Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Za leo wapendwa
Jamani matatizo mengi katika mapenzi yanatokana na siri za ndani kuvuja, na hili mara nyingi linasababishwa na jinsia ya kike ingawa kuna jinsia ya kiume ambao nao hawana siri lakini -ke tunaongoza.
Fikiria kwenu walijuaje mshahara wa mume wako? Baba yako akiwa na tatizo anapiga simu kichwani anawaza ile milioni 3 aliyopokea mkwe mwezi huu, wakati mkwe alichukuka mkopo wa milioni 30 bank ili apate kiwanja angalau maeneo ya hadhi yake, ana mkopo wa gari na kwa sasa hivi bado amepangisha.
Mnapokuwa kwenye mapenzi kabla ya uchumba ni muda wa kujenga uaminifu, uaminifu huu si tu wa ngono bali uaminifu wa kutunziana siri. Hakuna uchawi mkubwa Zaidi ya mwanaume kukuamini na siri zake, na yeye ni binadamu atatafuta tu mahali pa kupunguzia pressure.
Hata ikitokea mmegombana, mwanaume anaekuamini ataanza kufikiria jamani nimempoteza best friend wangu, atakuja tu na mtayamaliza. Sasa leo jamani mume amenunua nyumba Makongo Juu, anakutana na shost uliyesoma nae Kifungilo miaka ile ya Sr Redemta anamwambia shem hongera jamani mmenunua nyumba, mume anaona aibu. Yote hayo ni katika kumuonyesha shost wa Kifungilo kuwa na wewe matawi.
Mkigombana ndiyo mume anakuja mwanamke huna siri wewe, haya Yasinta alijuaje habari ya mimi kununua nyumba Makongo Juu. Unapoteza uaminifu, siku nyingine akifanya lake hakwambii. Mwisho akikutana na Sky Éclat akimwamini unakuja kunirarua makucha ya uso eti mimi mwizi wa mumeo.