Kutoka ndani ya moyo wangu


wake hawasababishi mitafaruku Nyamayao mara nyingi wakwe wanasahau kuwa kijana anapooa lazima kuna vitu vitabadilika kama alikuwa akikwama anaomba ushauri kwa babaye au kwa mamaye sasa akioa kapata ubavu hawezi tena kukimbilia huko lazima akikwama aanzie kwa mkewe na hapo wakwe hawakubali huu ukweli kuwa sasa wao ni chaguo la pili
 
Last edited by a moderator:

wake hawasababishi mitafaruku Nyamayao mara nyingi wakwe wanasahau kuwa kijana anapooa lazima kuna vitu vitabadilika kama alikuwa akikwama anaomba ushauri kwa babaye au kwa mamaye sasa akioa kapata ubavu hawezi tena kukimbilia huko lazima akikwama aanzie kwa mkewe na hapo wakwe hawakubali huu ukweli kuwa sasa wao ni chaguo la pili
 
Last edited by a moderator:
Off course na deal na yeye tu. Ila kuna mambo mengine ukimbadili mtu, moja kwa moja unawagusa wengine, mfano budgeting malengo ya kila mwaka.

Kuna saa inabidi tu, no way out.

 
huyo dada anaweza kuwa victim tu, sababu hakubaliki kwenye familia.
Inawezekana kabisa huyo dada kaolewa na kuwa ndani kama mke ambaye hapendwi, lakini hana mchango wowote kwenye ugomvi wa wanandugu. Kaka hampendi shem, mume anampenda, chochote kitakachofanywa na nduguye itasemwa ni sababu mke hapendeki....... ni kizaazaa.
 
Dada kubwa karibu!
Mno!

Hii mada hii!
Tukiolewa huwa tunabebeshwa makubwa sana nafkir kuliko uwezo hata ya waliotutangulia kwenye familia hizo
Kwa mfano familia isiyojebgwa kweny misingi ya upendo tu toka wanazaliwa na kulelewa na wazazi wao,kweli akiolewa binti wale ndugu wasipojaliana lawama ni kwa mke?.(hapa naongea kama mke)

.
Halaaaafu mwanaume uliye na misingi yako ya kibaba inakuwaje unakubali kubadilishwa uelekeo wako kwa ndugu zako na mke(hapa naongea kama wifi.)
 
Ha ha ha ha, unamaanisha familia inakuwa ilishasambaratika hata kabla ya mke kuolewa? Hii ina ukweli bana.

 
...hii yote inatokana na dhana ya kwamba nani ana haki zaidi juu yako (Mume)...

1. Mama mzazi anajiona yeye kalea mimba, amezaa na kuteseka na ulezi wa kichanga mpaka kufikia kutembea, kusema na mwishowe kujitegemea...
2. Madada (Mawifi) hawa huona wao ni ndugu toka nitoke....wamezaliwa tumbo moja na ndugu yao, wanajihisi wanauchungu wa damu kuliko weye Mke mtu baki tu ambaye hata ukiachika ataolewa mwingine...
3. Mke, ....huyu anajiona yeye ndiye aliyechaguliwa kuwa mama wa watoto wa huyo Bwana Mkubwa, Mwenza na mengineyo mengi yakiwemo faragha faraghani....!

Ni ubinafsi na "wivu" wa kijinga tu ambao wanawake wengi wamejaaliwa nao!
watu kutojua mipaka yao.


Au mnasemaje Dark City swahiba,.. King'asti, AshaDii, MwanajamiiOne, TIMING, et al?
 

hao wakwe wa kusahau hilo lazima nao wanashida, mkioana lazima kila mmoja wenu atabadilika kwa namna moja au nyingine, na hapa hatuzungumzii ushauri wa kawaida tuseme kimaendeleo hivi, mana wazazi wanajua sasa kijana wetu ameoa tunategemea afanye maendeleo na mwali kwa mfano, hata msipowashirikisha kwenye ushauri wa namna hii kwao ni poa tu mana wanaona maendeleo, tuje kwenye mitafaruku, hapa ndio shida iliyopo, nimesema tunachangia kwa namna fulani, wanawake tumeumbwa na kawivu fulani, naonaga hata kwa wifi yangu (dada wa msukuma) msukuma akisaidia kwetu wifi atalinyanyua na kulikuza, oohh naona anazidi kutawaliwa, oohh siku hizi ukimuomba kaka hela hakupi lakini kwa wakwe zake kafanya hivi na vile, mie kwangu hata msukuma afanyaje kwao/kwa ndugu zake wala mshipa haunichezi naona kama ni wajibu wake, nimekutolea mfano tu unaona huyu wifi yangu anachonifanyia nikiamua kuingilia kati hapa nina hakika nitasababisha mtafaruku mkubwa especialy pale anaponiambiaga hebu sasa hivi lipa fees mimi nimalizie kitu fulani ninachokifanya kwa wazee, ninaweza kugoma kulipa kwamba na mie kwetu ukifanya kitu nasimangwa na kwenu, unaona hapo? jamani, familia zote tuheshimiane.
 

...umeongea jambo la maana sana,
ni jukumu letu wanaume 'kumlinda' mke na hao ndugu.
Wakati huo huo, ni jukumu letu pia kulinda hadhi ya familia kwa huyo mke,
sio mwanaume unakuwa haujitambui,...unapelekeshwa tu kama bendera fata upepo!

​

Kwenye ndoa hakuna classes kusema ati mama mzazi ndio 1st Class, 2nd Class mawifi, na 3rd Class Mkeo
au Vice Versa...! Kwenye ndoa kila mtu ana mipaka yake, na hiyo mipaka izingatiwe na kuheshimiwa hata ikibidi
kwa 'kununiana!'
 
Off course na deal na yeye tu. Ila kuna mambo mengine ukimbadili mtu, moja kwa moja unawagusa wengine, mfano budgeting malengo ya kila mwaka.

Kuna saa inabidi tu, no way out.

ndio mana nikasema, tufanye yale tunayostahili, yaliyo na malengo/hekima/msaada kwetu, hakuna anaeweza kumpendeza/kumfurahisha/ridhisha kila binadam chini ya jua, unafanya kila unaloona unastahili kulifanya kwa faida yako na familia yako,( kwani nani anataka mateso bwana) mie ukiniambia nianzie ishu kwa mfano nilioutolea hapo juu wa wifi yangu naona kama najipotezea muda wangu tu, na mtafaruku usio na kiuno wala kichwa, maneno yapo tu mie sijali sana sana nasikilizwa, familia yangu inatimiziwa mahitaji maalum, maendeleo nayaona, mengine wamalizie yao, na familia ya msukuma inanijua vizuri sana inapokuja suala la wao kucheza na familia yangu.
 

yap, ni kizaazaa kiukweli, yote yawezekana, lakini kutokana na hili mwanamke ulishindwa kucheza nafasi yako kunusuru haya yasitokee? nimesoma pia wamehama kwenye villa waliyokuwa wanaishi pamoja, sasa wewe mwanamke unaejua una ishu na hii familia ungecheza part yako kuweka mambo sawa ili wao ndio wajione wajinga, sidhani kama kuna mwanamke aliyeolewa hajapitia kashkash za ndoa, kama wapo wamebarikiwa, mie nilipitia na wifi/mama mkwe, mgogoro haswaaaa, lakini nilipambana baba mkwe wangu ni bonge la muelewa alinisaidia sana katika kizaazaa nilichopitia, hapo ningesema ninunue kesi ingekuwa mtafaruku mkubwa sana,msukuma alikuwa hakubaliani na mama/dada yake hata kidogo, na kama sio mimi kumtuliza ingeshazaa mtafakuru haswaa, nililaumiwa kwa kila namna lakini nilipambana na sasa hivi ni marafiki zangu wakubwa sana, tunapopitia changamoto kwenye ndoa tusizikuze/chochea, bali tuangalie namna ya kupambana nazo.
 
Mdogo wangu asante sana.....
kama wifi nimefaulu, tena kwa kiwango cha juuuuuuu saaaanaaaaaaa. kwetu mimi huwa ni kimbilio la mawifi.....
Namwomba Mungu anisaidie niwe hivyo kwa wakamwana, lol!
Tukomae tu mdogo wangu, ndo dunia ilivyo
 
Ha ha ha ha, unamaanisha familia inakuwa ilishasambaratika hata kabla ya mke kuolewa? Hii ina ukweli bana.
ila sasa zamani hizo walikuwa wanashindwa kulaumiana, sasa wanakuwa wamepata mchawi wa kumsingizia
 
Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?
hata mke/mume siyo mmiliki wa mwenzi wake, mmiliki ni Mungu pekee ndo maana anakuleta na kukuchukua siku anayoitaka yeye.
Malezi yanakuwepo kwa zamu. Mama anaanza..... baba/dada/shangazi n.k wanaendelea...... mume/mke anamalizia. tumia ujuzi wako woote kumlea mtu anapokuwa mikononi mwako, akiondoka kubali kuwa sasa ni zamu ya wengine kulea.
Kuna kaswali najiulizaga, hivi wazazi wa wanawake huwa hawana uchungu na watoto wao? mbona hakuna migogoro hii ya kijinga inayotoka huko? binti akishaolewa wazazi hujiweka kando kabisaaaaaa.
Lile swala la kuacha baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzio huwa ni kwa wamama tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…