Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Team Membe

New Member
Jun 6, 2015
3
2
WanaJF,

Tayari baadhi ya makada tumewasili hapa mkoani Lindi kuja kumpa ushirikiano ndugu yetu Bernard Membe katika azma yake ya kutangaza nia ya kugombea urais. Makada wengi wamefika hapa Lindi, akiwemo mama Salma Kikwete. Na watu wengine mashuhuri wanatarajiwa kuja kuungana pamoja na bwana Membe ifikapo nyakati za baadae.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ni kwamba zoezi litaanza rasmi kuanzia saa 6 kamili mchana huu na linatarajiwa kumalizika saa 8 kama mambo yataenda kama yalivyopangwa. Wote mnakaribishwa.

Taarifa pia inazidi kusema: kwa wale wote ambao hamtapata nafasi ya kufika viwanja vya CCM, Lindi, basi mtaweza kuungana moja kwa moja na ndugu Membe kupitia vyombo vifuatavyo:

Kwa Televisheni-LIVE: Star TV, Azam TV, Mlimani TV na ITV

Kwa Radio-LIVE: RFA, E-FM, PRIDE-FM


==== Updates ========

IMG-20150607-WA0003.jpg

KAULI MBIU:
TWENDE NA MEMBE KWA MABADILIKO YA UHAKIKA


- Mkutano umeanza kuoneshwa live, Sir. George Kahama ameshawasili, huku mh. BM akiwa anasaini vitabu vya wageni.

- Viongozi mbalimbali wa dini nao wameshawasili kwenye eneo la mkutano.(Viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi)

- Viwanja vya CCM vimejaa huku rangi za njano na kijani ndio zikiwa zinavutia sana.

TWENDE PAMOJA ILI MPATE KUJUA YANAYOJILI kwenye viwanja vya CCM.

- Mzee Yusuph anaburudisha wahudhuriaji kwa nyimbo nzuri za Taarab akimsifia Mh. Membe.

- Benard Membe ndio anaingia kwenye ukumbi (Jukwaa Kuu) akiwa ameambatana na mke wake pamoja na viongozi waandamizi wa CCM mkoa wa Lindi.

- Benard Membe kashaketi jukwaa kuu huku utaratibu mwingine ukiendelea kulingana na ratiba.

- Sr. Kahama, Hadija Jabir,wabunge wa Lindi na Mtwara na wabunge wengine marafiki,w/kiti wa Pwani,Lindi Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi,Viongozi wa dini mbalimbali wanatambulishwa.

- Kilichovutia zaidi ni Uwepo wa mkongwe wa siasa za Tanzania Sir. Kahama aliyemaliza utumishi wake wa umma kwa uadilifu na heshima kubwa hapa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.Alipewa cheo cha Sir na malikia wa Uingereza.

- Mkutano unafunguliwa kwa Sala,Ameanza Sheikh kusoma dua kwa niaba ya Waislam ili kuombea mkutano na shughuli nzima.

- Mchungaji Patrick naye anafungua mkutano kwa sala kwa niaba ya Wakristu.

Anaongea Hadija Jabir kutoka Zanzibar

- Nimesimama hapa kutoa neno la shukrani kukushukuru wahudhuriaji wa leo. Wote tupo hapa kwa nia moja ambayo inabidi tuiendeleze, hii ni safari kwa niaba ya Benard Membe kuelekea Ikulu.

- Kwa niaba ya Wazee wa Zanzibar Tunakuombea ufike salama kwa safari ambayo umeianza mh. Benard Membe.

Anaongea Sir. George Kahama

-CCM Oyeee,Mh.Membe Oyeeee,Lindi Kuchere,Tanzania Kuchere.

Mh. Benard Membe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa muda wa wiki tatu nimesafiri sana nchini mwetu,Nimetembelea Dodoma,Mwanza,shinyanga,Tabora etc.Leo nipo hapa Lindi, wananchi ukiona mzee mstaafu kama mimi anasafiri mpaka Lindi ujue kuna jambo analitafuta.

