu wa kuuzuia uovu katika Taifa letu ikiwemo kuzuia viongozi kutenda uovu dhidi ya kundi lolote hata kama kundi hilo hulipendi. Je, tulitenda nini? Hatukutimiza wajibu wetu, tunatakiwa kutubu

6) Viongozi wa dini, kati ya majukumu yao, mojawapo ni kukemea uovu bila ya kujali unatendwa na nani. Kukemea uonevu hasa unaotendwa dhidi ya watu wasio na mamlaka. Je, nanyi mlitimiza wajibu wenu? Mnatakiwa kutubu.

7) Viongozi kwa kutumia nafasi zao vibaya, wamewafukarisha watu kutokana na chuki za kisiasa, kinyume cha utawala bora. Wanatakiwa kutubu.

Kwa wale wakristo (hata waislam naamini kutakuwa na aya za kuthibitisha umuhimu wa kutubu), biblia imeongea maeneo mengi juu ya toba (kutubu):

Warumi 2:5
Lakini unao ugumu na moyo usiotaka kutubu, na hivyo unajirundikia adhabu kwa siku ya ghadhabu wakati hukumu ya Mungu itakapodhirishwa.

Ufunuo 2:5
Basi pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Ufunuo 3:3
Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyosikia, uyatii na kutubu. Usipoamka nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutajua saa nitakayokujia.

2 Wakorinto 7: 9
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu.

Matendo 3:19
Basi tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Matendo 11:18
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, 'Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai'.

Kuna aya nyingi katika biblia zinaongelea kutubu kama ndiyo mlango wa kumkaribia Mungu.

Nini Maana ya Kutubu
Neno tubu katika imani lina maana ya 'geuka au badilika'. Katika toba kuna mambo makuu mawili, moja ni kugeuka au kuukana uovu, na ya pili ni kugeukia njia ya kweli yaani njia ya haki. Mara 3 Ezekiel aliwaambia Wayahudi, 'Tubuni, jitengeni na miungu na matendo yenu mabaya, badilikeni, badilikeni kutoka kwenye njia zenu za uovu.

Katika agano jipya, kutubu kunaelezwa kuwa lazima kuendane na mabadiliko ya fikra, na chuki dhidi ya uovu. Mtume Marko na Matayo wanaanza kuhubiri kwa kusema, 'Tubuni', na Paulo anasema, 'mgeukieni Mungu kwa kutubu'.

Toba ni lazima iendane na kuhuzunika kuwa upo au ulikuwepo katika upungufu, upungufu wa kuyaishi maagizo ya Mungu. Wakatoliki tunaamini kuwa kutubu au toba au kitubio ni sakramenti ambayo Mungu ametupatia. Kiufupi ni zawadi.

Kama hii ndiyo maana halisi ya kutubu katika mtazamo wa imani, kwa nini Askofu Kakobe alipomtaka Rais atubu, watu wamehamaki sana? Wamehamaki kwa sababu ya ujinga, ujinga wa kutolijua neno.

Mimi binafsi, naamini Rais, viongozi wa serikali, viongozi wa dini na hata wananchi wa kawaida, tukiacha makosa ya kila mmoja katika maisha yake, kama Taifa inatubidi kutubu. Rais anahitajika kutubu kwa yale aliyoyatenda kimakosa kama kiongozi mkuu ikiwemo kutokutimiza wajibu. watendaji mbalimbali wanatakiwa kutubu. Wananchi wa kawaida wanatakiwa kutubu. Kila mmoja kwa nafasi yake.

Kama sisi ni watakatifu sana, inakuwaje katika Taifa letu:
1) Watu wanapigwa risasi hadharani, hakuna anayeweza kuzuia, kukamata wala kuzuia? Niambieni ni maandiko gani yanaruhusu haya? Kama ni uovu, lazima awepo wa kutubu.

2) Wajane maskini wanavunjiwa nyumba zao zilizojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita? Kuwafanya maskini wajane na watoto wasiishi, kuna mafundisho yoyote ya Mungu yanayoelekeza hivyo? Kama sivyo, lazima kuwepo na mtu au watu wa kutubu.

