Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri

Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri

ifa96

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
511
Reaction score
345
Heshima kwenu wakuu

Kama kicha cha habar hapo juu mke wangu amekuwa na hili tatizo miez sita sasa amekuwa akitokwa na uchafu ukeni Kama maziwa mgando iv,hii shida ilianza alipopata uja uzito bahat mbaya mimba iliharibika nilimwaisha hospital akapata huduma saf na kusafishwa pia,lakin tangu apo ndo shida ilipoanza nimeenda sono zaid ya mara 6 hana shida,

Amepimwa saratan hamna ametumia dawa na sindano pia lakn bado shida iko pale pale magonjwa yote ya zinaa tumepima majibu ni hamna,
KWA SASA MKE WANGU AMEKOSA NURU,HAJIAMINI TENA,ANAONEKANA KAMA MTU ALIEKATA TAMAA
msaada wenu wakuu ili aweze kuwa salama tena
 
Heshima kwenu wakuu
Kama kicha cha habar hapo juu mke wangu amekuwa na hili tatizo miez sita sasa amekuwa akitokwa na uchafu ukeni Kama maziwa mgando iv,hii shida ilianza alipopata uja uzito bahat mbaya mimba iliharibika nilimwaisha hospital akapata huduma saf na kusafishwa pia,lakin tangu apo ndo shida ilipoanza nimeenda sono zaid ya mara 6 hana shida,amepimwa saratan hamna ametumia dawa na sindano pia lakn bado shida iko pale pale magonjwa yote ya zinaa tumepima majibu ni hamna,
KWA SASA MKE WANGU AMEKOSA NURU,HAJIAMINI TENA,ANAONEKANA KAMA MTU ALIEKATA TAMAA
msaada wenu wakuu ili aweze kuwa salama tena
Mfanyie Culture wa rule out bacteria wanaosababisha tatizo.
 
Nimewai kwenda mkuu aliambiwa ni bacteria ila kila akitumia dawa tatizo haliishi tumerudi kaandikiwa sindano akimaliza dose tatizo liko pale pale
MKuu na wewe unapaswa kupima, fanya kipimo cha kuotesha mkojo (Culture) huenda wewe ukawa ni carrier wa fangasi ukawa unamuambukiza yeye. Amini nisemayo, unaweza ukawa una candida kwenye njia ya mkojo ambao wewe hawakudhuru ila ukija kwa mwenzako unamwagia wa kutosha.

Lakini jambo la pili huenda huo uchafu ukawa unatokana na Hormone imbalance sio lazima iwe maambukizi pekee. Na hapo alipokua mjamzito ndlo alipatwa na mabadiliko makubwa ya hormone. Katika hili umuone daktari wa magonjwa ya wamama.
 
Tatizo dogo tu ilo ni P.I.D hiyo na Dawa za kuondoa tatizo kabisa zipo Mkuu, Kuna magome ya kuweka kwenye maji ya moto kwenye chombo ambacho ataweza kukalia akiwa uchi kwa wastani wa dk 15 tu ule mvuke uingie vizuri ndani ya wiki tu kwisha
 
Huu ni uchafu mkuu sio ute ni mfano wa mabonge madogo madogo ya mtindi asee yan amekuwa hajiamini kabisa mpaka nuru imepotea
Ooho hio sio kawaida ni hatari kwa afya ya mji wa mimba na mirija ya uzazi na hospitali mlifikia hatua gani?
 
Ooho hio sio kawaida ni hatari kwa afya ya mji wa mimba na mirija ya uzazi na hospitali mlifikia hatua gani?
Tukienda ni dawa ni sindano lakin bado tatizo haliishi na tunachoambiwa ni bacteria pia sono aliambiwa kuna shida kidogo kwenye mayai
 
Back
Top Bottom