mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Nimemsikia Mkuu wa mkoa Bw.Makonda akisema kuwa kuanzia sasa watu wasiwasaidie omba omba waliozagaa mitaani Na barabarani.Kwa maoni yangu nilidhani Bw.Makonda angefanya utafiti wa kina kujua in kwanini kuna Omba omba?,Pili wametoka wapi, kwanini wameamua kuomba? Serikali inahusikaje Na hao ombaomba? Majibu ya maswali hayo angepata suluhisho la kukomesha omba omba mkoani kwake.Suala la omba omba sio geni hapa Dar es salaam Na nchini Kwa ujumla tatizo Serikali haitaki kujua chanzo Na kukishughulikia .Wananchi sio rahisi kuacha kuwapa misaada hao omba omba kutokana Na imani zao za kidini Na Ubinadamu.