3) Watu wanakamatwa na kusweka mahabusu ovyo ovyo kama vile uwezo na uhuru wa kusema upo kwa watu wachache tu? Kuna imani inayofundisha kuwa Mungu hupenda uonevu? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

4) Watu wananunuliwa kusaliti matakwa ya waliowachagua ili waweze kuwahadaa wananchi? Kuna imani inayofundisha kuwa kumhonga mtu ni utakatifu? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

5) Polisi wanatumika kulazimisha ushindi wa CCM kwa kuwakamata wapinzani, kuwatesa, kuwateka, n.k.? Kuna utakatifu ambao unatamkwa na dini yoyote kuwa unaweza kupatikana kwa kulazimisha matakwa yao wakati kukiwa na sheria ambazo mliapa kuzisimamia, na nyinyi hamtaki? Kama hakuna, kuna watu wanatakiwa watubu.

6) Vyombo vya habari vinavyoelezea tofauti na matakwa ya watawala vinafungiwa ili viwepo vyombo vya habari vinavyosifia tu? Kuna dini inayolekeza kuwa kiongozi hata akitenda jambo baya kiasi gani hastahili kukosolewa? Kama haipo, kuna watu wanatakiwa kutubu.

7) Watu wanafukuzwa kazi bila kufuata taratibu, na wakati mwingine kwa kuonewa au kutokana na imani zao za kisiasa?
8) Watu wanapotea, haijulikani kama wapo hai au wamekufa
9) Maiti za binadamu zinaokotwa ovyo kwenye viroba, bila ya wale wanaofanya hivyo kukamatwa au kuadhibiwa?
10) Kunakuwa na ubaguzi wa kufanya shughuli za kisiasa. CCM wanaruhusiwa kufanya mikutano, vyama vya upinzani vinazuiwa?
Na mingine mengi.

Wakatoliki tunaposali ile sala ya toba huwa tunasema ....... kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. Hivi tunafahamu kuwa kutubu kule hakuna maana yoyote mbele ya Mungu kama hakuna dhamira ya dhati ya kuacha uovu?

Kutokana na haya, kama Taifa tunastahili kutubu (kugeuka) na kuyakana haya yaliyo ya shetani. Rais anastahili kutubu, au kutokana na yeye mwenyewe kuagiza, au pengine kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhakikisha wale waliopo chini yake hawafanyi chochote kinyume cha katiba na hekima ya Mungu. Lakini shetani anafanya kazi usiku na mchana, anawatumia mawakala wake, hao ndio wanaojifanya wanampenda Rais, na kutaka akubali uovu uliopo uendelee. Hawa ni mawakala wa shetani. Rais atafakari maeneo yote ambayo ametenda sivyo, amwombe Mungu amsaidie kumjalia hekima ili azitambue na hizi roho za shetani zinazokuja mbele yake na kujifanya wanampenda kuliko hata Mungu aliyemwumba. Rais atende kadiri ya Roho ya Mungu itakavyomwongoza.

Viongozi wa dini wanatakiwa kutubu kwa kushindwa kukemea uovu kwa dhamira ya moyo, na kuwa wakweli kama alivyokuwa nabii Mika na Yesu mwenyewe ambapo kuna wakati aliwakaripia watawala wa Kiyahudi (Mafarisayo na Wanasheria) akiwaambia ole wenu mafarisayo na waandishi wa sheria kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopambwa kwa nje kumbe ndani yamejaa uchafu.

Wananchi wa kawaida tunatakiwa kutubu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wetu kama raia wema, yaani kukemea uovu kwa nguvu zetu zote bila ya kuogopa chochote maana Mungu ametupatia roho ya ujasiri ya kunena UKWELI.

Wale wanaotaka kufanya toba wasali pamoja nami kwa dhamira:

Bwana Mungu wetu, Mungu wa msamaha, nashukuru kwa msamaha wako. Nashukuru kwa kunivumilia katika uovu wangu. Kama Kiongozi wa nchi/Kiongozi wa Dini/raia wa nchi, nimekutenda dhambi wewe na ndugu zangu kwani kwa kushiriki au kwa kutotimiza wajibu wangu, nimesaidia uovu uendelee kutendeka katika Taifa lulilonijalia.

Naomba roho yako ya ujasiri juu ya Kweli yako ikae ndani yangu ili nisiogope chochote mahali popote kuunena ukweli kwa kadiri ya mapenzi yako hata kama nitapuuzwa au kuteswa. Nitakapopuuzwa au kuteswa, ukuu wako ukazidi kudhihirika zaidi na zaidi.

