Kutoka Wanging'ombe: WanaCCM wagomea kushiriki kura za maoni kwa madai ya uonevu!

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
OKTOBA 24, 2019.

Wana CCM wa Kijiji cha Igwachanya, wamegoma kupiga kura za maoni za kumchagua mwakilishi ambaye atagombea nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho.

Hatua hiyo, imekuwa baada ya jina la mgombea mmoja ambaye ni mwenyekiti anayemaliza muda wake kutotajwa tena, licha ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake.

Wakizungumza na MTANZANIA baada ya kugomea uchaguzi wa ndani ya chama hicho juzi, wanachama hao walisema hawawezi kumchagua mtu yeyote kwa madai uchaguzi si halali.

“Uchaguzi huu, ni wa kihuni mwenyekiti wa awali wamemtoa, tunakiongozi ambaye alikuwapo ndiyo maana tumegomea hatuwezi kufanya uchaguzi huo,’’alisema Dickson Kiswaga.

Naye Tito John, alisema”Kuna mgombea tumekuja kuchagua ila kwa sababu ya wizi wa viongozi wa CCM kijiji kutaka kututeulia viongozi wanaowataka wao, tumesikia fununu wanakutana kuzungumza eti wanamtaka mtu mwingine ili kusudiaje awasaidie kwenye uchaguzi mkuu’’.

‘’Mimi nimegomea kwa sababu jina la kiongozi wangu sijaliona,hatujatendewa haki kama chama chenyewe kinafanya ufisadi,kama walimpendekeza mtu wanaomjua wao wasingetuita,’’alisema Lazaro Kilamlya.

Akisoma majina ya wagombea ambao wamepewa nafsi ya kuwania nafasi hiyo,Msimamizi wa Uchaguzi,Vumilia Kilamlya alitaja majina matatu huku jina la nne ambalo ni la mwenyekiti ambaye yupo madarakani kwa sasa halijatajwa.

Kwa upande wa mgombea ndani ya chama hicho, akiwamo Laulence Ngilangwa alisema wameshangazwa na kitendo cha wanachama kugomea uchaguzi huo na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa watampata kiongozi ambaye wanamtaka.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Jafari Kaganga ambaye amegombea kwa mara nyingine tena nafasi hiyo alisema anashangazwa na kitendo cha jina lake kukatwa kwa kuwa amekuwa akisimamia shughuli za kimaendeleo ipasavyo.

Katibu wa CCM Wilayani ya Wanging’ombe, Juma Nambaila alisema chama kina taratibu zake za kumpata mgombea anayefaa
 
Kosa kenu kukumbatia mashoga nuksi kila upande
1571388942696.jpeg
1571388942616.jpeg
tapatalk_1571921669725.jpeg
 
Hilo tatizo limetokea sehemu nyingi tu.
Hata mtaa wangu ninaoishi walifanya huo upuuzi, eti kisa kuna matajiri fulani mtaani hawampendi mwenyekiti wa mtaa anayemaliza muda wake japo alijaza fomu lakini waliongea na diwani pamoja nawajumbe wote wa kamati ya siasa jina lake halikurudi. WanaCCM waligomea uchaguzi hadi jina likarudi. na wamemchagua kwa kishindo. anapendwa hata na wanachama wa vyama vya upinzani.

Kisa cha matajiri kumchukia, kwa kuwa kuna eneo walikuwa wameongea na manispaa ili wakazi wa hapo watolewe, wajenge shule yao, sasa mwenyekiti wa mtaa akasimama kidedea wananchi wakashinda na kuruhusiwa kuendelea na makazi yao halali.
......
 
Ka wanawake kwao huwa ni kama kujichagulia mbuzi unayemtaka ale kisu siku hiyo. Wadhani mchezo wewe??
Kuna kisiwa fulani hivi, kiko ndani ya kisiwa cha Ukerewe (kisiwa ndani ya kisiwa), kinaitwa kisiwa cha KAMASI. Tulienda huko field siku moja, yaani tuliyoyakuta ni balaa. Mwenyekiti ndie, polisi, hakimu, jwtz. Kwa kifupi Mwenyekiti ndie kila kitu.
Tuliongea na wanawake, wanasema kuwa yaani kuna wavuvi wana amua kuwafanyia ushenzi, akimtongoza then akamkataa, mvuvi anakwenda kwa mwenyekiti, akifika anamwambia mwenyekiti kuwa kuna mwanamke fulani kala hela yangu halafu ananinyima, basi hapo mwanamke anaitwa kwa mwenyekiti. uamuzi wa mwenyekiti unakuwa huu hapa (fanya kama sauti ya JPM): "HEBU NENDA KAMPE MWENZIO WEWE, HAYA TOKENI MBELE YANGU NENDENI MKAFANYE, NA WEWE KIJANA ULETE MREJESHO KAMA AMEKUPA AU ANAENDELEA KUKUSUMBUA..."
 
Hahah nifanyie koneksheni niwe mwenyekiti wa huko mkuu.
 
Mkuu mbona hii ni kawaida visiwani
 
Back
Top Bottom