Natafuta kitu muhimu,natafuta uongozi bora wa kuongoza awamu ya tano na uongozi huo nimeukuta hapa Lindi na na mtu huyo sio Mwingine bali ni Benard Membe.

Nimemfahamu Benard Membe since 1990 hivyo watanzania tumuunge mkono. Kwanza Membe ni mpenda amani,Ni mcha Mungu,Mchapa kazi na ni muadilifu.Pia ni mtu muhimu mwenye uzoefu wa mambo ya kimataifa na mambo ya nje.

-Membe ana elimu nzuri na amesoma shule zenye sifa kemkem duniani (Anataja shule alizosoma Mh. Membe)

- Benard Membe ni msafi,hana kashfa

- Anachukia sana Ufisadi na rushwa

- Ana uwezo mkubwa wa mambo ya usalama,hii ni sifa kubwa kwa Ukanda wa Afrika ukizingatia ugaidi uliopo sasa hivi duniani.

- Nimekuwa Waziri(sir Kahama) tokea 1957 wakati wa serikali ya ukoloni,Pia serikali awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere,ya pili ya Mzee Mwiny,ya tatu ya mzee Mkapa na ya nne ya Mh. Kikwete katika uongozi huo wote wa awamu nne wameongoza nchi yetu kwa amani upendo umoja na ushirikiano.

- Membe ndio anaweza kuongoza kwasababu hana kashfa ya rushwa na ni muadilifu .... Lindi Kuchereee. Benard Membe anafaa kupokea kijiti kutoka kwa Mh. J. Kikwete.

-Namuombea kila la heri katika safari yake muhimu na yenye harufu ya uhakika.

- Lindi Kuchere,nashukuru sana kwa kunisikiliza.

Anaongea mzee Mtopa, Profesa wa siasa.

- Ng'ara Membe, nga'ara

- Lindi Oyee,mimi sina maneno mengi ntasema machache yenye maana. Sisi sote tupo kwenye gari la Membe.Kuna safari ya matumaini,safari ya kuelekea Ikulu.

- Katika gari hii ya Membe tunaita safari ya mafanikio.

- Mungu kapima, Haki ya Mungu Membe Rais.

- Chama chetu hakibadili jina Tokea ASP ,TANU mpaka CCM.Kuna wengine wamezunguka wakaja na UKAWA, tumegundua ujanja ujanja sio UKAWA bali UKIWA.

- Uadilifu upo hapa kwa Membe,hatukumpima hapa bali tulimpima Huko kwenye Umoja wa Mataifa.

* Membe anasalimia wananchi,Mzee wa Kimwera anatoa Tambiko la kimila. Anaongea Kimwera kwa msisitizo

Anaongea B. Membe.

CCM oyeee,wakina mama,wazee tungurume kama Simba.

- Sasa tutulie tusikie neno kubwa.(Anamshukuru Mungu.)

-Nichukue nafasi hii kwa niaba ya familia yangu kuwashukuru kwa kufika kwenu hapa.

-Jogoo litakapopambanishwa na wapinzani mwezi Oktoba.

- Anatambulisha wageni waalikwa waliofika na kuwashukuru,anawashukuru wanajimbo la Mtama kwa kumuamini kwa miaka 15 kuwaongoza katika ngazi ya ubunge.

- Jimbo la Mtama liko salama na litaendelea kuongozwa na CCM hata kama nikiondoka,hakuna cha UKAWA wala UKIWA kuongoza jimbo salama la CCM.

- Nimesimama mbele yenu kutia nia kuwania nafasi ya juu ambayo ni ya Urais.

- Nimejipima,nimetuma watu wangu nchini kufanya tathmini,nimeridhika.Nina uzoefu kwenye chama,serikalini na kimataifa hivyo nimeona nafaa,nafaa kushika nafasi kubwa nchini,nafasi ya urais.

- Nimeingia kwnye chama nikiwa na miaka 22 nimemkuta mwalimu Mangula,Amenifundisha siasa.Pia kwenye chama nimeshika nafasi mbalimbali za kiuongozi kuanzia ngazi ya chini mpaka za juu (Anazitaja) - Nani kama Membe? Wananchi... Hakuna. (Anaendelea...