Naomba uipokee sala yangu, sala ya toba, sala ya kugeuka kutoka kwenye njia ya uovu kuelekea kwenye njia yako. Bwana ulisema, 'ombeni mtapewa', nami kwaajili ya ahadi yako hii, daima nasimama katika tumaini la haya nikuombayo.
Mjomba naona umetumwa, mbona Hakuna mstari wa kukemea waovu wanaoshughulikiwa na serikali barabara?, wanao tuvunjia majumba usiku, wanaozini wake za watu, wasenge nk,umekazana kutaja serikali tu, wacha double standard ki aina kwa kujaza mistari mingi ya biblia
 
Nimezingatia hoja ya 'toba' yaani 'kutubu'.
 
Sasa kwenye toba mbona umeipoint viongozi wa serikali pekee, kwani toba inawahusu only them?

Soma vizuri.

Nimewataja viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wananchi wote. Ufahamu pia nilikuwa naongelea toba ya nchi kutokana na makosa yanayotendwa kitaifa ambayo yanathiri Taifa zima, siyo toba ya maisha yako binafsi au toba inayoendana na makosa katika familia.

Unapoongelea mambo yanayoathiri Taifa, nafasi kubwa inakuwa kwa wale waliopewa mamlaka ya kusimamia ustawi wa Taifa. Kwa mfano unapotokea ugandamizwaji wa haki za raia unaofanywa na Polisi, ni dhahiri wajibu mkubwa utakuwa kwa Amiri Jeshi Mkuu na makamanda wake. Nafasi ya raia itakuwa ni kupaza sauti tu. Hawana uwezo wa kutoa amri yoyote kwa Polisi. Hivyo toba juu maovu yanayofanywa na Polisi, kimsingi inatakiwa kufanywa na Amiri Jeshi Mkuu, makamanda na askari aliyetenda. Mwanannchi wa kawaida anaweza kulazimika kufanya toba kama alisaidia kuficha uovu au kushabikia au kufurahia uhalifu uliotendwa.
 
Naona polisi tena, ndo mfano, Haya!
 
hata hivyo Magu si kaapa kwa kutumia biblia? neno kutubu halimo? hizi zambi wanazomsema hafanyi?
 
Kwani siku ya hukumu nyie ndiyo mtakuwa msemaji wake mpaka muwashwe na dhambi zake?

Mkosoeni kwenye mambo yanayowahusu ambayo ameshindwa kutekeleza hayo mambo ya kutubu waambieni mama zenu ndiyo wanaowahusu.
 
Mtu alazimishwi kutubu Bali hutubu kwa hiari yake mwenyewe ili Mungu aweze kumsamehe na kumbadilisha, kumlazimisha mtu ni kuchochea au kumuongezea hasira hivyo akaamua kufanya lolote dhidi yako.

Kwa kuwa Mungu anatambua mamlaka za DUNIA basi anamtambua Mheshimiwa rais na viongozi wengine na mamlaka ya duniani ndio mamlaka ya mwisho yenye kutoa MAAMUZI kwa hata viongozi wa dini wanapaswa kutii..

Mheshimiwa rais wachukulie hatau wale wote ambao hawatii mamlaka ya serikali ambayo Inatambliwa na Mungu kupitia vitabu vitakatifu na wala usitishike na jambo lolote.
 
Pole sana inaonekana hujui hata maana sahihi ya hayo maneno, 'tiini mamlaka'. Mungu huruhusu hata uwepo kwa utawala mbaya kwa makusudi maalumu. Mojawapo ni kwaajili ya kuwaadhibu waliokengeuka. Kunapokuwa na dalili hizo, wanadamu hutakiwa kutubu kwa dhamira ya ama Mungu awaondolee utawala dhalimu au amjalie mtawala hekima ili baraka za Mungu zipate kushuka juu ya nchi.

Kutubu kuna maana ya kuomba upatisho kwa Mungu. Mfalme akifitinika hulaanika yeye, utawala wake na wanaotawaliwa. Ndiyo maana ni muhimu kwa watawaliwa, wakati wote kutaka uwepo upatisho kati ya mtawala wao na Mungu ili neema ya Mungu ishuke kwa watu wote.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom