Kutoka Mahakama Kuu Dar: Bodi ya Wadhamini ya Prof. Lipumba yashindwa kesi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Mahakama Kuu imetengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa chama cha CUF wa kambi ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba

======

Dar es Salaam. Mahakama Kuu imetengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) wa kambi ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Februari 18, 2019 na Jaji Dk Benhajj Masoud baada ya kubatilisha uteuzi wao.

Vile vile Jaji Masoud amesema majina yaliyokuwa yamependekezwa na kambi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad hawakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi hiyo kwa kuwa nao hakuwa wamekidhi matakwa ya sheria.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu uamuzi huo, mmoja wa mawakili wa CUF kambi ya Maalim Seif, Juma Nassoro amesema kwa uamuzi huo, wajumbe wa bodi waliokuwepo wanaendelea na majukumu yao licha ya kwamba muda wao umeshaisha hadi hapo wajumbe wengine watakapoteuliwa.

Mbunge wa Malindi (CUF) Ally Saleh alifungua kesi hiyo akipinga uamuzi wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) wa kuwaidhinisha wajumbe waliopendekezwa na kambi ya Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo.

======

MAHAKAMA KUU YAIFUTA BODI FEKI YA WADHAMINI YA LIPUMBA ILIYOSAJILIWA NA RITA KWA SHINIKIZO LA MSAJILI JAJI MUTUNGI:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
OFFICE OF THE SECRETARY GENERAL

MAELEZO YA KATIBU MKUU WA CUF, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, LEO TAREHE 18/2/2019 ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA WABUNGE WA CUF MAGOMENI, DAR ES SALAAM;

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) kimepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Masjala Kuu ya Dar es Salaam) chini ya Mheshimiwa Jaji Benhajj Masoud uliotolewa leo hii kuhusiana na Shauri Na. 13/2017 lililofunguliwa na Mbunge wetu, Mhe. Ally Saleh dhidi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency and Trusteeship Agency - RITA) na Wadaiwa wengine 17 ambapo kimsingi imetoa Tamko la Kisheria (Declaratory Decree) kwamba RITA haikufuata taratibu katika kusajili wale waliodaiwa kuwa ni Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CUF waliosajiliwa na RITA tarehe 12 Juni, 2017 ambao waliwasilishwa na Prof. Ibrahim Lipumba na Magdalena Sakaya na kudhaminiwa na Msajili wa vyama vya siasa.

Uamuzi wa Mahakama Kuu chini ya Mheshimiwa Jaji Benhajj Masoud kueleza kwamba RITA haikuzingatia matakwa ya kifungu cha 17 cha Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini (Trustees Incorporation Act – Cap 318 RE 2002) umekata mzizi wa fitina kuhusiana na madai yetu tuliyokuwa tukiyasema tokea awali kwamba RITA haikuwa sahihi kusajili watu waliopitishwa na kikundi kilichojiita Baraza Kuu la Uongozi la Taifa bila ya kujiridhisha iwapo kweli kikundi hicho kilikuwa ni Baraza Kuu halali la Uongozi la Taifa la CUF.
Mahakama Kuu imetamka wazi kwamba mbali ya kwamba ni masharti ya kifugu cha 17 cha Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini (Trustees Incorporation Act – Cap 318 RE 2002) kwamba RITA inapaswa isimamie (monitor) kikao kinachopitisha Wadhamini wa taasisi yoyote lakini kwa mazingira ya CUF ambapo kuna kambi mbili zinazokinzana, walipaswa kujiridhisha zaidi kuhusu uhalali wa chombo kilichopitisha Wadhamini . Kwa ufupi Mahakama Kuu imetamka kuifuta rasmi Bodi feki ya Lipumba na kikundi chake na kuitanabahisha RITA kwamba ifanye kazi zake kwa kuzingatia sheria.

CUF tumezingatia pia maelezo aliyotoa Jaji Benhajj Masoud kwamba pamoja na kutotakiwa kujielekeza kuhusu hadhi (status) ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF lakini kupitia ushahidi uliotolewa alielewa kwamba muda wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini waliokuwepo kabla ya tarehe 12 Juni, 2017 ulikuwa haujamalizika na kwamba unamalizika mwaka huu wa 2019.

Kufuatia uamuzi huu wa leo wa Mahakama Kuu, CUF tunamuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum wa fedha za ruzuku (ambazo ni fedha za walipa kodi wa Tanzania) zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa Lipumba na genge lake kupitia Bodi yao feki ya Wadhamini katika kipindi chote ambacho Msajili huyo na RITA waliipa uhalali Bodi hiyo wakitambua kwamba haikuwa halali.
Kwa hatua ya sasa itoshe kusema haya kuhusiana na uamuzi huo. Maelezo zaidi yatataolewa katika siku zinazofuata.
Nikiwa Katibu Mkuu wa CUF napenda kumpongeza kwa namna ya pekee Mhe. Ally Saleh (Mbunge wa Malindi – CUF) kwa kuchukua hatua ya kufungua shauri hili ambalo limeondosha utata uliokuwepo kuhusu Bodi ya Wadhamini ya Chama chetu. Mhe. Ally Saleh amekifanyia Chama kazi kubwa sana na ya kuheshimika na kuthaminika. Tunamwambia Ahsante sana.

Pia tunawashukuru kwa dhati Timu ya Mawakili wetu waliosimamia Shauri hili ambao ni Mhe. Mpare Kaba Mpoki, Mhe. Fatma Amani Karume, Mhe. Juma Nassoro Dovutwa, Mhe. Daimu Halfani, na Mhe. Loveness Denis kwa uweledi, umahiri na umakini mkubwa waliouonesha hadi kufikia mafanikio haya.

Shukrani nyengine zimwendee Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu, Mhe. Joran Bashange, kwa kujitolea kwa nguvu zake zote kusimamia bila ya kuchoka shauri hili na mashauri mengine yaliyofunguliwa na Chama. Tunawashukuru pia mashahidi wote waliosimama upande wa Chama kutoa ushahidi katika shauri hili. Kwa wote hao tunawaambia

Ahsante sana.

Napenda pia kuwapongeza sana wanachama wa CUF kwa uamuzi huu muhimu wa leo. Kwa niaba ya viongozi wenzangu nawataka waendelee kuwa watulivu wakisubiri uamuzi wa Shauri Na. 23/2016 ambao utatolewa siku ya Ijumaa ya tarehe 22 Februari, 2019.

Nilisema tokea awali kwamba tutaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na Mahakama na kwamba tumejiandaa kwa maamuzi yoyote. Bado tunasimamia msimamo wetu huo.

HAKI SAWA KWA WOTE

SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU – CUF

Imetolewa leo tarehe 18 Februari, 2019
 
Mbona tetesi za hongo zilitembea sana jana ziki wahusisha wakubwa serikalini?

Nivyema tukanyamaza kwanza kabla ya kuhukumu wengine kwa tuhuma zisizo na ushahidi. Nikweli cuf walifungua kesi kutafuta haki mahakamani. Lakini mtu 1 anakurupukatu nakutoa tuhuma zawazi kwa wengine siyo jambo zuri. Tuwe waungwana wakati mwingine.

nimalizie kwa kuupongeza upande ulioshinda kesi. Tunaweza kushindana kwa hoja na sio vihoja.
 
Lipumba msidhani kashindwa hajashindwa, yeye kashinda kwa njia msiyojua , yeye kashafanikisha lengo lake la wakati Ule, mpaka sasa huwezi amini No cuf at all , ni cuf mabendera tu,
Lakini baadae CUF inaweza kua imara kuliko wakati wowote baada ya haibu ya lipumba maana yake sasa lipumba sio mwenyekiti baada ya maamuzi hayo labda kwa haraka Rais atatia sahihi ile sheria ili ianze kutumika kwa kukifuta Cuf au kumvua maalim uanachama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa kazi ya Lipumba ishamalizika aliyoagizwa, ndo maana siyo CCM wala lipumba wanaoumia kwa maamuzi ya Leo ya mahakama, hata Jaji Mutungi haumii wala hajutii kwa Lolote, ndo maana mipango ya kuivuruga CUF ilikuwa na umuhimu wakati ule wala si wakati huu
 
Mbona tetesi za hongo zilitembea sana jana ziki wahusisha wakubwa serikalini?

Nivyema tukanyamaza kwanza kabla ya kuhukumu wengine kwa tuhuma zisizo na ushahidi. Nikweli cuf walifungua kesi kutafuta haki mahakamani. Lakini mtu 1 anakurupukatu nakutoa tuhuma zawazi kwa wengine siyo jambo zuri. Tuwe waungwana wakati mwingine.

nimalizie kwa kuupongeza upande ulioshinda kesi. Tunaweza kushindana kwa hoja na sio vihoja.
Bila tuhuma hizo, The vice versa was true.

Ni kweli Mkuu
 
Kwa sasa kazi ya Lipumba ishamalizika aliyoagizwa, ndo maana siyo CCM wala lipumba wanaoumia kwa maamuzi ya Leo ya mahakama, hata Jaji Mutungi haumii wala hajutii kwa Lolote, ndo maana mipango ya kuivuruga CUF ilikuwa na umuhimu wakati ule wala si wakati huu
Tunaangalia mbele yalipoita si ndwele ndiyo siasa yenyewe.
 
Back
Top Bottom