Kutokuwa na Ajira, nini sababu Kwa Vijana Wa kitanzania

good96

JF-Expert Member
Nov 20, 2015
518
537
Habarini wakuu
Nijielekeze moja kwa moja kwenye mada, nimekua nikijiuliza Kwa muda mrefu nini hasa ni chanzo ama sababu Kuu ya kuwepo/kuongezeka Kwa tatizo la Vijana wasio na ajira mtaani.
1)Je ni Mfumo Wetu wa elimu unatufanya kujenga Vijana tegemezi? au
2)Ni uoga wa kuthubutu kujiajiri na kubaki kutegemea mfumo wa Ajira(kuajiriwa) ama
3)Ni uvivu umejengeka Katika kizazi cha Vijana Wa kileo?

Karibuni Kwa mjadala wakuu
 
Vyote ulivyoorodhesha vina sehemu yake kwenye tatizo hili la kitaifa. Kuiacha sababu yoyote kati ya hizo tajwa juu ni kuitetea na ukandamizaji kwa nyingine.
Kama tujinasue kitaifa, basi haja ya kuzipandikiza fikra za kijasiriamali tangu shule za msingi ipo na iwe mtaala kama ilivyo vyuoni. Si kwamba nailaumu sababu ya 1, bali naganga yajayo. Mtu mzima aliyetoka tangu shule ya awali na wazo kuwa akimaliza elimu ya juu anapatiwa kazi, unataka kumbadili chuoni GHAFLA kwa somo la ujasiriamali na kujiajiri (Entrepreneurship)...?
Bahati kwa wanaolielewa haraka, ila tusiwalaumu wasiolielewa kama nilivyoielewa nukta ya 2.
 
Umeeleweka Vyema mkuu
 
Elimu ya kwenye vyeti ni tatizo kubwa sana hili suala hutaliamini ila nakuhakikishia wasomi wengi wa kitanzania wanakosa ajira hapa namaamisha kujiajiri na kuajiriwa pia,,,ni kama wiki mbili zilizopita ofisin kwetu tulikua tunahitaji wanne mabinti watatu mwanaume mmoja ila kubalance gender kwan waliopo wote ni vidume nikaanza kutangaza hyo kazi ilikuwa ni post ya afisa mauzo kwenye bank kubwa tu nilibahatika kupata CV za wasichana wawili walikuja ofisin nikapannga siku ya interview huwezi amin nlpoanza kuwaeleza job description kuwa watakua wanaenda kutafuta wateja kwenye makampuni kwa ajili ya mikopo na accounts then watakuwa wanalipwa kwa commission na mtu una uwezo wa kujilipa hadi million tano it depends na volume ya mikopo yako...wakawa inspired sana walipoanza kazi ndo vituko sasa wanakwambia mm na degree yangu nianzu kuzurura juani kama machinga hawakudumu hata mwez wakakmbia..
Nilinote kitu hizi taalum za kwenye makaratasi ni upuuzi sana znafanya tusiwe committed,tuwe na negative mindset juu ya kaz fulani
 
Duuh hio ni changamoto mkuu
 
Kuna ongezeko kubwa la wasomi nchini, ukijumlisha na population pia ya nchi!

So tutegemee hilo zaidi
Mkuu mi nadhani population ikiongezeka na wasomi inabidi pia waongezeke maana hii kitu inakuwa direct proportional. Mfano kama kulikuwepo na viwanda vinne vya unga wa kula itabidi viongezeke ili kuweza kufeed the increased population hivo wasomi zaidi watahitajika viwandani hapo, shule nazo zotaongezeka hivo hivo walimu zaidi watahitajika.......
 
Wengi hawataki kujiajiri kwa kusingizia mtaji hawana, wameshakariri kwamba akitoka chuo ni kuajiriwa tu hakuna kingine. Sasa ukishailock mind yako ikawa hivi ni tatizo kubwa sana, lazima vijana muwe wabunifu kwa kutumia elimu mliyopata vyuoni, mkishindwa kabisa fanyeni copy and paste kutoka kwa watu waliofanikiwa
 
Moja mpaka tatu vinaweza kua sababu...

Tupo wategemezi sana kuliko kujitegemea hilo ni tatizo sana...

Cc: mahondaw
 
Mkuu mi nadhani population ikiongezeka na wasomi inabidi pia waongezeke maana hii kitu inakuwa direct proportional. Mfano kama kulikuwepo na viwanda vinne vya unga wa kula itabidi viongezeke ili kuweza kufeed the increased population hivo wasomi zaidi watahitajika viwandani hapo, shule nazo zotaongezeka hivo hivo walimu zaidi watahitajika.......
Nakubaliana na wewe....
Tatizo unakuta Kuna wasomi wengi katika kozi moja ambayo tayari huku makazini au kwenye ajira imeshajikamilisha na wengine wako majumbani....

Wizara ya Elimu nayo iongeze kozi kulingana na jinsi nchi inavyojiendeleza...

Wengi wanaosoma nje ya nchi wakirudi wanaajiriwa mapema kuliko aliyesoma Tz sababu alichopata huko nje Tanzania hakipo...na unakuta Kampuni nyingi zinahitaji watu wa namna hiyo...
 
I got your point bro.....
 
Back
Top Bottom