- Pia katika upande wa serikali hii,Nimepata uzoefu. 1978 nimekuwa kwenye idara ya usalama wa taifa.Nimefanya kazi kwenye Ubalozi kuanzia 1992 mpaka 2000 huko Canada.

- Nimekuwa naibu Waziri (Anantaja wizara husika mbili)

- Nimekuwa waziri wa Mambo ya Njee na ushirikiano wa kimataifa kwa muda mrefu.

- Anataja uzoefu wake nje ya mipika ya Tanzania (Kimataifa)

- Uzoefu huu na elimu ya kutosha vinakidhi vigezo vilivyoweka na CCM ili kuwa mgombea wa Urais.Hata vikiongezwa vingine basi tutavitimiza. Nani kama Membe...Hakuna.

- Nimetafakari sana kuhusu Urais nimeona niombe,Nimejilinganisha na watu wengine wote watia nia, na baada ya kumpitia mmoja baada ya mwingine nimeona Lindi tuna nafasi ya Kuchukua na kuwa na kiongozi wa juu Tanzania.

- Kuna nafasi za kukurupuka kuchukua lakini sio hii ya Urais, hii nafasi Muachie Membe ndio anafaa.

- Mwezi Machi mwaka huu nilikwenda Butiama kwenye sherehe za wazanaki,Nilialikwa na Chifu wa wazanaki (Wanzagi), Sikutaka kupoeza hiyo nafasi nilikimbilia haraka ili pia nikazulu kaburi la Baba wa Taifa.

- Nilisali sana kwenye kaburi la baba wa Taifa. Nilimuomba kuhusu kutia nia yangu ya kugombea Urais,kuna viatu ulivyovyiacha alivaa Mzee Mwinyi,Mzee Mkapa na Kikwete,wote hawa viliwatosha. Sasa naomba uniachie mimi nivivae.

- Pia nilimwambia mwalimu kama unaona hivi viatu havinitoshi,wewe na Mungu nipitishieni Mbali kikombe hichi.Lakini timu yangu niliyokuwa nayo iliniambia niombe,nikajiuliza mwalimu Nyerere kanisikiliza.

- Nimemtaja Mwalimu Nyerere kwasababu yeye ndio baba wa Taifa na aliyetuletea uhuru.

- Kiongozi unajisikia raha gani kuingia Ikulu kwa kununua Urais,tununue vyeo vingine lakini sio Ikulu.Ikulu hainunuliki.

- Mkapa alivyoingia alifungua barabara hasa huku Lindi na Mtwara sasa panapitika.

- Alivyoingia Kikwete aliendeleza pale na kufungua milango ya elimu. Kikwete ametoa mchango mkubwa wa kuendeleza elimu kuliko Marais waliomtangulia.

- Nikichaguliwa kuwa Rais nataka watoto wetu wawe wenye afya na wapate elimu,wamama wasitembee umbali mrefu kufuata zahanati.Madawa yawepo ya kutosha kwenye zahanati.

- Nina mambo mawili ambayo ningependa kuyasema, moja ni kuichukua Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa viwanda ulioegemea kwenye kilimo.

- Gesi iliyogunduliwa hapo pale ili kulete mwanga tu bali kuleta uchumi wa viwanda.Tunataka viwanda vitakavyo ajiri vijana.

- Pili kuuza malighafi zinazozalishwa viwandani.Tumechoka kuuziwa bidhaa kutoka jirani zetu.Yaani maligafi tuzalishe huku,wenyewe wachukue wakasindike alafu waje huku kutuuzia.Tunahitaji viwanda vyetu wenyewe ambavyo vitakuwa vinazalisha bidhaa.

Utawala Bora,
Nianze ulinzi na usalama.Nchi yetu ina tatizo la kuuawa albino,madawa ya kulevya,ujambazi na vitisho.Breki ya matukio haya unaisha mwezi wa saba.Nitapambana na kutokomeza mabo yote yanayoathiria usalama wa taifa letu na wala sitotetereka.

