Kutokomeza rushwa na ufisadi Tanzania - nini kifanyike?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Ndugu zangu wana jamvi, kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa katika wimbi zito la rushwa na ufisadi ambalo limetawala mijadala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Athari za rushwa na ufisadi uliokithiri hapa nchini zinaonekana moja kwa moja katika ufanisi wa Serikali na taasisi zake na taasisi binafsi kwa sababu ya udhaifu wa regulatory system na mfumo wa maisha.

Jitihada mbaliambali zenye nia thabiti ya kurekebisha hali hii zile zile za funika kombe mwanaharamu apite zimefanyika na matokeo yake ni kidogo sana na yamejaa mashaka kama si kwamba hayapo kabisa.

Tume mbalimbali zimeundwa lakini aidha zimetoa matokeo yasiyosahihi kwa makusudi, ama zingine zimetoa matokeo sahihi lakini hakuna hatua rekebishi zilizochukuliwa.

Takukuru ndiyo imekuwa mlinzi na mtetezi na msafishaji wa ufisadi kwa sababu mfumo huu umeasisiwa na Serikali ambaye ndiye mwajiri wa Takukuru.

Wanasiasa wa vyama pinzani hasa CHADEMA na hatimaye wameungwa mkono na wale wa chama tawala ccm wamefichua mambo makubwa ya kifisadi na kuyapigia kelele. Hakuna hata mtuhumiwa mmoja ambaye amethibitisha kuwa msafi katika hizo tuhuma, lakini la kusikitisha, hakuna hatua yoyote imechukuliwa badala yake tunaona serikali ikiungana na hao watuhumiwa na kuendelea kudunda as if hakuna kitu.

Wananchi maskini wanazidi kuwa maskini wa raslimali na ufahamu. Kwa umaskini huo hata uwezo wao wa kuelewa na kuchukua maamuzi sahihi ni mdogo. Wanahadaika kwa vitisho na hofu ya wasiyoyajua na hivyo kuwa submissive wakisuribiri siku zao za kuondoka duniani zifike wafe wazikwe basi yaishe.

Sasa kwa kuwa TAKUKURU, MANENO YA WANASIASA, TUME, MAISHA DUNI YANAYODIDIMIA KILA KUITWAPO LEO YA WATANZANIA, havijaweza kutikisa mfumo wa Rushwa na Ufisadi, nini sasa kifanyike?

Wanajamvi naomba tushauriane hapa ili tupate njia sahihi itakayoifanya Serikali hii inayoendekeza rushwa na ufisadi, kutokujali mauti ya Watanzania, iweze kuwajibika na kutambua kwamba iko madarakani kwa ajli ya wa Tanzania. Iweze kulinda katiba na kuwatumikia wa Tanzania kwa nia na moyo wa kizalendo.
 
Tuwekeze kwemye elimu kwanza ili watanzania wasipige kura kama vile wanachagua vitumbua. Kura nyingi zinatoka vijijini, huko kama mwaka wa uchaguzi kukiwa na mvua ya kutosha na wananchi wakavuna mazao ya kutosha basi wao upigia CCM ambayo ni fisadi.

Bila kuondoa CCM madarakani rushwa kuisha ni ndoto
 
.Sasa kwa kuwa TAKUKURU, MANENO YA WANASIASA, TUME, MAISHA DUNI YANAYODIDIMIA KILA KUITWAPO LEO YA WATANZANIA, havijaweza kutikisa mfumo wa Rushwa na Ufisadi, nini sasa kifanyike?

Wanajamvi naomba tushauriane hapa ili tupate njia sahihi itakayoifanya Serikali hii inayoendekeza rushwa na ufisadi, kutokujali mauti ya Watanzania, iweze kuwajibika na kutambua kwamba iko madarakani kwa ajli ya wa Tanzania. Iweze kulinda katiba na kuwatumikia wa Tanzania kwa nia na moyo wa kizalendo.

How old are you buddy? No disrespect. Because even my STD I hero boy will give a definite answer of your question.

The Solution of all this mess is TO VOTE CCM OUT OF POWER. With CCM clinging on power we are doomed
 
Sawa kiongozi. Kama tatizo la maumivu ya wa TZ ni ccm, kwa n ini bado wanaendelea kuipa uongozi? Nini kifanyike ili kuitoa ccm madarakani kama ndiyo solution?
 
Mind set ni jambo la msingi hapo. Ni lazima tujifunze uzalendo wa dhati, pia watakao bainika wamejihusisha na rushwa na ufisadi wachukuliwe adhabu kali ili liwe fundisho na kwa wengine.
 
