Ndugu zangu wana jamvi, kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa katika wimbi zito la rushwa na ufisadi ambalo limetawala mijadala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Athari za rushwa na ufisadi uliokithiri hapa nchini zinaonekana moja kwa moja katika ufanisi wa Serikali na taasisi zake na taasisi binafsi kwa sababu ya udhaifu wa regulatory system na mfumo wa maisha.
Jitihada mbaliambali zenye nia thabiti ya kurekebisha hali hii zile zile za funika kombe mwanaharamu apite zimefanyika na matokeo yake ni kidogo sana na yamejaa mashaka kama si kwamba hayapo kabisa.
Tume mbalimbali zimeundwa lakini aidha zimetoa matokeo yasiyosahihi kwa makusudi, ama zingine zimetoa matokeo sahihi lakini hakuna hatua rekebishi zilizochukuliwa.
Takukuru ndiyo imekuwa mlinzi na mtetezi na msafishaji wa ufisadi kwa sababu mfumo huu umeasisiwa na Serikali ambaye ndiye mwajiri wa Takukuru.
Wanasiasa wa vyama pinzani hasa CHADEMA na hatimaye wameungwa mkono na wale wa chama tawala ccm wamefichua mambo makubwa ya kifisadi na kuyapigia kelele. Hakuna hata mtuhumiwa mmoja ambaye amethibitisha kuwa msafi katika hizo tuhuma, lakini la kusikitisha, hakuna hatua yoyote imechukuliwa badala yake tunaona serikali ikiungana na hao watuhumiwa na kuendelea kudunda as if hakuna kitu.
Wananchi maskini wanazidi kuwa maskini wa raslimali na ufahamu. Kwa umaskini huo hata uwezo wao wa kuelewa na kuchukua maamuzi sahihi ni mdogo. Wanahadaika kwa vitisho na hofu ya wasiyoyajua na hivyo kuwa submissive wakisuribiri siku zao za kuondoka duniani zifike wafe wazikwe basi yaishe.
Sasa kwa kuwa TAKUKURU, MANENO YA WANASIASA, TUME, MAISHA DUNI YANAYODIDIMIA KILA KUITWAPO LEO YA WATANZANIA, havijaweza kutikisa mfumo wa Rushwa na Ufisadi, nini sasa kifanyike?
Wanajamvi naomba tushauriane hapa ili tupate njia sahihi itakayoifanya Serikali hii inayoendekeza rushwa na ufisadi, kutokujali mauti ya Watanzania, iweze kuwajibika na kutambua kwamba iko madarakani kwa ajli ya wa Tanzania. Iweze kulinda katiba na kuwatumikia wa Tanzania kwa nia na moyo wa kizalendo.