Kutokea Kigali Rwanda: Kachero Mbobezi na Mshirika wa karibu wa Paulo Kagame akamatwa na kuswekwa lupango

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Mshirika huyo ambaye alikuwa mtu wa karibu na Paulo Kagame anayeenda kwa Jina la Paulo Muvunyi alikamatwa siku ya mkesho wa Christmas na hadi sasa bado anashikiliwa.

Kachero huyo ambaye pia no mfanyabiashara mkubwa alihusika na kufanisha pakubwa kwenye mchakato wa kumfuatilia, kumchunguza na hatimaye kukamatwa na Mfanyabiashara Asinapoli Rwigara.

Mfanyabiashara huyo mkubwa nchini Rwanda aliyetofautiana na Kagame baadaye aliuawa kikatili Februari mnamo 4, 2015.

Paulo Muvunji alitumika pia kuchafua jina la Marehemu Rwigara hata baada ya kifo chake.

Muvunyi anekamatwa pamoja na mshirika wake Luteni Kanali Ruzibiza kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za kufoji.

Muvunyi ni Mfanyabiashara tajiri anayemiliki Hoteli mbalimbali nchini humo ikiwemo Kivu Safari Lodge, iliyopo Wilaya ya Karongi, Jimbo la Kaskazini

Aliwahi kuhudumu akiwa Mwenyekiti wa Klabu ya Rayon Sports FC kwa vipindi viwili vya kuanzia 2005 hadi 2007 na 2017 hadi 2019.

Luteni Kanali Ruzibiza alikuwa ni Mkuu wa Brigedi Ya 307th ya Jeshi La Rwanda (RDF) Wilayani Karongi.

paul-muvunyi.jpg
 
Museveni alipoingia madarakani kwa mapinduzi 1986 alimtafuta jambazi mmoja mzowefu akaingia naye deal. Akamwambia yeye anapewa msamaha na kulipwa mshahara kwa sharti ya kuwaonyesha majambazi wote.

Jamaa alikula bata huku akifanikisha kuwapata majambazi wengi sana ambao waliuwawa na Uganda ikawa ni miongoni mwa nchi salama sana katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Walipohakikisha wamemaliza tatizo la ujambazi wakarudi kwa yule jambazi kuu aliyekua akiisaidia serikali/polisi, wakamalizana naye kwa kumpiga shaba kwa madai eti kauliwa na wenzake aliowasaliti
 
Hivi umesoma hoja hapa au ugolo mida hii
Kama wakurugenzi waliotumika kuharibu uchaguzi hapa wanavyofanyiziwa sasa. Siku 7 zimepita, mbona hatusikii mrejesho wa wakurugenzi wa ma VXR?
 
Ila tatizo kama hili lazima lifike mwisho. Kila unayemtumia leo anajua mwisho wa wenzake waliotumika kabla yake! Hawa wakubwa hujisahau hadi watapokuja kupigwa ghafla ndio watajua hawajui na mbaya zaidi hawatopata nafasi ya kujirekebisha!
 
Back
Top Bottom