JamboJema
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,143
- 209
Mengi yamesemwa kuhusu Chadema chama ambacho kilionekana kuwa kingeleta upinzani wa kweli kwenye ulingo wa siasa.
Lakini baada ya mambo kadhaa ya yaliofanywa na Chadema ambayo yamedhihirisha dhamira yao ya kutaka kutaka kuongoza nchi kwa kutumia mbinu chafu.
Nyingi zimeshajulikana nisingependa sana kuzirudia maana zinajulikana haswa lile la kushawishi madaktari wagome hata kwa kutumia madaktari wasioajiliwa na wanachama wao wakashawishi mgomo ..
Na sababu kuu ya mgomo kwa nini wabunge wanapokea pesa nyingi kulko wao(Ikumbukwe katika wabunge hao kuna wengine wa Chadema ambao nao wanapokea pesa na kila kitu cha bunge na hawasemi kama pesa hizi nyingi)
Sasa basi kumekuwa na mtindo wa wana Chadema kupita mitaani na kutaka kununua mashina ya CUF ambayo kwa sasa yanaonekana hayana uhai..wana Chadema hao ambao wanapita usiku na wote kama kawaida yao wa Kaskazini yaani ukikutana nao utasikia INji hii (badala ya nchi hii).
Nilibahatika nao kukutana nao Yombo Kiembe samaki wakitaka kununua shina kwa laki moja na kushawishi wanachama wa CUF wajiunge,kwa hili hawakufanikiwa ila huu mchezo mchafu hautowasaidia CUF nayo inabidi kutambua kuwa wilaya ya temeke watauzwa kwa shs 100,000/- tu.
Hii mbinu ni moja ya mapungufu ambayo yataimaliza Chadema kabla ya 2015 kwani wameshindwa kuzungumza sera zao na sasa wanatumia pesa ambazo hazijulikani zimetoka wapi ..
Hivi hamuoni aibu kujengea watu utabaka huu? Hili la ukabila halitawasaidia kuwarudisha nyuma CDM kwani wananchi washaitambua mbinu yenu hii kuwa ni potofu! Ila sasa unalojaribu kulijenga - kuleta uhasama kati ya CDM na CUF, kweli hapo ndo unaniacha hoi. Siamini kama CDM wanapesa ya kufanya hivo. Ingekuwa ni CCM ndo unawatuhumu hivo wala nisingekuwa na wasiwasi sana....kwani hao wanapesa. Hata hivyo hiyo sidhani kama inaweza kuwa mbinu yoyote ya kutukuka kwa chama chochote kinachotaka kujiimarisha. NAOMBA UJIPANGE UPYA!