TZ haina tatizo. Tatizo ni CCM na serikali yake zaifu isiyo na mwelekeo. Kiufupi hatuna viongozi waadailifu wanaofuata utaratibu uliowekwa. Mfano ni sula la Mh Lissu na sakata la uteuzi wa majaji wasio na sifa. Mifano ni mingi mno ktk kila sekta na ndio kiini cha rushwa na ufisadi uliokithiri amabyo sasa ndio itikadi ya CCM wakiita takrima. waTz tunanze sasa kuwaondo CCM na Chama chechote kitakacho kuja ambacho hakitaweka mbele maslahi ya waTZ.
 
kuitoa CCM madarakani si rahisi kama mnavyodhani manake wana-jeshi la polisi, JWTZ, wana mahakama, wana-takukuru kwahiyo si rahisi kiasi hicho manake vyama vingine hawana vyombo hv
 
Katiba ya Nchi yetu haisemi Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Nchi ni vya Chama Tawala, Bali ni Vya Wananchi na Vyama na Taasisi Vyote aka Wote, Kila Mwananci ana Haki ya Kulindwa kwa Mali na Uhai wake.
Kazi yao kubwa ni Kulinda Mali za Wananchi na Mipaka ya Nchi na Kudumisha Amani na Usalama wa Wananchi.

Tatizo ni Sisi Wananchi aka Watanzania, acha Kuwasingizia CCM na Serikali. Wananchi aka Watanzania ndio wenye Nchi, Ndio tumemwajiri Rais.

TZ haina tatizo. Tatizo ni CCM na serikali yake zaifu isiyo na mwelekeo. Kiufupi hatuna viongozi waadailifu wanaofuata utaratibu uliowekwa. Mfano ni sula la Mh Lissu na sakata la uteuzi wa majaji wasio na sifa. Mifano ni mingi mno ktk kila sekta na ndio kiini cha rushwa na ufisadi uliokithiri amabyo sasa ndio itikadi ya CCM wakiita takrima. waTz tunanze sasa kuwaondo CCM na Chama chechote kitakacho kuja ambacho hakitaweka mbele maslahi ya waTZ.
 
ccm nilazima kife kibudu

Kiongozi kama mwarobaini wa matatizo haya ni kuindoa ccm madarakani, kwa nini bado inaendelea kupewa nafasi za uongozi? Nini kifanyike ili hii ccm ife hicho unachokisema? Toa maoni kiongozi.
 
kuitoa CCM madarakani si rahisi kama mnavyodhani manake wana-jeshi la polisi, JWTZ, wana mahakama, wana-takukuru kwahiyo si rahisi kiasi hicho manake vyama vingine hawana vyombo hv

Sasa tunafanyaje mkuu. Kumbuka tunazidi kuteketea sisi na watoto wetu!. Unashauri tufanye nini sasa katika hali hii?
 
Katiba ya Nchi yetu haisemi Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Nchi ni vya Chama Tawala, Bali ni Vya Wananchi na Vyama na Taasisi Vyote aka Wote, Kila Mwananci ana Haki ya Kulindwa kwa Mali na Uhai wake.
Kazi yao kubwa ni Kulinda Mali za Wananchi na Mipaka ya Nchi na Kudumisha Amani na Usalama wa Wananchi.
hilo linafahamika wazi na ndivyo inavyotakiwa but angalia yanayotendeka kama yanaendana na katiba, angalia ya Iringa kwa Kamuhanda, angalia mauji mengine yanayofanywa na vyombo vya dola kila kona, tuna kwa uonevu kisa wanasapoti vyama vya upinzani, hata JK juzi kawambia waache kutegemea polisi,angalia usalama wa Taifa wanavyotetea na kuihakikishia maisha CCM
 
Katiba ya Nchi yetu haisemi Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Nchi ni vya Chama Tawala, Bali ni Vya Wananchi na Vyama na Taasisi Vyote aka Wote, Kila Mwananci ana Haki ya Kulindwa kwa Mali na Uhai wake.
Kazi yao kubwa ni Kulinda Mali za Wananchi na Mipaka ya Nchi na Kudumisha Amani na Usalama wa Wananchi.

Sawa mkuu, umesema vyema. Sasa tunapoona chama tawala kinatumia hivi vyombo vya umma kwa maslahi yake binafsi katika ufanikisha kudumu katika utawala kwa njia zisizo sahihi, tunafanyaje sasa? Mchango wako ni wa thamani sana kiongozi.
 
Wapinzani waongeze Wabunge Ubungeni sio lazima wawe wa Chadema tu, hii itapunguza baadhi ya Mambo kupitishwa kirahisi bila kujadiliwa kwa kina. Somo la Elimu la Uraia kama halipo lirudishwe Mashuleni, hii itasaidia Wananchi aka Watanzania kujua Haki na wajibu wao. Kuhamashisha Wananchi aka Watanzania Kulipa Kodi ili tupate Huduma Bora na Nzuri, Wachache wanakwepa Kodi kama sio Wengi. Viongozi wawe Wazalendo wakubali kuwajibika watambue Uongozi ni dhamana. Viongozi aka Wananchi aka Watanzania tufuate na kutii Sheria na Katiba ya Nchi.

Ndugu zangu wana jamvi, kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa katika wimbi zito la rushwa na ufisadi ambalo limetawala mijadala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Athari za rushwa na ufisadi uliokithiri hapa nchini zinaonekana moja kwa moja katika ufanisi wa Serikali na taasisi zake na taasisi binafsi kwa sababu ya udhaifu wa regulatory system na mfumo wa maisha.

