Kutoka Singida: Rais Magufuli aweka jiwe la Msingi ujenzi daraja la Sibiti; akemea viongozi kuchongeana

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Mubashara muda huu kutoka Singida, Rais Magufuli anaweka jiwe la msingi daraja la Sibiti linalounganisha mikoa ya Singida, Simiyu na Mara.

Sibiti1.jpg


Daraja hili ni kubwa kama lile la Mkapa linalounganisha mikoa ya kusini. Daraja hili lina changamoto nyingi lakini Rais anaahidi kulikamilisha bila kukosa.

Rais anasema wataalam wameeleza changamoto za kushindwa kukamilisha ujenzi wa daraja hili kwa wakati lakini anasema nakataa sababu hizo, kwani mkandarasi hakujua sababu hizo wakatia saini mikataba? Hakujua wakati anakubali kufanya kazi?

Anasema mkandarasi afanye kazi usiku na mchana kazi hii iishe, anasema sitaki maneno wananchi wanataka daraja sio ahadi.

Katika upande mwingine Rais amekemea viongozi kuchongeana.

Namnukuu:

"Watendaji wangu hawa ndani ya Serikali wengi wanajitahidi sana, wanafanya kazi nzuri sana. Lakini muda mwingine wanachongewa na wanasiasa. Hili nililiona kule Serengeti Mbunge mmoja wa chama fulani anazungumza kwa mishipa imesimama kabisa kumchongea mtu fulani bila hata mkumuogopa Mungu.

Anamchongea mtu ambaye anachapa kazi sana. Kwahiyo wachapakazi hawa ndani ya Serikali saa nyingine wanachongewa. Labda anataka apeleke mradi wa maji mahali fulani Mwanasiasa mwingine anataka upelekwe mahali fulani, mradi umepangwa mahali fulani anang'ang'ania kwenda mahali fulani. Akikataa imeshakuwa nongwa. Tusifanye hivyo!"

"Watendaji niliowateua na watendaji wote ndani ya Serikali na nyinyi wananchi pamoja na madiwani na wabunge twendeni pamoja kwa sababu nyumba tunayoijenga ni moja, nia yetu ni moja!"

Mwisho wa Kunukuu.

Vilevile, Rais amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kuiombea Nchi amani. Rais Magufuli amekiri wazi kuwa yeye kama binadamu hajakamilika ila ana dhambi ndogondogo tu.

Sibiti2.JPG
 
Rais anaongea kwa uchungu na ukali mkubwa na kumtaka waziri aache mzaha. anamshangaa waziri kumtetea mkandarasi badala ya kumsimamia
 
Anasema nataka kuona watu busy kazini , magari yapishane hapa kutengeneza hili daraja, anataka wenyeji wapewe ajira ya kufanya kazi hapa
 
rais anasema barabara hii ni muhimu kwa shughuli za kiuchumi kwa nchi yetu. hii ni barabara ya kiuchumi
 
Rais Dk. John Pombe Magufuli, leo akiwa ziarani mkoani Simiyu kwenye kuweka Jiwe la Msingi la Daraja la Mto Sibiti na Barabara inayounganisha Mikoa ya Simiyu na Singida, amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kuiombea Nchi amani.
Rais Magufuli amekiri wazi kuwa, yeye kama binadamu hajakamilika ila ana dhambi ndogondogo tu.
 
kumbe anajijua ana dhambi, sasa mbna akiambiwa atubu anakuwa mbogo?
 
Back
Top Bottom