-Nitaimarisha vyombo vya usalama kwenye miji mikubwa na midogo.Nchi hii ilikuwa ya amani na itaendelea kuwa ya amani.

Muungano:

- Tanganyika na Zanzibar.Muungano wetu ni wa kipekee duniani,hakuna sehemu nchi nyingine muungano uliodumu kama huu wetu.Hii ni TUNU aliyotuachia baba wa Taifa.Nikichaguliwa nitaulinda huu Muungano na hakuna wa kuuvunja.

-Mapinduzi Zanzibar - Kuna watu wanakebehi Mapinduzi ya Zanzibar,hawajui kuwa mapinduzi yale yalimuweka huru mtu mweusi.Nikichaguliwa nitayazingatia Mapinduzi ya Zanzibar

Sekta binafsi

- Nchi yetu lazma isukumwe kimaendeleo na sekta binafsi. Hatujaweza kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza uchumi na kuleta ajira. Hatujaunganisha sekta binafsi na sekta za umma ili kuleta maendeleo.Nikichaguliwa nitaunganisha na kuletea umoja ili ushirikiano ule uweze kukuza uchumi.

- Nikichaguliwa kuwa Rais lazma nihakikishe wakina baba wanawaheshimu wakina mama.Wakina baba muache ulevi,muache kulewa na kuwaonea wakina mama.

ELIMU:

Nikichaguliwa mkazo mkubwa utakuwa kwenye shule za Ufundi na VETA.Tutafufua vyote hivi maana ndio vinaongoza kwa kutoa ajaira.Hata kwenye viwanda wanahitaji wenye ujuzi ambao wengi wanazalishwa na vyuo hivi vya ufundi.

Michezo na sanaa;

Nikichaguliwa nitafanya
- Nitasimamia kuondoa zana kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kuwa tunakuwa wa mwisho kwenye michezo

- Tutafungua vyuo vya michezo mbalimbali na kuwaandaa wanamichezo.

Maigizo; Tutahakikisha kuwa tunawasimamia ili mpate haki zenu za msingi kama Hatimiliki,tatutawalinda kwa nguvu zote.

UTAWALA BORA: Nikichaguliwa nitasimamia....
1.Rushwa: Anayetoa rushwa ana makosa na anayepokea ana makosa, tutakibadilisha hiki kifungu na kumbana yule Anayepokea,aliyeomba(Anatoa mifano Scenario)

- Anawaasa watu kuwa waweze kutoa taarifa za rushwa kuliko kukaa kimya huku mambo yakiharibika.Anawaambia waandishi wa habari kufichua mianya ya rushwa kutoa taarifa na kuiachia polisi kufanya kazi yake.

-Anasema hatafumbia macho mla rushwa,lazma nchi hii tuiweke kwenye mstari wa mwalimu Nyerere,Mwinyi, Mkapa na Kikwete.Lazma tuiweke kwenye misingi bora. Anasema wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi watalipa tu hizo kodi.Nichague mimi ili niweze kusimamia serikali yenye uadilifu.

* Anamalizia kwa kuwashukuru wa kumsikiliza.

Naweka nia kugombea Urais awamu ya tano.Chama cha CCM kina marafiki wengi sana njee ya mipaka ya Tanzania( Anataja Vyama rafiki vya CCM duniani.) Lazma chama tukijenge,lazma chama chetu kichaguliwe mwaka 2015.

*Anawaonea huruma wenzao (Upinzani) kuwa tokea mfumo wa vyama vingi hawajawahi kushinda urais.

-Anawashangaa kuwa kila uchaguzi wanaweka mgombea yule yule ambaye anakuwa kama mfalme pamoja nauongozi wake kushindwa urais mara kwa mara.

- Kila uchaguzi wanasingizia kuibiwa kura.

- Anasema kuwa wale wafalme hawataki kuachia ngazi na kubadilisha uongozi wa kifalme( Anaelezea sokosoko utakalopata kama ukitaka kugombea nafasi ya juu na kuitwa msaliti mamluki).

- Anasema uongozi ule ule unaoshindwa miaka yote hawawezi kushinda,watachapwa asubuhi mapema.