Jitihada mbaliambali zenye nia thabiti ya kurekebisha hali hii zile zile za funika kombe mwanaharamu apite zimefanyika na matokeo yake ni kidogo sana na yamejaa mashaka kama si kwamba hayapo kabisa.

Tume mbalimbali zimeundwa lakini aidha zimetoa matokeo yasiyosahihi kwa makusudi, ama zingine zimetoa matokeo sahihi lakini hakuna hatua rekebishi zilizochukuliwa.

Takukuru ndiyo imekuwa mlinzi na mtetezi na msafishaji wa ufisadi kwa sababu mfumo huu umeasisiwa na Serikali ambaye ndiye mwajiri wa Takukuru.

Wanasiasa wa vyama pinzani hasa CHADEMA na hatimaye wameungwa mkono na wale wa chama tawala ccm wamefichua mambo makubwa ya kifisadi na kuyapigia kelele. Hakuna hata mtuhumiwa mmoja ambaye amethibitisha kuwa msafi katika hizo tuhuma, lakini la kusikitisha, hakuna hatua yoyote imechukuliwa badala yake tunaona serikali ikiungana na hao watuhumiwa na kuendelea kudunda as if hakuna kitu.

Wananchi maskini wanazidi kuwa maskini wa raslimali na ufahamu. Kwa umaskini huo hata uwezo wao wa kuelewa na kuchukua maamuzi sahihi ni mdogo. Wanahadaika kwa vitisho na hofu ya wasiyoyajua na hivyo kuwa submissive wakisuribiri siku zao za kuondoka duniani zifike wafe wazikwe basi yaishe.

Sasa kwa kuwa TAKUKURU, MANENO YA WANASIASA, TUME, MAISHA DUNI YANAYODIDIMIA KILA KUITWAPO LEO YA WATANZANIA, havijaweza kutikisa mfumo wa Rushwa na Ufisadi, nini sasa kifanyike?

Wanajamvi naomba tushauriane hapa ili tupate njia sahihi itakayoifanya Serikali hii inayoendekeza rushwa na ufisadi, kutokujali mauti ya Watanzania, iweze kuwajibika na kutambua kwamba iko madarakani kwa ajli ya wa Tanzania. Iweze kulinda katiba na kuwatumikia wa Tanzania kwa nia na moyo wa kizalendo.
 
Sasa tunafanyaje mkuu. Kumbuka tunazidi kuteketea sisi na watoto wetu!. Unashauri tufanye nini sasa katika hali hii?
tuunde mkakati wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia ifike wakati kila mtu haswa wa vijijini waichukie CCM wakisika tu neno CCM wazomee hapo hata CCM wenyewe wataona aibu wataachia nchi wenyewe
 
Wapinzani waongeze Wabunge Ubungeni sio lazima wawe wa Chadema tu, hii itapunguza baadhi ya Mambo kupitishwa kirahisi bila kujadiliwa kwa kina. Somo la Elimu la Uraia kama halipo lirudishwe Mashuleni, hii itasaidia Wananchi aka Watanzania kujua Haki na wajibu wao. Kuhamashisha Wananchi aka Watanzania Kulipa Kodi ili tupate Huduma Bora na Nzuri, Wachache wanakwepa Kodi kama sio Wengi. Viongozi wawe Wazalendo wakubali kuwajibika watambue Uongozi ni dhamana. Viongozi aka Wananchi aka Watanzania tufuate na kutii Sheria na Katiba ya Nchi.

uzalendo sijui kama utawezekana manake kila mmoja anawaza wizi tu, mara EPA, Kagoda, Meremeta, mara RADA mara mabilioni ya Uswis duuuuuuh sijui hata where are going
 
Dawa ya Viongozi wabovu ni kwenye Uchaguzi, tusikubali kununuliwa, tusikubali kuwachagua Viongozi wabovu kwa ajili tu ni Ndugu aka Rafiki zetu, maana matatizo yakitokea ni ya Wananchi wote haijalishi ni CCM, Chadema, CUF.

Sawa mkuu, umesema vyema. Sasa tunapoona chama tawala kinatumia hivi vyombo vya umma kwa maslahi yake binafsi katika ufanikisha kudumu katika utawala kwa njia zisizo sahihi, tunafanyaje sasa? Mchango wako ni wa thamani sana kiongozi.
 
Turudi kweneye historia ya utawala wa TANU/CCM wakiti wa "party supremacy" na katiba yake. Huo mfumo ndio matokeo tulinayo lalamikia hivi sasa. Lakini inchi ni wa waTZ ndio wenye uamuzi si watu wache. waTZ wakiachana na kukubali kuhongwa khanga, kofia, bakuri za maharage, kuuza kadi za kupiga kura nk., kujiandikisha na kupiga kuro kuiondoa CCM,. CCM itaondoka tu.
 
Back
Top Bottom