Waziri wa Mambo ya Nje Mulamula natumai Ziara yako nchini Rwanda na Kuonana na Rais Kagame kutainufaisha Tanzania Kimaendeleo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,860
Achana na hawa Watu wengine wenye Chuki zisizo na sababu na Rwanda, Wanyarwanda na Rais Paul Kagame bali endelea Kushirikiana nae Rais Kagame kwani kwa sasa huyo ndiyo 'Genius' pekee wa Maendeleo, Uchumi na Mikakati aliyebakia Barani Afrika baada ya Kuondoka aliyekuwa akimrithi Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Binafsi kama GENTAMYCINE nimefurahi mno kusikia na hata kuona Picha zako Mama yangu na Mtani wangu mkubwa wa Kihaya Mwanadiplomasia Nguli Waziri Balozi Liberata Mulamula ukifanya Ziara nchini Rwanda na hasa hasa kuonana na African Genius President Kagame.

Nina uhakika kuwa hata Wewe Waziri Mulamula umefaidika na Madini mengi ya Rais wa Rwanda Kagame na utayatumia hayo Madini katika Kumshauri Bosi wako Mkuu na Watendaji wa Tanzania ili wayatumie na Tanzania ipige hatua zaidi za Kimaendeleo na iachane na Uswahili Uswahili ambao ndiyo Unawachelewesha hadi hata Kuzidiwa na Rwanda ambayo imepitia Mapito mengi na Changamoto nyingi.

Na namwomba pia hata Waziri wa Ulinzi Mama Dk. Stegomena Tax nae ikimpendeza asione Aibu au Uwoga kufanya Ziara kwenda Rwanda kuonana na Bingwa wa Medani za Vita, Ujasusi na Mikakati Rais Kagame kwani kwa Ubora wa Jeshi lake la RDF na jinsi alivyolijenga Kimafunzo, Kimbinu, Kivifaa, Kimaadili na Kimedani yako mengi ya Kujifunza na kuja kuyaiga huku Tanzania ( hasa katika ) Jeshi letu la Tanzania ( JWTZ )

Rwanda hii sasa ndiyo 'Israel' ya Afrika.
 
Aisee umejitaidi ila ungeelezea in football terms ningekuelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom