Kutoka Uwanja wa Taifa: Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC Vs Azam FC

kama kawaida simba wamenunua mechi. simba wanaharibu sana ladha ya soka la tanzania ndio maana Watanzania wanaifuatilia yanga timu ya wananchi
Hii ni dalili ya kushindwa simba ikipata ushindi imenunua yanga ikishinda imeshinda kihalali

Kubali tuu mkuu kuwa simba wanaweza

Subiri game ya simba na yanga utajua tu kama wananunua au lah
 
Ametoka Kahata ameingia Ajibu upande wa Simba SC
 
Simba SC wameweka kambi lango la Azam FC zikiwa zimesalia dakika 3 kumalizika kwa mchezo huu.
 
90+3 kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa VPL

Ni goal kick kuelekea lango la Azam FC refa anaangalia saa yake

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ambapo Simba SC anaibuka na ushindi wa bao moja bila likiwekwa kimiani na Meddie Kagere kunako dakika ya 49 hivyo kwa matokeo haya Simba imejikita kileleni kwa alama 15 kwa michezo 5.

Simba SC 1-0 Azam FC
 
Wouzeeeerrrr
 
Mwana kulitaka mwana kulipewa,

Hongera mnyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…