Kutokomeza rushwa na ufisadi Tanzania - nini kifanyike?

Ni Kweli Zema, inatia Uchungu aka inauzunisha na kusikitisha kuona na kusikia baadhi ya Watu aka Mafisadi wakitafuta bila huruma Mali za Watanzania wote inhali Huduma Muhimu zikiwa Duni. Ila mimi naamini kila kitu Kinawezekana, Tukiamua. Uzuri Watanzania aka Wananchi wa leo sio wa Miaka ile, Mijini unaona wanavyotoka Usingizini, Elimu hii ipelekwe na Vijijini. Siku moja Mambo yatanyooka tu.

uzalendo sijui kama utawezekana manake kila mmoja anawaza wizi tu, mara EPA, Kagoda, Meremeta, mara RADA mara mabilioni ya Uswis duuuuuuh sijui hata where are going
 
Rushwa haitakwisha ng'oo coz na hzo posho walizoondoa kwa watumishi wa umma wanategemea nini?

Mkuu, ni nini maoni yako kwa wale Watanzania ambao hawana vyeo na wala si watumishi wa umma? Inapofika kwamba ili apate haki yake ya kiraia na kikatiba aipate ama aikose inategemea na uwezo wake wa rushwa? Unamlinganishaje mtu huyu ambaye afanye kazi asifanye, mshahara wake uko pale pale na mtu yule ambaye hajui hata kazi anayofanya kama itamzalia matunda. Na huu ndio uhai wake na wanaomtegemea? Kwamba sasa ananyimwa huduma ama haki zake kwa kuwa eti watumishi wa umma hawapewi posho ingawa mishahara wanapata? Pengine ukizingatia kwamba mishahara hiyo hiyo wanalipwa kwa nguvu za huyo mtu wanayemnyima haki kwa sababu posho hawapewi la sivyo atoe rushwa?

Toa ushauri wako mkuu.
 
Sawa kiongozi. Kama tatizo la maumivu ya wa TZ ni ccm, kwa n ini bado wanaendelea kuipa uongozi? Nini kifanyike ili kuitoa ccm madarakani kama ndiyo solution?



Rais wa CCM hakushinda uchaguzi uliopita 2010 maana hata kura alizopata hazijulikani popote sio tume ya uchaguzi wala kwa msajili vya vyama wanajua tu %,,hata yeye mwenyewe JK hajui wapi alipata ngapi na wapi hakupata sasa hapo unasemaje??/
 
Rais wa CCM hakushinda uchaguzi uliopita 2010 maana hata kura alizopata hazijulikani popote sio tume ya uchaguzi wala kwa msajili vya vyama wanajua tu %,,hata yeye mwenyewe JK hajui wapi alipata ngapi na wapi hakupata sasa hapo unasemaje??/

Mkuu ninakubaliana na wewe. Kama uchakachuzi na ubabe, pengine kwa msaada wa polisi, tume ya uchaguzi, usalama wa taifa, takukuru diyo kinachowafanya waendelee kutawala bila idhini ya wa Tanzania, na pengine hata mchakato wa katiba wanampango wa kuuchakachua, tutafanyaje sasa? Kama raisi anajua hakushinda, lakini bado ni mbabe mwenye kiburi wala hana woga hata aibu, kikubwa ni kuendeleza huduma, ufisadi na rushwa, tufanye nini sasa kiongozi hapo?
 
jibu litapatikana CCM itakapoondoka madarakani na tukapata rais aneyechukia na kupambana na ufusadi kama dr Slaa.

Mengine yote ni ngonjera!
 
Kweli ukitaka kujua mizizi ya rushwa nchi hii subiri upatwe na tatizo linalokulazimu kupata huduma kutoka serikalini. Juzi nilimpeleka mgonjwa wangu hospitalini Muhimbili baada ya kupata rufaa kutoka hospitali binafsi, jambo la kushangaza mgonjwa wangu akiwa katika hali mbaya alicheleweshwa kwa makusudi pale mapokezi kiasi kwamba niliingiwa na wasiwasi wa kupoteza, baada ya kuuliza kulikoni mgonjwa mmoja alinijulisha kuwa natakiwa nitoe kitu kidogo kwa wale watu wa mapokezi na hii iko wazi. Baada ya kutoa rushwa kwa kuogopa kumpoteza mgonjwa wangu nilipata huduma ipasavyo.

Swali linakuja Je takukuru hawafahamu uhalifu huu unaoendelea pale Muhimbili?naanza kuamini huenda viongozi wa juu wa utawala wameruhusu jambo hili liendelee bila kificho ili waweze kujikimu lakini wakumbuke kwamba huduma wanazotakiwa kutoa sisis wananchi tumeshazilipia kwa kodi zetu!

Nakumbuka enzi za utawala wa Raisi Mobutu Seseseko Wa Zabanga wa Zaire aliwakabidhi askari bunduki na kuwaambia katika bunduki hiyo ndio atapata rizki yake. Sasa naitaka serikali itamke wazi kama ni hivyo basi tukae tukijua kinachoendela na kwamba takukuru ni joka la kibisa lisilokuwa na meno.
 
Na tatizo kubwa sasa limeongezeka, la ubabe na vitisho vya wazi kwa wanaotaka mabadiliko. Ninaona kama hali ya nchi sasa ni mbaya.

Kama kuna vyombo ama taasisi huru za kimataifa, ziambiwe kuna tatizo Tanzania, ziingilie kati ili zisaidie kurekebisha hali kabla damu nyingi zaidi haijamwagika.

Nina mkumbuka Mchungaji Mmoja anaitwa Mwasumbi, alitembea Tanzania nzima akihubiri kwamba Tanzania itubu maana hukumu ya uovu wake imefika. Sasa sijui ndio muda huu Mungu anaachilia ujinga na upofu kwa watawala ili damu zetu zimwagike?

Viongozi wa dini na serikali, waambieni watu watubu dhambi na kuacha njia mbaya ili tupone.

ccm na king'ang'anizi chako cha kutawala nchi. Utamtalwala nani wakati umeua watu wote? Nani atazalisha? Nani atalipa kodi? Utapata wapi hela za kufanyia anasa zako na uongozi wako utakuwa na manufaa gani kwako?

Kumbuka vita vikishaanza havipiganwi upande mmoja. THERE IS NO VICTORY IN DEATH MS CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom