Kutotendewa haki kwenye kikao cha nidhamu

mle

New Member
Jul 29, 2022
3
0
Habari wakuu.

Nimeajiliwa kwenye kampuni flani Kuna kosa lilitendeka likafanyiwa uchunguzi na nikaitwa kwenye kamati ya kikao cha nidhamu yenye wajumbe 6 waliokiwepo kwenye kikao hicho, lakini pia kampuni ilikuwa na mashahidi 3 kati ya mashahidi hao mmja ndio aliyefanya uchunguzi wa hii kesi.

Cha kushangaza shahidi wa kwanza alikuwa ndo aliyefanya uchunguzi wa hii kesi alipoingia alitoa maelezo juu ya ushahidi wake alipomaliza ilitakiwa nianze kumuuliza maswali lakini cha kushangaza yeye akaruhusiwa na mwenyekiti kuanza kuni attack kwa maswali juu ya tuhuma hizo na mimi nikawa namjibu.

Lakini pia baada ya kuwa amemaliza alisema Kwa kuwa yeye ndiye aliyefanya uchunguzi anaomba yeye mwenyewe ndiye awaite mashahidi wengine 2 waliobakia na akaruhusiwa na mwenyekiti hata baada ya kutoa ushahidi aliendelea kukaa kwenye chumba hicho cha kusikiliza shauri mpaka mwisho wa kikao je hiyo inaruhusiwa kisheria? Na kwa maelezo hayo Sheria inasemaje juu hilo. Naomba kuwasilisha.

Asante
 
Sijaona tatizo kwa mtazamo wa Kisheria.
Aliyekuchunguza ndiye shahidi namba moja na kwamba katika uchunguzi wake alipata mashahidi wengine ili kuthibitisha Yale aliyosema ktk uchunguzi wake.

Wewe shida yako haswa nini mkuu?
 
Back
Top Bottom