- Anasema kuwa wao wanabadilisha Magamba kuanzia kwa Mwalimu Nyerere,Mzee Mwingi,Mzee Mkapa na mpaka sasa Rais Kikwete. Hivyo lazma waendelee kushinda.

-Nchi hii itakuwa salama endapo Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwa madarakani.Tunahitaji Rais muadilifu,mwenye nia ya dhati,mwenye maono.

- Naomba mnisindikize kwenye jengo kubwa,jeupe,jengo la Ikulu ili twende tukamalizie ambapo pale mzee Kikwete ameishia.

Anamalizia kwa kuimba nyimbo ya Kimwera.

**********************************

-Mama Membe ameingia Jukwaa kuu na kuwasalimu wananchi.

- Sasa hivi ameingia Peter Mshechu kuburudisha, Amebadilisha mashairi ya wimbo wa "NYOTA ING'ARE"

Nyota na ing'are Membe

*******************

- Kuna wasanii mbalimbali wa Bongo Movie.(Steve Nyerere,Mkwere,Ray Kigosi,Tino,Swebe,Dude,Safina,JB, na wengineo)

-Anaongea Steve Nyerere kwa kuiga sauti mbalimbali za viongozi mbalimbali kitaifa.

- Anaongea Mlugaluga kwa kuiga sauti mbalimbali pia za viongozi.

- Sasa ni wasaa wa Kupiga picha na Mh. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mkutano umefana sana,watu walikuwa wengi na hotuba imevutia sana.

*Mh. Membe anaaga wananchi na Kuondoka katika viwanja vya CCM mkoa wa Lindi.

MWISHO
 
Hakika UKAWA wanayo kazi yani wanapigwa kutoka kila mkoa leo watapigwa kutoka Lindi na baadae watapigwa kutoka Dar....! Bavicha hawana jinsi inabidi wacheze ngoma ya CCM maana sasa wameamini Rais wa nchi hii lazima atoke CCM!

Aisee. Sasa hapo Membe anapambana na UKAWA? Membe anatakiwa acheze mechi tatu ndo aingie fainali na UKAWA.Mechi na CC, Mechi na NEC na Mechi na CCM GA.
 
Hakika UKAWA wanayo kazi yani wanapigwa kutoka kila mkoa leo watapigwa kutoka Lindi na baadae watapigwa kutoka Dar....! Bavicha hawana jinsi inabidi wacheze ngoma ya CCM maana sasa wameamini Rais wa nchi hii lazima atoke CCM!
UKAWA tunaheshimu hadhi ya cheo cha rais sio CCM ambao wamekifanya kama sehemu ya kujifunzia siasa hadi watoto wa shule wa miaka 20 nao wametangaza.
 
Atatangaza na wale maadau zake 11.leo??

Aisee nitamshangaa mtanazaia atakae poteza saa 24 za kujiandikisha kwenye bvr

Aje apoteza saa zaidi ya sita kupiga kura alafu mtanzania huyu aipigie kura ccm hii iliyojaa wezi na mafisadi wala rushwa

Nitashangaa sana,ni heri kutokupiga kura!!
 
Aisee. Sasa hapo Membe anapambana na UKAWA? Membe anatakiwa acheze mechi tatu ndo aingie fainali na UKAWA.Mechi na CC, Mechi na NEC na Mechi na CCM GA.

Wakati Yeye Akijianda Kucheza Hizo Mechi Zake Tatu Ulizomtajia Hapo Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo Kaisha Maliza Ligi Nzima Na Ndiyo Rais.
 
Mbona Ratiba Zake Zinabadilika Badilika Kama Mwanamke Mjamzito Anayekaribia Kujifungua? au Ndiyo Miiko Ya Kiuganga Na Kiuchawi Hiyo?
 
Mwenyewe nipo live nafuatilia.
Lakini style ni ile ile ya ukusanyaji watu. kama si mfalme Mzee Yussuf ..................
 
Kweli mtu wa Pwani ni wa Pwani tu,yaani Ni kama kigodoro fulani cha kumtoa mwali.Hawa ndio tuwape Urais?
 
Back
Top Bottom