real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,287
Waziri wa Fedha Philip Mpango ameiagiza TRA kufanya mabadiliko makubwa kwa watumishi wake waliopo bandarini baada ya kubainika wanahusika na upotevu wa mapato.
Dk. Mpango alitoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara yakushtukiza kitengo cha forodha bandarini Dar Es Salaam na kutoa siku 7 kwa TRA kumpa majibu juu ya utekelezaji wa agizo hilo.
Amesema watakao bainika waondolewe kabisa kwani kuna vijana wengi waliohitimu ambao wapo tayari kufanya kazi.
Dk. Mpango alisema akisikia juu ya upotevu wa mapato tena atawatimua wakuu wa kitengo hicho.
''Sasa next time nikija nikiyasikia tena haya ina maana hamjapiga jicho la kutosha, na mimi subira Mungu hakunipa, sina.Nitakutazameni usoni nitawatimueni''
------------
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Forodha Bandarini, na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kufanya mabadiliko ya watumishi walioko katika idara ya upimaji na ukaguzi wa mizigo.
Akiwa kwenye ziara hiyo Dk Mpango alisema imebainika kwamba kuna baadhi ya watumishi wanaojihusisha na upotevu wa mapato ya Serikali.
Waziri huyo alitoa siku saba kwa TRA kumpa taarifa kamili ya utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwamo kuwahamisha watumishi wote waliokaa muda mrefu kwenye eneo hilo la upimaji na ukaguzi wa mizigo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali katika bandari hiyo.
Waziri huyo alishangazwa na kitendo cha mapato bandarini kutoongezeka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kuiboresha akisema inatokana na baadhi ya watumishi kushirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi ya Serikali.
“Pamoja na kuwepo kwa mitambo ya kukagua mizigo (scanners), baadhi ya bidhaa zinakadiriwa kodi ndogo ikilinganishwa na thamani ya mizigo huku mizigo mingine ikiwa si ile iliyotajwa kuwamo kwenye makontena na hupitishwa na watumishi wasio waaminifu” alisema Waziri Mpango.
Aliuagiza uongozi wa TRA kuhakikisha unaongeza mapato katika Bandari ya Majahazi kutoka wastani wa mapato ya Sh3.5 bilioni kwa mwezi hadi Sh5 bilioni kuendana na malengo yaliyowekwa baada ya kubainika kwamba kuna ukwepaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika eneo hilo.
Pia, Dk Mpango ambaye aliwahi kuwa Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha waziri, aliutaka uongozi huo wa TRA kuhakikisha kuwa Bandari ya Majahazi inaanza mara moja kutumia mfumo wa kukusanya mapato ujulikanao kama Tansis ili kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.
Aidha, aliviagiza vyombo vya dola kuwachunguza watumishi wote wakiwamo wa ngazi za juu katika idara ya forodha bandarini na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vyovyote vinavyoikosesha Serikali mapato.
Ofisa Habari Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Leonard Magomba alitoa tahadhari kwa watu wote ambao wana tabia ya kuingia maeneo ya bandari kwa lengo la kuiba mali za wateja akiwataka kuacha mara moja kwani vifaa vya ulinzi na usalama vilivyopo hivi sasa ni vya kisasa na vina uwezo wa kubaini wezi katika maeneo yote ya bandari.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alitembelea TPA na kuiagiza mamlaka hiyo kununua mashine nne za kukagulia mizigo inayoingia bandarini hapo.
Pia, Rais Magufuli aliagiza mkataba wa kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Shehena za Kontena Bandarini (Ticts), ufanyiwe marekebisho ili kulinufaisha Taifa kutokana na oparesheni zake bandarini.
Rais aliitaka TPA kujenga bandari kavu Mlandizi na kutozitumia binafsi zilizopo kwa kuwa zinatumika kukwepa kodi.
Itakumbukwa kwamba, Novemba 2015 muda mfupi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya ghafla TRA na bandarini na kuwasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya Sh80 bilioni.
Desemba 2015, Waziri Mkuu alifanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.
Alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICD).
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
Akiwa kwenye chumba cha scanner, Waziri Mkuu alikuta manifest ikisema kontena limejaa diapers, lakini picha ya kompyuta ya scanner ilionyesha ndani ya kontena hilohilo likiwa na vitu kama vifaa vya umeme.
-Mwananchi-